Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, imeshindwa kuwasilisha hotuba mbadala ya bajeti kama ilivyo kawaida, baada ya wabunge wote wa Chadema kutohudhuria.Wabunge hao walielezwa kuwa wapo mkoani Arusha kufuatilia mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita, eneo la Soweto na kuua watatu wawili na kujeruhi 70.Tukio hilo ambalo ni la kwanza kutokea, lilitokea baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge kuwasilisha taarifa yake kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2013 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2013/14 na tathmini ya utekelezaji Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13.Baada ya Chenge kumaliza uwasilishaji wake, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliita msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha (Zitto Kabwe), hata hivyo hakuwapo.“Baada ya Chenge kumaliza ilikuwa zamu ya upinzani kuwasilisha bajeti yao, lakini siwaoni na sina taarifa rasmi za kutokuwapo kwao leo wala sijapokea simu,” alisema Makinda alisema na kuongeza:“Sasa kwa kuwa hawapo nitawataja wabunge kadhaa kwa ajili ya kuchangia hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2013/14.”Hata hivyo, baadaye Kambi Rasmi ya Upinzani ilisambaza kwa waandishi wa habari hotuba yake mbadala ya bajeti iliyokuwa isomwe bungeni na Zitto, ambayo Msemaji wa Chadema, John Mnyika alithibitisha kuwa sahihi.Katika hotuba hiyo, Zitto licha ya mambo mengine, Serikali ya CCM imechukua na kuyafanyia kazi na kuleta matokeo mazuri.Alisema kwamba Kambi Rasmi ya Upinzani itaendelea kuionyesha njia Serikali na CCM kuhusu namna bora na rahisi ya kuondoa nchi katika giza la uchumi na lindi la umaskini. Zitto alisema deni la taifa limeendela kuwa changamoto kubwa kwa uchumi, hali inayosababisha bajeti ya Serikali kuendelea kuwa tegemezi, hivyo kushindwa kutatua kero za uchumi wa wananchi.
No comments:
Post a Comment