CHADEMA Kanda ya Kaskazini, inawatangazia umma wote kuwa,
Ndugu ABDI SHEKIMWAGA amesimamishwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Bumbuli
kuanzia 21 Desemba 2013.
Ofisi ya kanda, ilipokea nakala ya taarifa na miniti ya
kikao kilichoketi tarehe 22 septemba 2013 kutoka kamati tendaji ya wilaya/jimbo
pamoja na nakala ya barua ya tuhuma alizoandikiwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA ili
ajieleze na kujibu, ikiwemo na barua ya tarehe 12 Desemba 2013 aliyoandikiwa
katibu wa mkoa kujulishwa mapendekezo na hatua za kunusuru chama dhidi ya hila
mbaya zilizokuwa zinafanywa na ABDI SHEKIMWAGA. Kwa bahati mbaya sana ndugu
SHEKIMWAGA alitoa maneno ya kashfa na dharau pamoja na kutumia lugha isiyofaa
kwa viongozi na kuamua kugoma kujibu barua ya tuhama hizo.
Uongozi wa Kanda baada ya kupitia taarifa hizi na baada
ya kufanya kikao cha pamoja na viongozi wa wilaya tarehe 21 Desemba 2013 huko
wilaya lushoto mkoani Tanga, unamtangaza ndugu SHEKIMWAGA kuwa kwa kukinisuru
chama dhidi ya tuhuma dhidi yake, kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa tuhuma
dhidi yake, kwa ajili ya hofu na kutokuwa na imani kulikoonyeshwa na viongozi
na wanachama wenzake AMESIMAMISHWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA KUANZIA TAREHE 21
DESEMBA 2013. Hatua hii ni ya kuzingatia pendekezo la kamati tendaji ya
wilaya/jimbo kwa mujibu wa ibara ya 6.3.4 (c), “amekoma kuwa kiongozi kwa
kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni na
maadili ua chama”.
Aidha uongozi wa kanda, unaliagiza baraza la uongozi la
mkoa ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa wilaya/jmbo kwa mujibu wa katiba ya
chama ibara ya 6.3.6 (a) sehemu (iV) kuwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA APEWE FURSA
NYINGINE TENA akiwa katika hali ya kusimamishwa uongozi kwa kuandikiwa barua
tena ya tuhuma dhidi yake na apewe muda wa kikatiba kujibu ama sivyo hatua kali
zichukuliwe dhidi yake. Tuhuma hizo ni;
1.
Kuamua kwa makusudi kuzuia na kukwamisha
kazi za CHAMA, programu ya CHADEMA ni msingi. Ndugu SHEKIMWAGA ametoa maneno ya
uzushi na upotoshaji kwa uwazi mbele ya viongozi wenzake na maafisa wa kanda
kuwa hayuko tayari kufanya kazi ambayo yeyé aliitafsiri kuwa ina lengo la
kumjengea mtu fulani mtandao ndani ya chama. Hii ni kinyume na kanuni ya
maadili ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (viii)
2.
Ametoa lugha na matamshi yenye kuonyesha
udini na ukabila mbele ya viongozi wenzake na mbele ya maafisa wa kanda kuwa
kaimu katibu wa CHADEMA mkoa wa Tanga ndugu Jonathan Leonard Baweje kuwa ni
Mkristo na ametokea mkoa wa Kigoma hivyo hawezi kuwa katibu wa mkoa wa Tanga
kwa sababu sio muislam. Hii ni dhambi mbaya sana na ni kinyume na kanuni ya
maadili ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (iv), “Kiongozi
yoyote asijihusishe na vikundi vyovyote vyenye misingi ya ukabila, udini, au
ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama au miongozi mwa jamii
kisiasa au kijamii”.
3.
Amejitambulisha wazi mbele ya viongozi
wenzake na mbele ya maafisa wa kanda kuwa yeyé yupo kundi la Zito Kabwe na
atahakikisha CHADEMA inakufa Bumbuli iwapo maamuzi ya kamati kuu ya kumvua
uongozi Zito Kabwe hayatabadilishwa. Kitendo hiki cha kujitengenezea makundi na
upotoshaji ni kinyume na kanuni ya maadili ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za
chama sura ya 10.1. (iv), “Ni mwiko kwa kiongozi kujihusisha na
upotoshaji wa maamuzi halali ya vikao vya chama”.
4.
Amezuia kwa makusudi kazi za chama na
amekuwa akifanya hujuma dhidi ya viongozi wengine ambao wamekuwa wakifanya kazi
za chama. Sambamba na hili ametuhumiwa kuwa anashirikiana na wapinzani wetu CCM
katika kuhujumu chama na kwa kumwaga sumu na maneno ya uongo. Kitendo hiki
kimekuwa sababu ya kuzuka kwa migogoro isiyokwisha katika jimbo la bumbuli na
imeendelea kuvunja moyo na kuleta mifarakano inayorudisha nyuma kazi za chama.
Jambo hili ni kinyume na kununi ya maadili ya uongozi na uendeshaji wa kazi za
chama sura ya 10.1 (ix), “Kiongozi asijihusishe au kushiriki na
vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa
chama au wanachama wake”.
Taarifa hii inaenda sambamba
na ndugu ABDI SHEKIMWAGA kukabidhi vifaa vyote vya chama, ikiwemo kadi za chama
mpya zipatazo 400 zenye thamani ya Tshs 600,000 ndani ya siku TATU kuanzia
tarehe ya taarifa hii kwa KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA.
CHADEMA Kanda ya Kaskazini
inaendelea kuonya kuwa haitavulia kabisa kuona CHAMA CHETU ambacho ni tumaini
kwa Watanzania wengi kikivurugwa na watu wachache wenye hila mbaya na chafu.
Aidha nitoe rai kwa WanaCHADEMA wote wa kanda ya kaskazini na Watanzania
wapenda haki na kweli wasiwe na hofu yoyote na matukio haya ya kukisafisha
chama maana hatuna budi kusafisha na kufukuza bundi wote waondoke.
Imetolewa
leo tarehe 24 Desemba 2013
Amani Golugwa
Katibu wa
CHADEMA – KANDA YA KASKAZINI.
Makao Makuu ya Kanda – Arusha, Tanzania:
Simu: +255 754 912 914
No comments:
Post a Comment