Sunday, December 8, 2013

Mamia wajitokeza Kumsikiliza Dr Slaa kwenye Mkutano wa Chadema Kasulu

Pamoja na Mbinu Chafu za Kutaka Kuvuruga Mkutano wa Chadema Kasulu Uliokuwa Unahutubiwa na Dr Slaa, lakini wananchi wengi wa Kasulu walijitokeza kumsikiliza Dr Slaa na kufurahishwa na hotuba yake iliyobeba maneno ya kuwapa Matumaini. Kulikuwa na kikundi cha Vijana wapatao kumi wenye mabango ambayo yaliandaliwa mahsusi ili yatumike kuvuruga mkutano huo lakini mbinu zao chafu zimeshindikana. Ili kuzima mipango yao michafu vijana hao walipewa fursa ya kukaa mbele na mabango yao yenye ujumbe wa kuwaponda viongozi wa Chadema. Vijana hao walipewa fursa hiyo ili kuonyesha kwamba Chadema kinaendeshwa kwa Demokrasia ya kumruhusu mwanachadema yeyote kutoa mawazo yake anayopenda ili kudumisha Demokrasia ndani ya Chama.
Dr Slaa akihutubia katika Mkutano uliofanyika  Kasulu, Kigoma

Dr Slaa akiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kitanga, Kigoma.


2 comments:

  1. Kuna taarifa za kutokea vurugu zilizo pelekea kuvunjika kwa mkutano na kwamba Dr alirushiwa mawe, naomba kujuzwa zaidi!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo kweli kamanda,mimi nilikuwepo kwenye mkutano hapa kasulu mwanzo mwisho,kilichotokea vijana wa ccm wameshughulikiwa na polisi.Ni propaganda za magazeti ya ccm uhuru,habari leo,jambo leo,rai na mitandao ya kinafiki

      Delete