Saturday, November 16, 2013

CHADEMA Arusha yanyakua kiti cha Naibu Meya

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jiji la Arusha,kimeshinda uchaguzi mdogo wa kiti cha unaibu Meya wa Jiji hilo. Katika uchaguzi huo,mgombea wa Chadema, Diwani wa Daraja Mbili, Prosper Msofe, alichaguliwa kushika nafasi hiyo,baada ya kupata kura 25, kati ya kura 28, huku mbili za hapana, na moja iliharibika. Chama cha Mapinduzi (CCM) hawakusimamisha mgombea, huku chama cha TLP, chenye Diwani mmoja, Michael Kivuyo ambaye awali alitangaza kugombea lakini alipima upepo na kuamua kujitoa kabla uchaguzi kufanyika.

1 comment:

  1. Ccm wanabana wanabana lakini Arusha wameachia mavi debe!

    ReplyDelete