Sunday, July 7, 2013

Polisi yazuia Mkutano wa Chadema Gairo.

JESHI la Polisi wilayani Gairo, limezuia Mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) uliokuwa ufanyike leo (jana) Jumamosi, July 06, 2013 katika viwanja vya shule ya Msingi Gairo.
Akizungumza na Katibu wa Chadema Gairo kwa simu, Dickson Lenjima, Kiongozi wa zamu wa Polisi Gairo ambaye alisema si Msemaji alidai, Kichwa cha Habari cha Maombi ya Chadema kimekosewa, badala ya kuomba kufanya mikutano, kisema taarifa ya kufanya mikutano.
Zuio hilo lililolalamikiwa na Chadema, limekuja siku chache baada ya kuwepo Kikao cha Mkuu wa Polisi Mkoa (RPC), Faustini Shilogile, Mkuu wa Wilaya, Hanipha Karamagi, Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa, kulilalamikia Jeshi hilo kuzuia Mikutano, na RPC kusema ruksa!
Mkutano huo umezuiwa kukiwa na sintofahamu ya malalamiko ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Omari Awadhi, wilayani humo, kwamba alikuwa amemwagiwa Tindikali usoni na wapinzani wake hivi karibuni na watu waiojulikana waliomtaka ajiuzulu nafasi yake.
Wananchi waliokusanyika kuskiliza Mkutano huo wamelaani kitendo cha Polisi kuzuia Mkutano huo wakidai, kama RPC Shilogile alisema katika kikao cha maridhiano ruksa! Zuio hilo linatoka wapi? Mmoja wa Viongozi wa CCM aliyeomba asitajwe alisema, CCM walihofu suala Tindikali kusemewa na Chadema mkutanoni.
Aidha Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Chadema Morogoro Suzan Kiwanga, Salum Mpanda, ambaye alikuwa mmojawapo wa Wahutubiaji wa Mkutano huo alikiri kuzuiwa kwa Mkutano wao na kudai, "Mtu Muongo mpe Kamba ndefu, asisieme hakujinyonga kwa ufupi wa Kamba".

Na Bryceson Mathiasm Morogoro.

No comments:

Post a Comment