Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, ambaye amelazwa kwenye Taasisi ya Magonjwa ya Mifupa (MOI), akisumbuliwa na maumivu ya shingo pamoja na mkono anaendelea vizuri.Ofisa Habari wa Taasisi hiyo, Patrick Mvungi, aliiambia NIPASHE jana kuwa Lwakatare ambaye alifikishwa Hostitalini hapo Jumanne ya wiki hii, anaendelea na matibabu huku akiwa chini ya jopo la Madaktari ambao walimfanyia vipimo alipofikishwa hospitalini hapo.
Mvungi aliongeza kuwa Lwakatare alikuwa analalamikia maumivu ya shingo pamoja na mkono, na jopo hilo la madaktari wanaangalia ni jinsi gani wataweza kulishugulikia tatizo hilo ambalo anasema limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu kidogo.
No comments:
Post a Comment