Saturday, September 7, 2013

Ndugai atakuwa wa kwanza kuhatarisha Amani ya Nchi.

Na Bryceson Mathias
 
KWA muda mrefu nimekuwa simuelewi, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kama yale anayoyafanya akiwa kwenye kiti cha Spika huwa anayafanya kwa maslahi ya Nani! Maana kama ni kwa ajili ya wananchi! Hawatendei haki.
 
KAMA Mwananchi wa nchi hii ninayelipa Kodi kuliwezesha Bunge lijadili na kupeleka Kero na Mawazo yetu Serikalini, nimekerwa na na tabia ya Ndugai, inayoisababisha kila mara anapokuwa kwenye Kiti cha Maaamuzi ya Bunge, na atakuwa wa kwanza kuhatarisha Amani ya Nchi.
 
Kwa nini nakerwa ni kutokana na kwamba, vitendo na maamuzi anayofanya Ndugai akiwa kwenye Kiti hicho kila siku, yana kila dalili za wazi za kuhatarisha Amani ya Nchi yetu, ambayo sidhani kama yeye binafsi ana chembe hata ya Haradali ya kuitafuta.
 
Namtaka Ndugai afike mahali abaini makosa yake ya kutaka kutusababishia Maafa, Vifo na Umwagaji wa Damu, ambao watanzania si Jadi yetu Kuutaka, Kuutaja na hata Kuuona labda tutauona kama tutafikishwe hapo na watu kama Ndugai, jambo ambalo tutalipinga kwa nguvu zetu zote hadi tone la Mwisho.
 
Kama Ndugai ni Mkristo liko andiko katika Biblia Mathayo 15:4 linasema, “Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe”. Hilo ni andiko linalotulazmisha na kutuogofya iwapo tutakiuka kuwashemu waliotutangulia.
 
Tukio la kupigana bungeni lililotokea hivi karibuni, si la kawaida, Naibu Spika ni kiongozi wa Bunge lakini wapo watu wakubwa ambao anapaswa kuwaheshimu au kuheshimika  nay eye anakuwa kwenye kiti chake.
 
Kambi ya Upinzani ina kiongozi wake ambaye ni, Freeman Mbowe, mwenye nafasi kubwa kama aliyonayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni. Tofauti ya Pinda na Mbowe ipo nje ya Bunge lakini wakiwa ndani ya Bunge wote wana heshima ya kufanana.

Sijui Jeuri ya Ndugai imetoka wapi hivi Pinda angekuwa amesimama bungeni kuomba Mwongozo, Naibu Spika angewaamuru askari wa Bunge wamtoe? Ndugai anapaswa kutuomba radhi watanzania maana amepoteza Kodi Yetu na Muda kuwalipa wabunge bila kufanya kazi.
 
Ukichunguza kinachobishaniwa katika Muswada huo kuwa haukuwa na ushirikishwaji, Kauli zinaweka wazi yuko mtu anasema Uongo na mwingine anasema ukweli. Ukweli huu sasa tunatamani sana Wahariri na Waandishi wao watuusaidie kama Mhimili wa ukweli uliojificha.
 
Waandishi wakitusaidie hilo, ni wazi tutabaini Ndugai alitumika Vibaya na Chama chake Tawala, alikiuka kanuni kwa maslahi ya CCM, na pia tutabaini Mkweli ni Wapinzani au Serikali kwa sababu, ukweli wa kwanza ni  Wabunge wa CUF, wanadai hawakuhusishwa!
 
Ieleweke, Barua ya Makamu wa Rais wa Pili Z’bar si Wanzanzibar wote, Mawazo ya Chama cha Siasa cha JAHAZI si Wazanzibar wote, ADC si Wazanzibar wote, kama ilivyo Tanzania bara kwa CCM, Chadema, CUF, NCCR na Kura za Wabunge 150 si za Watanzania wote.
 
Tunatakiwa kujiuliza na kuwaomba wenzetu wa Mhimili wa Nne (Wanahabri) ni kutupattia ufafanuzi chokonozi, kujua kwa nini CUF ambao wana Serikali ya Umoja wa Kitaifa na CCM Wabunge wake wakate kuwa hawakushikishwa? Kwa tamko la Serikali ya Z’bar lisiwe la Pamoja ila liwe la Makamu wa Pili wa Rais, Makamu wa kwanza liko wapi?
 
Vyombo vya Habari ndiyo Msema kweli wetu Mkuu wananchi, anatakayetupatia kilichojificha nyuma ya Pazia na kutuelekeza yupi Muongo, Serikali au Wapinzani? Lakinni isitoshe bado tunayo maswali mengi kwa Ndugai, wanandishi pia watuhabarishe Naibu Spika amekiuka Kanuni za Bunge?
 
Kuendesha Kikao cha Wabunge wachache wakati Waziri Mkuu Kiongozi wa Serikali hayupo kwenye Kiti chake kutokana na kuondoka kwenye Kikao hicho? Je Askari au Mtu yeyote anaweza kuingia bungeni bila kutenguliwa sheria za kuwaruhusu kufanya hivyo?
 
Wawahili wanasema Wingi wa Kamasi si Ukubwa wa Pua. Huwezi kuamua kumpiga Risasi Nyani anayetorosha Mtoto wako akiwa amembeba, kwa madai utamulenga Nyani, unaweza kumkosa na ukamuua Mwanao.
 
Ni rai yetu sasa kwa Waandishi, waende mbali kwa Kuhoji Vyombo husika na ushirikishwaji huo kama vihisishwa, Wananchi, Wasemaji wakuu, CUF Z’bar, Taasisi, Asasi na makundi Maalum yaliyokusudiwa, Vyama vya Upinzani na Viongozi wa Dini ili tubaini nani Muongo!
 
Aidha Waswahili wanasema Mtu Mzima hawezi kusema Uongo mara mbili, lakini nyakati hizi tunashuhudie hata watu wenye Malaka hawaoni aibu wala Soni kumwaga Uongo tena hadharani.
 
Ni Ombi letu kwa wanahabai kufanya hivyo wa sababu, Katiba si ya Viongozi wa CCM, CHADEMA< NCCR, CUF, ADC, JAHAZI na Vyama vyao, bali ni ya watanzania wote na vizazi vijavyo hivyo.
 
T unahitaji uchokonozi huo utusaidie wananchi kufanya maamuzi ya kujua Mbivu na Mbichi, Pumba na Mpunga katika kura ijayo ya Maoni, hasa kutokana na hofu ya kuwepo watu kama Ndugai wanaoweza kuhatarisha Amani yetu kwa uchochezi wa kuikana kweli.
 
Hali ya kukosa Hekima ya Kiti, ndiyo inayosababisha Vurugu, Fumo na ningependa wabunge wafikie kupiga kura za siri katika kutafuta au kutoa uamuzi kuepusha mizozo ya mara kwa mara inayozidi kujitokeza katika vikao vya bunge mjini Dodoma kiasi cha kupapaka uovu wa vurugu.

Ni vema Utaratibu wa Siyo na Ndiyo utumike wa kura ya siri ili kurudisha nidhamu iliyopotea kwa kipindi kirefu, hasa kwa kuwa mizozo hiyo inazidi kutoa sifa mbaya kwa wapiga kura na jamii kwa ujumla.
 
Kama ni Muungwana, Ndugai aiombe radhi Kambi ya Upinzani kwa kitendo cha kumtoa ndani ya Bunge kiongozi wa kambi hiyo bungeni (Mbowe). Maana kitendo hicho ni ukiukaji wa kanuni na sheria za Bunge, na kimeidhalilisha kambi hiyo.
 

No comments:

Post a Comment