Mbunge wa Kigoma Kaskazini(Chadema), Zitto Kabwe amealikwa kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen mwaka huu, linaliofanyika Marekani.
Tamasha hilo linawajumuisha pamoja watu mashuhuri katika nyanja mbalimbali duniani lengo likiwa ni kuwawezesha kubadilishana mawazo na uzoefu.
Kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Zitto amesema ushiriki wake katika tamasha hilo utamwezesha kukutana na kubadilishana mawazo na magwiji wa masuala mbalimbali duniani.
“Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu kwangu mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa masuala mbalimbali, pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa waalikwa wenzangu. Nina uhakika kuwa watu nitakaokutana na kubadilishana nao mawazo na uzoefu watasaidia kupanua uelewa wangu wa masuala kadhaa,” alisema Zitto.
Alisema tamasha hilo litaendeshwa litaanza Juni 26 mwaka huu, limegawanyika katika sehemu mbili.
Alisema ya kwanza itahusisha majadiliano ya pamoja, ya vikundi na ya mtu mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment