Tuesday, October 8, 2013

Bbq funga mwaka iliyoandaliwa na chadema uk yafana.

YAVUNA WANACHAMA WAPYA NA MICHANGO MINGI
BBQ funga Mwaka iliyofanyika Reading siku ya Jumamosi tarehe 05/10/13 imeelezwa kuwa ni ya mafanikio makubwa. WaTanzania wenye mapenzi na nchi yao walijitokeza na kushiriki kwa pamoja bila kujali dini, itikadi za kisiasa, rangi wala kabila. Waliohudhuria wengi walieleza kufurahishwa sana kwa mpangilio mzima na kwa wakati mzuri walioupata kubadilishana mawazo na kutafakari mustakabali wa nchi kwa pamoja kama waTanzania.
Aliyekuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo, Mr Amani Golugwa alitia chumvi na chachu kubwa kwa waTanzania kwa hotuba yake iliyokuwa na weledi wa hali ya juu. Aliwaeleza waTanzania kujihusisha kwa karibu na kushirikiana na wenzao walioko Tanzania katika kutatua changamoto zinazoikabili nchi yetu. Aliwataka waTanzania hasa vijana kujihusisha kwa namna moja au nyingine katika kuleta mabadiliko bila kujali chama wanachokiunga mkono. Hata hivyo aliwashauri vijana kwamba kama wanaamini katika mabadiliko, itakuwa ni vigumu kuyapata kwa kupitia chama tawala (ccm). Sababu kubwa ni kutokana na kwamba ccm ni chama ambacho kimejisahau na kukua kupita kiasi (too big to change). Kuleta mabadiliko (radical changes) ndani ya ccm ni vigumu sana kama siyo kutokuwezekana.
Katika siku hiyo CHADEMA imefanikiwa kupata ahadi za mchango wa pikipiki 10 zitakazoelekeza nguvu kwenye kukijenga chama kwenye ngazi za chini (mashina). Pamoja na pikipiki waTanzania wengine waliojitokeza waliahidi kuchangia gharama za ofisi na pango kwenye baadhi ya mashina ya CHADEMA vijijini na mijini pia. Ili kuimarisha na kuiweka CHADEMA tayari kwa ajili ya karne ya 21, baadhi ya waTanzania waliahidi kuitengenezea CHADEMA website ya kisasa kabisa.

Katika kuwavutia waTanzania wasomi na wajuzi ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara, mkutano huo ulidhamiria kuunda chombo cha kisasa kitakachowawezesha waTanzania kuchangia maendeleo ya nchi yetu. Chombo hicho kitakachojulikana kama Center for Leadership and Development (CELEDE), kitawakutanisha waTanzania wote kulingana na fani zao mbali mbali. Taarifa kamili kuhusu hili itatolewa hapo baadaye.
Haya ni baadhi tu ya mambo machache ambayo yanategemewa kufanyiwa kazi siku kadhaa zijazo. Hata hivyo ilikuwa siku nzuri pia kuwakaribisha wanachama wapya (wanawake kwa waume) walioamua kujiunga na chama siku hiyo. CHADEMA ni chama kinachopigania haki ya mTanzania wa kawaida. Namba kubwa ya waTanzania wameshalielewa hilo. Hata hivyo kwa wale ambao bado wanaendelea kudanganyika na hila za viongozi walioko madarakani kwa faida yao wenyewe huku wengi wakiishi maisha duni usiku na mchana, kinachohitajika ni kuwaelimisha. Mwisho wataelewa. CHADEMA kimejitolea na kina nia ya kuendelea kuifanya kazi hii bila kuchoka.
Aidha CHADEMA UK, wandaaji wa shughuli hiyo wanapenda kuwashukuru sana waTanzania wote kwa kujitokeza kwa wingi kukamilisha shughuli hiyo. Kwa wale ambao wameomba tuandae nyingine kabla ya mwisho wa Mwaka huu, tunawaahidi kwamba mtapata taarifa siku siyo nyingi sana. Itakayofuata itakuwa ni moto zaidi ya hii.
Ilikuwa pia ni furaha ni furaha kuwaandaa BAWACHA na BAVICHA ya kesho.









No comments:

Post a Comment