Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ametahadharisha kuwa kung'ang'ania kuendesha nchi kwa kufuata mfumo wa sasa wa utawala wa Serikali mbili ili kuepuka gharama za uendeshaji wa serikali tatu kunaweza kusababisha kuvunjika kwa Muungano siku za usoni.
Alisema Watanzania wanapaswa kuamua kujitoa kwa gharama ndogo kwa ajili ya serikali tatu kwa kukubalia mapendekezo ya rasimu ya Katiba mpya vinginevyo wataukosa kabisa Muungano wenyewe ambao umedumu kwa takribani miaka 49 sasa.
Jaji Warioba aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni ya ITV wakati wa mahojiano na kutoa mambo muhimu juu ya rasimu ya katiba iliyozinduliwa Juni 3, mwaka huu.
"Wenzetu wa Zanzibar walikuwa na mambo mengi ya kutoridhishwa juu ya Muungano kuliko Tanzania Bara. Ni vema tukatafuta njia ya kupunguza gharama badala ya kuiepuka kama tunataka kuuokoa Muungano. Maamuzi haya tumeyatoa baada ya kutafakari maoni ya waliowengi na siyo hivi hivi tu. Tumezingatia mapendekezo ya Watanzania wengi,” alionya Jaji Warioba.
Jaji Warioba pia alijibua changamoto zinazotolewa na watu juu ya dira ya taifa, alisema Tume imeweka wazi katika utangulizi wa rasimu yake kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongozwa kwa misingi ya demokrasia na utawala bora na kusisitiza juu msingi ya kujitegemea.
"Serikali inatakiwa kutoa taarifa zake kila mwaka kwa wananchi katika Bunge la Agosti ni jinsi gani imefanya kazi bila kujali itikadi za kisiasa," alisema.
Jaji Warioba alizitaja maeneo ambayo yalijadiliwa zaidi katika ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya kuwa ni ardhi, elimu na afya.
“Kwenye ardhi kulikuwa na matatizo mengi hasa juu ya umiliki wake na matumizi yake kuna ubishani mwingi juu nani mwenye haki ya milki ya ardhi. Pia kuna suala matumizi ya ardhi kati wawekezaji na wananchi, Hata hivyo, ardhi siyo suala la Muungano,” alisema Jaji Warioba.
Kauli ya Jaji Warioba inatolewa siku chache tu baada wanataaluma na wansisiasa kuelezea wasiwasi wao juu ya mfumo wa serikali tatu wakisema utakuwa wa gharama kubwa na ni kuzidi kuwabebesha mzigo walipa kodi.
Wakati huo huo; Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimeyataka mabaraza ya katiba kupambana kwa ajili ya kuondoa mapungufu juu ya haki za wanawake na watoto ili kuleta haki, usawa na maendeleo ya nchi.
“Tamwa inaamini katika kuleta mabadiliko ambayo ushawishi wa maendeleo katika Tanzania ni muda muafaka kwa mabaraza kuangalia rasimu na kuhakikisha mapungufu yanatolewa kabisa kuwapo kwa usawa kwa wanawake na wanaume Tanzania,” alisema Mwenyekiti wa Tamwa Valerie Msoka.
Msoka alisema kunahitajika nguvu za wanaume na wanawake katika kukabiliana na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia na sheria kandamizi kwa wanawake na watoto wa kike.
Aliipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kutoa rasimu hiyo kwani itakuwa ni fursa kwa wananchi, wanawake na wanaume kushiriki katika demokrasia ya nchi yao, hasa kwa kulinda mwanamke na mtoto wa kike dhidi ya vita ubakaji, ndoa za mapema na ukeketaji.
Juni 3, mwaka Tume hiyo ilizindua rasimu ya kwanza ya katiba ambapo miongoni mwa masuala ambayo ilikuwa ni pamoja na kuundwa kwa serikali tatu idadi ya mambo ya Muungano kuwa saba kutoka 22; nafasi ya Spika wa Bunge na Naibu wake kutotokana na chama chochote cha siasa.
Mengine ni mawaziri kutokuwa wabunge; nafasi za uteuzi wa Rais kuidhinishwa na Bunge; kuongeza umri wa kuwa mbunge kutoka miaka 21 hadi 25; kuingizwa kwa ibara za haki ya kupata habari katika katiba.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi hasa Zanzibar wameeleza kutokufurahishwa na mapendekeo hayo wakitaka mamlaka kamili ya Zanzibar.
CCM wametandikwa mwiba wa makalioni.
ReplyDeleteMuungano wa serikali mbili anayeuweza ni shEtani tu. Hili suala la gharama ni suala la uongo.
CCM ni chama kisichojali gharama katika kuendesha serikali yake. Ona misafara ya Rais wa nchi , Ona jinsi misafara ya chama ya kipuuzi inavyotumia fedha za walipa kodi?
Wizi mkubwa wa aina ile ya EPA unafanyika kila mwaka.
Suala la umeme wa Mgao ni mzigo mkubwa ambao CCM wamekuwa wakihakikisha unaendelea kubebwa na wananchi kwa nguvu zote. Zigo la Tanesco ni Ulaji wa moja kwa moja wa CCM.
CCM has to come clean on this.
Hivi ni gharama za kundesha serikali Tatu ndizo zinawafanya wajae pumzi na kuugua presha???? Au ni ukweli kwamba wanajua mwisho wao wa kutawala kwa HILA za Kishetani umeshajitimiliza????
Masikini WAO M, WAO M, WAO M, WAO M, WAO M!!!!!!!! !!!!!!!!!!!!!
M wa M
CCM wanaogopa Kivuli chao wenyewe! Wananchi wengi tunataka Serikali Tatu. Hizo Mbili zimefikia kileleni,haziwezi kwenda mbele tena miaka 5 au 25 ijayo. Tumeschoshwa na UNDUMILAKUWILI wa CCM, Hizo gharama wanazotuogopesha nazo hazipo,na kama vipi watafute njia mbadala ya kupata mapato,ikiwemo kuondoa kabisa misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa.
ReplyDelete