TAMKO RASMI CHADEMA UK
CHADEMA UK awali ya yote tunapenda kutoa pole kwa waTanzania na wapenzi wa
CHADEMA waliopatwa na kukutwa na janga la kurushwa kwa bomu kwenye mkutano wa
CHADEMA wa kuhitimisha shughuli za kampeni za uchaguzi wa madiwani huko Arusha.
Tunatuma salam zetu kuwafariji wale wote walioguswa kwa namna moja ama nyingine
katika jambo hili.
Kama waTanzania,
tunapinga vikali na kukemea kitendo hichi kwa nguvu zetu
zote. Mazingira na jinsi kitendo hichi kilivyotekelezwa tuna kila sababu ya
kuamini kwamba hili ni tendo la kigaidi. Na kwa sababu hiyo ni jukumu la
mamlaka (yaani serikali) na vyombo vyake vya dola kulinda na kuepusha matendo
ya kigaidi kama haya.
CHADEMA ni chama
kinachoongozwa na watu makini (effective and responsible leaders) wenye
kuheshimu mamlaka ya sheria za nchi. Wanachama wa CHADEMA wamekuwa watulivu
siku zote wakifuata na kuheshimu sheria kama chama kinavyowaelekeza. Hata
pamoja na kwamba yamekuwepo matendo mengi sana yanayoashiria kuukandamiza upinzani
(hasa CHADEMA) kwa uwazi kabisa, viongozi wamekuwa mstari wa mbele kuwatuliza
wananchi na kuwataka waendelee kuwa na imani na mamlaka. Hii ni dhahiri kwamba
imesaidia kuepusha vurugu kusambaa na kuiingiza nchi kwenye balaa la vita baina
yetu sisi wenyewe.
Japokuwa chama na hasa sisi wanaCHADEMA UK tutaendelea
kutafuta mbinu nyingine katika kupambana na uonevu huu kwa njia ya amani
(baadhi kama tulivyoanisha hapo chini), tunapenda pia kuitahadharisha mamlaka
kutokujisahau (against complacency) kwamba kama hatua za msingi hazitachukuliwa
uvumilivu wa waTanzania utafikia kikomo. Hili ni KARIPIO KALI kwa mamlaka zinazohusika na kwa
sababu hiyo tumechukua hatua zifuatazo:
1. Tumetuma barua ya
rasmi ya ushauri kwa kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano mh. J.M Kikwete. Pamoja
na mambo mengine tumetoa maoni yetu kama ifuatavyo:
Usalama wa taifa ufanyiwe marekebisho makubwa: Tanzania Intelligence Services (TIS) inahitaji kufanyiwa marekebisho na ikibidi ivunjwe na kuwe na vikosi vifuatavyo:
Usalama wa taifa ufanyiwe marekebisho makubwa: Tanzania Intelligence Services (TIS) inahitaji kufanyiwa marekebisho na ikibidi ivunjwe na kuwe na vikosi vifuatavyo:
o Tanzania Secret Intelligence
Services (TSIS): Hii iwe ni mamlaka ya kutafuata, kupata na kusimamia siri za
kimataifa ikiwa ni katika kulinda nchi na mipaka yake. Kwa kushirikiana na
vyombo mbali mbali TSIS itakuwa na jukumu la kupata siri za kijeshi, ugaidi wa
kimataifa, n.k.
o Tanzania Serious
Organised Crime Unit (TSOCU): Kitengo hiki kiwe na wajuzi wa maswala mbali
mbali ikiwahusisha Polisi maalumu, wataalamu wa computer na mawasiliano, na
wajuzi wenye uelewa wa kuchunguza matendo ya kijangili. Kazi kubwa ya kitengo hiki
iwe ni kuchunguza na kuwakamata wahalifu wote wanaofanya matendo ya kijangili
ikiwa ni pamoja na madawa ya kulevya; wizi ndani ya mashirika na taasisi za
serikali unaofanywa na kupangwa na wafanyakazi kwa kushirikiana na watu mbali
mbali; Mauaji; n.k. Hata hivyo kazi nyingine muhimu ya TSOCU iwe ni, kwa
kutumia njia za kisasa kabisa, kugundua mapema na kuzuia uhalifu kutokea. Kama
wakipatikana wana usalama wenye uwezo, kitengo hiki kitaepusha upotevu wa
maisha ya watu wasio na hatia kwa kiwango cha juu. Cha muhimu ni kuhakikisha
kitengo hiki kinapatiwa vifaa na mafunzo ya kisasa kabisa ili kufanya kazi zake
kwa ufanisi zaidi.
Kuna umuhimu mkubwa
sana wa kuvipa uhuru vyombo hivi vya usalama kutoka kwa wansiasa. Kwa mfano
ilivyo sasa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ndiyo wenyeviti wa kamati za
usalama za wilaya na mikoa. Hivi vyote ni vyeo (appointement) vya kisiasa. Kwa
hivyo kama CHADEMA hatuamini kabisa kwamba vyombo hivi vinaweza kusimamia
maswala ya kiusalama kwa haki bila upendeleo wa kisiasa.
Kazi za jeshi la
polisi ziwe za kufanya kazi karibu kabisa na wananchi katika kusimamia sheria,
kulinda wananchi na mali zao, kuzuia uhalifu, na kuwapunguzia wananchi hofu ya
kufanyiwa vitendo vya kihalifu ili kumfanya kila mwananchi ajisikie huru. Hii
itakuwa ni kuhakikisha jamii inaishi kwa kufuata sheria na taratibu
(maintaining public order), kupambana na wahalifu na kwa kushirikiana na vyombo
vingine vya usalama.
Hata hivyo jeshi hilo
linahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa. Dosari kubwa zinaonekana dhahiri
kuanzia kwenye ngazi za mkuu wa jeshi hilo nchini (IGP), kwenda chini kwenye
ngazi za wakuu wa polisi wa mikoa (RPCs), wakuu wa vitu (OCSs) na polisi wa
kawaida. Kwa mfano mauaji yanapotokea, hakuna uwajibikaji (accountability).
Kwa sababu hiyo kuna
umuhimu wa kuzipa nguvu kamati ya ulinzi na usalama ya bunge ili ziweze kuwaita
na kuwahoji wakuu wa usalama ili wajieleze mbele ya kamati pale inapohitajika.
2. Tumeandika barua
kwenda kwenye ofisi za haki za binadamu (International Human Rights Office) hapa
London. Nia na madhumuni ni kuwapa picha ya vitendo vya kinyama vinavyofanywa
na baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi.
3. Tumetuma barua kwenye
balozi zaidi ya nane za nchi mbali mbali tukiyaeleza na kuyaanisha matukio
yanayoendelea ndani ya nchi huku viongozi wetu wakikaa kimya.
4. Tumevitaarifu vyombo
mbali mbali vya habari kama vile BBC, RT Television na Aljazeer kuhusu hali na
mwelekeo wa kisiasa Tanzania ambao umeanza kuchukua sura mpya.
Kwa nguvu zote
tutaendelea kuueleza ulimwengu na kukaripia uhalifu huu tunaofanyiwa ndani ya
nchi. Ni muhimu kwa waTanzania kufahamu kwamba upinzani siyo dhambi . Upinzani
ni mawazo mbadala.
Kwa wana-CHADEMA wenzetu
Tanzania ni nchi yetu tunayoipenda na kuithamini. Tunaamini kabisa kwamba amani na utulivu ni vitu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Sote tunatamani kuwarithisha watoto wetu (next generation) nchi itakayowapa fursa ya kusonga mbele. Hata hivyo amani tunayoiongelea hapa si amani ambayo tumeaminishwa na serikali ya ccm kwa miaka mingi. Amani tunayoisema ni amani ya kweli, amani inayoheshimu utu, amani inayompa fursa kila mwananchi kufanya shuughuli zake bila kuogopa ili mradi anafuata sheria za nchi.
Tanzania ni nchi yetu tunayoipenda na kuithamini. Tunaamini kabisa kwamba amani na utulivu ni vitu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Sote tunatamani kuwarithisha watoto wetu (next generation) nchi itakayowapa fursa ya kusonga mbele. Hata hivyo amani tunayoiongelea hapa si amani ambayo tumeaminishwa na serikali ya ccm kwa miaka mingi. Amani tunayoisema ni amani ya kweli, amani inayoheshimu utu, amani inayompa fursa kila mwananchi kufanya shuughuli zake bila kuogopa ili mradi anafuata sheria za nchi.
Ni dhahiri kwamba
wengi tumechoshwa na uongozi mbovu ambao tumeifikisha nchi hii hapa tulipo leo.
Wengine hata tunashangaa kwamba hawa hawa ambao wamekuwa madarakani kwa miaka
zaidi ya 50 bila kuleta maendeleo yeyote, leo hii wanaonekana kutaka
kung’ang’ania madaraka kwa gharama zozote zile hata kwa kumwaga damu. Watu hawa
wanaonesha uchu na jazba ya hali ya juu lakini wakiambiwa wajieleze ni nini
wamekifanya kwa miaka 50 hawana jibu. Ikiwa kama haitoshi, wengi tunaona kwamba
sasa imetosha, tumeshavumilia vya kutosha (enough is enough).
Pamoja na hayo
tunawaomba tuendelee kutetea bila kuchoka juhudi za kulikomboa taifa letu.
Endeleeni kuwaelimisha na wengine ambao bado wanahitaji kufumbuka macho. Ukiona
hali inafikia hapa ilikofikia, kwa wale wanaojua kusoma nyakati, watajua kwamba
ushindi umekaribia.
Chanzo Vijimambo Blog
Mungu awabariki.
ReplyDeleteyou will never walk alone viva M4C
ReplyDeleteMmefanya vema watu wa UK. Ila itakuwa vema zaidi kama mtaweza kuandaa maandamano ya amani kueleza ulimwengu juu ya yanayoendelea Tz. Naamini huko UK hamtapigwa mabomu mkiandamana.
ReplyDeleteHongereni sana watu wa UK mmefanya vema. Ila itapendeza sana kama mtaweza kuji organize na watu wa US mkafanya maanadamano ya amani kulaani vitendo viovu vinavyoendelea Tz. I hope huko mliko hamtapigwa mabomu!
ReplyDelete