Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kimefungua rasmi
Tawi lake katika Jimbo la Ohio Marekani Siku ya Jumamosi tarehe 26 Oktoba 2013. Sherehe hizo
zilihudhuriwa na Wakazi mbalimbali wa Jimbo la Ohio na Majimbo mengine ya Jirani kama
Alabama. Mgeni rasmi katika Sherehe hizo alikuwa Mwenyekiti wa Chadema
Washinton DC, Ndugu Kalley Pandukizi aliyeambatana
na Katibu wa Chadema Washington DC Liberatus
Mwang’ombe na Viongozi wengine wa Chadema DMV. Tukio hilo la ufunguzi
lilianza kwa Mwenyekiti wa Chadema wa Ohio Ndugu Salva Muhaya kuongea historia fupi ya Kuanzishwa kwa Tawi hilo.
Baadaye lilifuata tukio la kukata utepe kama ishara ya kufungua tawi hilo
rasmi, lililofuatiwa na tukio la kukata keki kama ishara ya kuanza sherehe za
Ufunguzi rasmi. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na mmoja wa Wanachama Wakongwe
kabisa wa Chadema Mzee Gervas Kavishe
aliyejiunga Rasmi Chadema kama mwanachama tangu mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi
ulipoanza. Akizungumza katika Sherehe hizo Mgeni rasmi Ndugu Kalley Pandukizi
aliwasisitiza Watanzania wanaoishi Diaspora kujiunga na Chadema ili kuleta
Ukombozi kwa Mtanzania aliyekatishwa tamaa na hali mbaya ya Maisha. Naye Katibu
wa Tawi la Chadema Washington DC, Ndugu Liberatus Mwang’ombe aliwasisitiza
Watanzania wanaoishi Diaspora Kujua umuhimu wa kutoa Michango yao ya Hali na
Mali katika Harakati hizi za Kulikomboa Taifa, Kwani wanaoathirika na hali
mbaya ya Maisha ni Ndugu zetu hivyo lazima tuguswe na hilo na tutafute namna ya
kuwasaidia kwa kila hali.
Katibu wa Chadema Washington DC Ndugu Liberatus Mwang'ombe akihutubia siku ya ufunguzi wa Tawi la CHADEMA Ohio, Marekani.
Mwenyekiti wa Chadema Ohio, Salva Muhaya akitoa Historia fupi ya Ufunguzi wa Tawi la CHADEMA Ohio, Marekani, Kushoto ni Katibu wa Baraza la Wanawake DMV Ndugu Baybe Mgaza na Kulia ni Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Ndugu kalley Pandukizi.
Mgeni rasmi ndugu Kalley Pandukizi akitoa hotuba fupi kwenye ufunguzi wa Tawi la CHADEMA Ohio.
Mgeni Rasmi Ndugu Kalley Pandukizi akikata utepe kama ishara ya Ufunguzi rasmi wa Tawi la CHADEMA Ohio, Marekani. Kutoka kulia ni Katibu wa CHADEMA Ohio Ndugu Hellen Ongara, katibu wa wanawake CHADEMA DMV, Baybe Mgaza. Kutoka kushoto ni Katibu wa Chadema DMV Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti wa CHADEMA Ohio ndugu Salva Muhaya.
Mgeni rasmi akikata keki kama ishara ya kufungua sherehe rasmi ya Ufunguzi wa Tawi la CHADEMA Ohio, Marekani.
Mwanachama mkereketwa wa CCM Benjamini Mwaipaja alikuwa ni mmoja ya watu mbalimbali waliohudhuria sherehe za Ufunguzi wa Tawi la CHADEMA Ohio, Marekani.
Pichani Kutoka kulia ni Mwanachama mpya wa CHADEMA DMV Asia Dachi, Katibu wa CHADEMA Ohio Ndugu Hellen Ongara, Mkereketwa wa CCM kutoka DMV Ndugu Benjamini Mwaipaja, Mweka Hazina Wa Chadema DMV Ndugu Ludigo Mhagama na Katibu wa Wanawake CHADEMA DMV Ndugu Baybe Mgaza
Viongozi wa Chadema Ohio na DMV wakiwa katika picha ya pamoja.
Pichani katikati ni Mmoja kati ya Wazee waanzilishi wa Chadema tangu mwaka 1992 Mzee Gervas Kavishe akiwa na Katibu wa Chadema DMV ndugu Liberatus Mwan'ombe aliyeshika Kadi za Uanachama za Mzee kavishe aliyekata tangu mwaka 1992 na ya mwaka 2005. Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema DMV, Ndugu Kalley Pandukizi.
Wadau Muhimu wa Chadema Ohio
Ukumbi Uliofanyika Sherehe za Ufunguzi wa Tawi la Chadema Ohio Ulivyosheheni wakazi mbalimbali wa Ohio waliohudhuria sherehe hizo.
Wadau wa Chadema Ohio wakijadili mambo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Chadema DMV ndugu Kalley Pandukizi akibadilishana mawazo na Viongozi wenzake.
Pichani kutoka kushoto ni Katibu mwenezi wa Chadema Ohio dada Mwenda, Katibu wa CHADEMA DMV Liberatus Mwang'ombe, Katibu wa Chadema Ohio Ndugu Hellen Ongara, Mwenyekiti wa Chadema Ohio Ndugu Salva Muhaya na Mwenyekiti wa CHADEMA DMV, Ndugu Kalley Pandukizi.
Viongozi wa CHADEMA Ohio na Viongozi wa CHADEMA DMV katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment