Friday, October 18, 2013

Diwani Chadema apiga marufuku tozo la Barua za Dhamana Mahakanani na Mikopo!

Na Bryceson Mathias, MJi Mdogo Madizini.
DIWANI wa Kata ya Mtibwa wilayani Mvomero, Luka Mwakambaya, amewajia juu watendaji wa Vitongoji na Vijiji na Kata hiyo, huku akipiga marufuku kuwatoza wananchi kati ya Sh. 5,000/- na 10,000/- ili wasainiwe barua za kuombea Dhamana ndugu zao mahakamani na Mikopo kwenye taasisi za kifedha.
Mwakambaya alisema atakula sahani moja na watendaji hao na ikiwezekana kuwapeleka mahakamani wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu kuwatendea hivyo wananchi walalahoi hakuna tofauti na unyang’anyi unaofanywa na maharamia wanaojipatia fedha kwa njia za Rushwa.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Madizini Mwakambaya alisema, Kama watendaji hawa wakiendewa na watu 100 wenye shida ya kusainiwa barua za dhamana ya ndugu zao mahakani na watu 50 wenye shida ya kusainiwa barua za Mikopo kwenye taasisi za fedha watapa kiasi gani? Wizi!
“Ingawa wananchi tunalalamika kuwa tuna majambazi, wala rushwa, wauzaji wa madawa ya kulevya na kuitaka serikali iwashughulikie, lakini wengine tunao miongoni mwetu kama watendaji wa Vitongoji, Vijiji na Kata wanatoa tozo kwa kusaini barua za Dhamana mahakamani na Mikopo kwenye taasisi za fedha”.
Aidha Diwani huyo alipiga marufuku tozo ya Ushuru wa Gulio katika Soko la Madizini inayotozwa na Serikali ya Kijiji, kwamba haistahili kufanya hivyo kwa sababu haijakidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kuwa na Miundo mbinu ya Vyoo, Maji taka na Dampo la takatakama zingine za kijamii.
Aling’aka akisema, kama Kanuni tu ya Ufugaji Ng’ome inasema huwezi kumkamua Ng’ome usiyemlisha na kumtunza, sasa inakuwaje viongozi wa Mji Mdogo Madizini wawakamue wananchi tozo za Ushuru Gulio ikiwa hawajatengenezewa Huduma za Kijamii ikiwemo Vyoo? Alishangiliwa na wananchi.
Aliwataka wanananchi wasikubali na wakatae kutoa Ushuru, na kusaini hati barua za kuwaombea ndugu zao Dhamana mahakamani na mtu atakayedaiwa amuarifu na yeye atashugulika naye kisheria na kudai hajaona kumbukumbu yoyote fedha hizo zinafanya kazi gani za maendeleo zaidi ya kuingia matumboni mwa watendaji hao.

No comments:

Post a Comment