Saturday, November 30, 2013

Nitapambana na Abood - Afande Sele

Msanii wa kizazi kipya, mfalme wa rymes, Selemani msindi a.k.a baba tunda, simba dume, AFANDE SELE amesema sasa yupo tayari kwaajili ya mapambano ya kweli katika kuhakikisha jimbo la morogoro linapata kile walichokikosa kwa miaka 50 sasa. 

Akizungumza ofisin ya chadema kata ya msufini, mkali huyo mwenye nyimbo za kuelimisha kasema sasa watanzania twahitaji kubadilika na kuangalia mbele kwani ni muda mrefu sasa tumechoshwa na unyanyasaji wa uongozi wa ccm, tumehaidiwa mengi na bwana mkuu lkn hakuna anachokitekeleza zaidi ya kutembea nchi za watu.

Anasema taifa haliwezi kuendelea kwa kuomba misaada nchi za nje bali kwa jasho la mtanzania mwenyewe ambaye atapata elimu bora itakayo mwezesha kujiajiri mwenyewe na sio mfumo wa sasa wa elimu unao tegemea ajira kutoka serikalini. Akiongeza kua nimejiunga chadema kupambana na wasiopenda haki na demokrasia, wasiojali utu na umasikini wa mtanzania, wasiojua shida ninin hasa, wasio jua uchungu wa vifo vya wa mama wajawazito na watoto wanaokufa kwa malari kutokana na huduma duni zinazo tolewa na serikali isiyowajali watu wake kwa mda mrefu tangu serikali ya awamu ya tatu.

Anasema sasa yupo fiti kuungana na watanzania wapenda haki na wanademokrasia kuzunguka nchi nzima kuelimisha jamii kuhusu serikali hii mbovu ya ccm.Akizungumzia mgoogoro unaokikumba chama anasema ni vema mh.zitto akawa mpole na kujishusha ilikufikisha chama salama,, anaongeza kuwa haoni sababu ya malumbano yasio kuwa ya msingi hasa wakati huu ambao tunaukaribia uchaguzi wa serikali za mtaa kwahiyo ni bora zitto akapatana na mwenyekiti wake ili tutimize ndoto ya watanzania 215.

Akizungumzia nia yake yakugombea ubunge jimbo la morogoro mjini anasema watakavyoona wananchi ndivyo atakavyo fanya yeye kwani anatamani jimbo hilo lisiwe chini ya ccm 2015 tena chini ya abood.Anasema abood kageuka kuwa mfazili na sio mbunge wakupeleka matatizo ya wananchi bungeni, wananchi wa morogoro hawataki msaada wa magari ya kusafirisha maiti kwakuwa hata iwevipi maiti haiwezi kuozea ndani kisa hakuna ufadhili wa magari ya abood na nitahakikisha abood analiacha jimbo hilo kwa watu wanaojali utu wa mtanzania, aliongeza afande sele. 

1 comment:

  1. afande sele a.k.a simba dume nimemsanii anayejitambua ni msanii kioo cha jamii ni msainii mwenye maadili ni msanii mwanaharakati ni msainii muelimishaji ni msanii aliyepitia shida nyingi hadi hapo alipofika ni msanii mwenye busara na hekima ni msanii anayependa nchi yake ni msanii mzalendo msanii huyu anasifa zote za kutuwakilisha bungeni mwaka 2015 jimbo la morogoro kwa sasa watanzania tumechoka kuongozwa na degree, diploma, master, phd wala certificate tunataka kuongozwa na busara na hekima aliyonayo afande sele, tukumbuke wafalme wazamani waliongozwa na hekima katika kuwaongoza watu wao hawakuwa na degree ambazo zinatolewa na watu bali hekima itokayo kwa mungu ndiyo ilikuwa silaha yao.ndugu zangu watanzania na wana morogoro tutumie macho ya kiroho ilituweze kuchagua viongozi wazuri 2015 watakao linusulu taifa letu.

    ReplyDelete