Tuesday, June 4, 2013

Tundu Lissu awa ndio nguzo kubwa ya katiba mpya bora- CCM wamuundia mizengwe asiijadili

Kamanda hodari, msomi mzalendo mwana wa Tanzania Antipasi Tundu Lissu amejikuta akiundiwa zengwe la kutolewa bungeni ili tu asishiriki kwenye mchakato wa katiba.Maongezi ya muda mrefu kati ya makada na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) yamekuwa jinsi ya kumfungulia kesi ya kupinga ubunge wake, kumuandaa jaji wa kutengua matokea ili hata rufaa ikikatwa na kushinda awe tayari amekosa kipindi cha kujadili rasimu hii ya katiba.
Kwanini wanafanya hivyo. CCM hawana msomi mwenye weledi wa Tundu Lissu , mwenye uwezo wa kujenga hoja, kutetea ukweli na kuweka masilahi ya Taifa mbele badala ya kwake. Mwenye kujua na kuona mbali hasa mahitaji ya kisheria na kikatiba ya nchi yetu.
Ndani ya bunge wako wanaCCM wengi wanasheria tena wazuri waliobobea wenye ujuzi na mihela mingi ya kazi yao. Ila wote ndani ya CCM wamefunikwa na kikombe cha ufisadi na kushindwa kutetea kweli. Wapo akina mkono, Mwakyembe, Chenge, nk nk ila huwezi hata siku moja ukiwasikia wakiongelea mambo muhimu kwa mustakabali wa nchi. 
Taifa likatae mahakama kufanywa misukule na majaji wa kununuliwa waonekane ni adui namba moja wa taaluma ya sheria na ustawi wa nchi huru na ya haki.

Fuefue

1 comment:

  1. Tunakiomba Chama kuungana pamoja kwa ujumla wake kuondokana na udhalimu huu unaoendeshwa na CCM kwa maslahi ya wachache badala ya watanzania.
    Kamwe msife moyo viongozi wetu na tambueni wananchi tuko nyuma yenu kuhakikisha tunalikomboa taifa.
    Sote tuseme Hapana Hapana Hapana kwa Lissu kuvuliwa ubunge kupitia mahakama ambazo zinashinikizwa na CCM kama tulivyoona Huko Igunga.

    ReplyDelete