MKUU WA MKOA, POLISI WAPIGWA ‘STOP’
UCHAGUZI mdogo wa madiwani katika kata nne za Halmashauri ya Jiji la Arusha unafanyika leo huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikiwapiga marufuku Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo na Kamanda wa Polisi wa mkoa na Jeshi la Polisi kutojihusisha na usimamizi wa uchaguzi huo.
Ujumbe mzito wa watendaji wakuu na maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Damian Lubuva ‘wamehamia’ jijini hapa kwa ajili ya kuratibu mwenendo mzima wa uchaguzi huo uliotawaliwa na hofu ya kutokea tena vurugu.
Msafara wa viongozi hao wa tume kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam umezua sintofahamu miongoni mwa wananchi wakiwamo waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa maandalizi ya uchaguzi huo.
Akizungumzia hatua hiyo na msimamo wa tume yake, Jaji Lubuva alisema watendaji hao wa serikali hawana mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo isipokuwa tume yenyewe.
Amedai kuwa wameamua kuweka ‘kambi’ ya muda katika uchaguzi huo kwa kuwa Mkoa wa Arusha umekuwa na historia, hasa kufuatia tukio la mlipuko wa bomu uliotokea wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa CHADEMA eneo la Soweto, ambapo watu wanne walifariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
“Tumekuja hapa kwani tukio hilo limeacha historia, kwani halijawahi kutokea hapa nchini, hivyo tupo kufuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa uchaguzi… na zaidi tutatoa ushauri utakapohitajika,” alisema.
Mbali na Jaji Lubuva, wengine waliowasili jijini hapa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti, Hamid Mohamed Hamid, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba na maofisa wengine wapatao kumi.
Jaji Lubuva akizungumzia maandalizi ya uchaguzi, alisema yamekamilika na kuwaomba wananchi kushiriki uchaguzi huo bila hofu, kwani usalama umeimarishwa na kutoa onyo kwa baadhi ya watu kutowazuia wanaokwenda kutumia haki yao ya kikatiba.
Alisema vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni na kuongeza kwamba idadi ya wapiga kura ni 60,123 katika kata zote utakapofanyika uchaguzi huo; za Kaloleni, Themi, Elerai na Kimandolu.
Vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kupiga kura ni 136, ambapo Kaloleni ina vituo 27, Elerai 56, Kimandolu 39 na Themi ina vituo 15, katika uchaguzi huo unaosubiriwa kwa hamu.
Alisisitiza kuwa watakaoruhusiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura ni wasimamizi wa uchaguzi, makarani, wapiga kura, mjumbe wa tume kwa kibali maalumu, askari polisi na wakala wa chama.
Alisema kuwa karatasi za kupigia kura zimebadilishwa rangi kutoka zile zilizoandaliwa awali katika uchaguzi ulioahirishwa kutokana na hofu ya udanganyifu katika kura.
Wagombea udiwani katika Kata ya Kaloleni waliopitishwa na vyama vyao kwenye mabano ni pamoja na Emmanuel Milliani (CCM), Kessy Lewi (CHADEMA), Ngilisho Paulo (Demokrasia Makini) na Darwesh Mkindi (CUF).
Katika Kata ya Kimandolu ina wagombea wawili tu ambao ni Edna Saul (CCM) na Rayson Ngowi (CHADEMA), ambapo katika Kata ya Themi wagombea ni Malance Kinabo (CHADEMA), Victor Mkolwe (CCM) na Lebora Ndarvoi (CUF).
Uchaguzi katika Kata ya Elerai unawajumuisha wagombea ambao ni pamoja na John Bayo (CUF), Injinia Jeremia Mpinga (CHADEMA), Emmanuel Laizer (CCM) na Boidefi Shirima (TLP).
CHADEMA yaonya
Wakati huohuo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini kimewataka viongozi wa kimila wa kabila la Wamasai (Laigwanan) kutokubali kutumiwa na wanasiasa kuvuruga nchi.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Israel Natse, alisema viongozi hao wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwa malengo ya kisiasa na kuharibu heshima yao katika jamii
ambayo ni kubwa.
“Sisi kama CHADEMA hatuna ugomvi na viongozi hao wa kimila, bali tuna ugomvi na viongozi wa chama tawala,” alisema.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, aliwataka wakazi wa Arusha kujitokeza kupiga kura na wao kama chama wamejipanga vema kulinda kura zao.
“Tumejipanga vema kulinda kura zetu na nawaomba Wana CHADEMA wawe watulivu kesho (leo) hata kama watapata msukosuko wawe wavumilivu, lakini ikifikia hatua ya manyanyaso kupindukia wamuombe Mungu awaongoze katika maamuzi,’’ alisema Lema.

No comments:
Post a Comment