SERIKALI imekiri kuwapo kwa msongamano wa wafungwa katika magereza yote nchini likiwamo Gereza la Ngudu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, alisema jana bungeni kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo Jeshi la Magereza kupitia bajeti linayopewa na serikali limekuwa likiyatatua kwa awamu, kwa kuyafanyia ukarabati magereza yaliyopo, kukamilisha na kujenga magereza mapya katika wilaya ambazo hazima magereza.
Alisema lengo ni kuongeza nafasi za kuhifadhi wafungwa magerezani.
Naibu waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere (CHADEMA), ambaye alitaka kujua serikali itarekebisha lini jambo hilo na msongamano katika magereza hasa Gereza la Ngudu ili kuepuka ukiukwaji wa haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment