NCHI za Afrika zinahitaji mabadiliko katika mfumo wa ulipaji kodi kwa faida ya maendeleo kwa kuwa ni nchi zinazoendelea.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe huko Marekani wakati akihutubia mkutano kuhusu masuala ya kodi na uchumi.
Zitto alisema nchi zilizoendelea zinapaswa kukubaliana na kubadilishana utaalamu kuhusu masuala ya kodi na nchi zinazoendelea.
Alisema sheria ya kodi duniani inaeleza wazi kwamba nchi yoyote itoe taarifa ya kodi zake kwa makampuni ya kimataifa ili wawekezaji wanapowekeza waweze kulipa kodi kwa haki kulingana na eneo husika.
Hata hivyo, alisema kwa sasa wataalamu wa Umoja wa Mataifa kupitia kamati ya masuala ya kodi wanajadili sheria mpya juu ya mkataba wa kodi kwa nchi mbili kati ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea.
Zitto alisema nchi za Afrika hazina haja ya kamati ya kuwa na wataalamu bali ukweli unabaki pale pale kwamba serikali inapaswa kukabiliana na suala la mkataba wa kimataifa juu ya kodi kuliko kuwa na mikataba baina ya nchi miongoni mwa nchi.
Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) alisema zaidi ya miongo mitano sasa, Afrika mjadala wa maendeleo umekuwa unaongozwa na hadithi moja yenye jina ‘Misaada ya Nje’
No comments:
Post a Comment