Saturday, June 22, 2013

Maoni ya Prof Shivji Kuhusu Rasimu ya Katiba

UTATANISHI NA UKIMYA KATIKARASIMU YA KATIBA MPYA
Issa Shivji
MHADHARA WA KUAGA KIGODA CHA MWALIMU
KIGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERKE
Copyright © Issa Shivji, 2013

Kwa dhati kabisa ningependa kuwashukuru wanakigoda wenzangu, Ng’wanza Kamata, Saida-Yahya-Othman naBashiru Ally, kwa mazungumzo marefu na mabishano makali ambayo yamenisaidia kunoa hoja zangu na kuwazayasiyowazika. Shukrani zangu kwa Walter Rodney Luanda na Bashiru Ally, waliosimamia uchapishaji wa Mhadhara katika muda mfupi wa siku mbili. Walter amekuwa bega kwa bega nami kwa miaka mitano yote ya uNyagoda wangu. Amefanyakazi za Kigoda kutokana na imani na msimamo wake na siokiajira tu. Mwishowe, namshukuru sana, kwa moyo mkunjufu, SaidaYahya-Othman ambaye amehariri Mhadhara kwa ustadi wamtaalam wa lugha katika masaa ishirini na nne, tena katikasiku yake ya mapumziko maalum.
Shukrani


1.Naialika kaumu, tutafakari pamoja, Kuhusu Tunu muhimu, Rasimu ilizotaja, Kati ya Tunu adhimu, mojawapo ni umoja, Kabla ya Ukombozi, Umoja hauwi Tunu
2.Umoja hauwi Tunu, Kwa taifa tegemezi, Bali umoja ni Tunu, baada ya ukombozi,
Umoja hasa ni mbinu, ya kuunda mapinduzi, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
3.Uchumi wa nchi yetu, ni uchumi tegemezi, Na hasa kilimo chetu, siyo cha kimapinduzi, Na pia elimu yetu, ni chombo cha ubaguzi, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
4.Tanzania nchi yetu, sasa haina amani, Uhuru na utu wetu, kwa sasa viko rehani, Fikra na mila zetu, havina tena thamani, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu,
5.Tutafakari maoni, ya waliotangulia,
Ya Mkwawa na Fanoni, na ya Bibi Titi pia, Umoja walithamini, hoja waliujengea, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
6.Umoja imara hasa, siyo uliopo sasa, Huu umoja wa sasa, ni umoja wa mikasa
Mikasa ya kisiasa, na hila za wenye pesa, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
7.Umoja si mapatano, baina ya wala tonge, Umoja si mikutano, ya Jangwani na Kisonge, Umoja ni muungano, wa tabaka la wanyonge, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu,
8.Umoja sio ubia, wa mitaji ya ‘mabwana’, Umoja ni ujamaa, wa watu wasonyonyana,
Umoja kwa wenye njaa, ni nyenzo muhimu sana, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
9.Mhimili wa umoja, ni dira ya ukombozi, Na adui wa umoja, ni mifumo kandamizi, Na kitanzi cha umoja, ni sera za kibaguzi, Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.
10.Tunataka ukombozi, wa fikra za wanyonge, Tunataka mapinduzi, ya uchumi wa wanyonge, Tunataka mageuzi, ya Umoja wa wanyonge Kabla ya Ukombozi, Umoja hauwi Tunu
1.
UMOJAHAUWI TUNU,KABLA YAUKOMBOZI
– Na Mwalimu Bashiru Ally


UTANGULIZI
Niliposimikwa mnamo tarehe 18 Aprili 2008 kuwa Profesa wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika Umajumui wa Afrika, nilitoa mhadhara wa uzinduzi juu ya ‘Umajumui wa Afrika katika Fikra za Mwalimu’. Sasa ninakaribia kumaliza muda wangu hapo tarehe 31 Agosti 2013, nimeona si vema nikiondoka bila kutoa mhadhara wa kuaga Kigoda, wanakigoda na wanachuo wenzangu, na wale wote waliokuwa pamoja nasi katika shughuli na mijadala yetu.
Tumepanga mhadhara huu mapema kidogo kwa sababu mbili. Moja, wanafunzi, vijana wa Kigoda, wanaondoka leo kwenda kwenye likizo yao. Ya nini kutoa mhadhara wakati wenyewe hawapo? Pili, mapema mwezi ujao, pamoja na wasomi wenzangu wawili, tumejipangia kwenda nje ya nchi kufanya utafiti wa kuandika wasifu (biography) wa Mwalimu. Kwa hivyo, tukaona tarehe ya leo ni mwafaka.
Nimegawa mhadhara huu katika sehemu kuu nne. Hoja yangu ambayo itaeleza udhani (hypothesis) wangu ulioniongoza kuchambua Rasimu ni sehemu ya kwanza. Sehemu ya pili itazumgumzia dhana ya ‘ukuu wa katiba’ ya shirikisho, yaani

Kwa kirefu kidogo, ‘moyo’ wasuprasimu,emacy ofyaanithemuundofederal constitutionna taasisi za muungano, nitazichambua katika sehemu ya tatu. Sehemu ya mwisho, ambayo ni ya nne, kabla sijahitimisha mhadhara wangu, itakuwa juu ya matumaini ya wananchi ya Tanzania Mpya.

Bonyeza Read More Kuendelea


HOJA
Awali ya yote ningependa kuweka wazi, mosi, mtazamo wanguutakaoniongoza katika kuchambua Rasimu ya Katiba Mpya; pili,jambo ambalo ninaliona kuwa ni ‘moyo wa Katiba,’ na tatu udhani(au hypothesis) wangu.
Mtazamo
Kwanza, kwa wananchi walio wengi, mchakato wa Katiba mpyaulitoa matumaini ya mwanzo wa kujenga Tanzania Mpya: nchina jamii zitakazojikita kwenye kujali wavuja jasho, zenye msingiwa haki ya kijamii (social justice), na sio tu haki ya kisheria (legaljustice). Tulitarajia kwamba tutatafakari kwa makini hali halisiya watu wetu kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita ambacho
kimetufikisha kwenye hali hii ya leo. Tulifikiri tutatafuta njia
mbadala itakayorudisha imani na matumaini ya watu katikamifumo yetu ya utawala, siasa na uchumi - mfumo unaowekamazingira na nafasi pana kwa wananchi walio wengi kuendelezamapambano yao ya kujikomboa.Kwa dhati kabisa, tungechagua njia mbadala itakayojengamshikamano palipo na utengano; itakayotuelekeza kwenye usawa,palipo na mpasuko wa kitabaka, itakayo imarisha Muunganokwa mtazamo wa Umajumui wa Afrika, palipo na mwelekeowa kurubuni wananchi na kugawanya madaraka. Na tulitarajiakwamba Katiba Mpya itatangaza rasmi matumaini haya nadhamira hii bila kupinda dhana au kutafuna maneno.Haya ndio yalikuwa matumaini yetu ya Katiba Mpya na haya ndioyatakayoniongoza katika kuchambua Rasimu. Ila nitatumia piautaalaam wangu wa kisheria, nilioupata kutokana na wananchiwenyewe waliogharimia elimu yangu. Huu ndio mchango wangumdogo kwa jamii iliyonilea.

‘Moyo wa Katiba’
Pili, moja kwa moja, niseme kwamba moyo wa katiba yetu, aumchakato wowote wa kuwa na katiba mpya, ni Muungano. Hililinatokana na hali halisi ya kihistoria ya katiba zetu. Suala laMuungano ndilo limesheheni mambo muhimu ya mfumo wakidemokrasia na jamii. Kwa hivyo, muundo wa Muungano siosuala la idadi ya serikali – moja, mbili, tatu, mbili na nusu n.k. –bali ni suala la demokrasia.Isitoshe, maoni yaliyokuwa yanakusanywa yalikuwa juu ya Katibaya Muungano, wala sio katiba ya Tanganyika au katiba ya Zanzibar.Na Rasimu iliyokabidhibiwa kwetu kwa ajili ya kujadiliwa pia niRasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hivyo,uchambuzi wangu, kwa sehemu kubwa, ni kuhusu Muungano.

Udhani (hypothesis)
Baada ya kuisoma Rasimu kwa kina, mimi nadhani kwambamasharti mengi ya Rasimu na muundo wake mzima ni matokeo yamivutano mikali katika Tume. Bahati mbaya hatuna mwenendo wamajadiliano ya Tume wala taarifa yao rasmi, hata taarifa ya awali.Lakini usomaji wangu wa awali unaniambia kwamba Rasimu hiini maelewano kwa maana ya
compromise, na sio mapatano, aumwafaka, kwa maana ya consensus. Nijieleze kidogo.Katika maelewano au compromise, pande zinazokinzana hatimayezinakubali kwa shingo upande ili kutokukwamisha maamuzi.Pande zote zinapata kidogo na kupoteza kidogo, na kila upandehuwa na mkakati wake wa kupata zaidi katika duru ya pili.
Kwa hivyo, maelewano kamwe hayawezi kuwa kwa moyo safi.
Maelewano au
compromise, yanazaa uamuzi legelege.Mapatano au consensus, kwa upande mwingine, ni maafikianoyanayofikiwa baada ya mjadala mrefu, kila mmoja akilenga
kuthibitisha hoja yake na kwa njia hii kusadikisha wenzake
8
kwamba hoja yake ni sahihi. Baada ya kufikia uamuzi wa mwafaka,
kila mmoja anatoka akiwa ameridhika na amefurahi. Katika
compromise
, kila mmoja anatoka amenuna. Ni wazi kwambahuwezi ukapata mwafaka fastafasta. Lazima utachukua muda.Ili nieleweke vizuri, nitoe mifano miwili, mmoja mwepesi,mwingine mzito. Ib. 1(3) ya Rasimu inasema:Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katikaIbara ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa kadriitakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo waMakubaliano hayo.Maana ya aya hii ni:Hati ya Makubaliano ya 1964 ni msingi wa Katiba hii (yaaniRasimu); naKatiba hii ni mwendelezo wa Makubaliano.Ukiangalia kwa jicho la kisheria, , ukisema Hati ndio msingi, maanayake ni kwamba Hati bado inaendelea kuwa na nguvu ya kisheriana ndio sheria kuu inayotawala Katiba. Lakini Hati iliweka serikalimbili; sasa, iweje rasimu inayozungumzia serikali tatu iwe namsingi ambao ulijengeka kwenye serikali mbili?La pili, Katiba iliyojikita kwenye serikali tatu haiwezi, kwa vyovyotevile, ikawa mwendelezo wa Hati.Ni kweli kabisa kwamba Hati ya Makubaliano ya 1964 ni chanzocha Muungano. Historia hii, kama inavyostahili, imewekwa kwenyeUtangulizi. Lakini masharti ya katiba yenye nguvu za kisheriahayawezi tena kurudia historia. Ukitaja maneno kama haya katikamasharti ya Katiba, kimahakama inachukuliwa kwamba nia yakoilikuwa kuipa Hati nguvu ya kisheria. Nina uhakika kabisa kwambahaikuwa nia ya Tume kuifufua Hati ya 1964 na kuipa nguvu yakisheria.
9
Pia, ninaamini kabisa kwamba Tume iliyosheheni wanasheriawazoefu na waliobobea huenda walijua na kuelewa kabisawalichokuwa wanaandika. Kwa hivyo, haiwezekani kwambawalikosea, au kuteleza, bali ilikuwa ‘kusalimu amri’ na “kuelewana”ili mambo yaendelee. Ndivyo tulivyopata ibara legalege ambayokisheria haina kichwa wala mkia.Inawezekana kabisa kwamba ibara hii isiwe na madhara makubwakwa sababu majaji wenye busara, kwa hakika, hawatatia maananisharti kama hili. Lakini unaweza kupata jaji ambaye anaegemeazaidi kwenye ufundi na kuitafsiri ibara hii kama ilivyo. Madharayake yanaweza kuwa makubwa. Vyovyote vile, ibara kama hiiisiyoeleweka inashusha hadhi ya Katiba.Mfano wa pili, mzito zaidi, ni kuhusu mipaka ya madaraka. Eneola utawala wa Serikali ya Shirikisho limetajwa kuwa ‘eneo lote laTanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lotela Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari’ (ib. 2). Lakinieneo la utawala wa serikali ya Bara na serikali ya Zanzibarhalikutajwa. Bila shaka, katiba za Washirika zitataja maeneo yaona kuna uwezekano mkubwa kwamba kutakuwa na msuguanona kutoelewana hasa juu ya mipaka ya bahari katika ‘Zanzibarchannel’. Katiba ya Zanzibar ya Mwaka wa 1984 iliopo, kwa mfano,inataja mipaka ya Zanzibar kuwa ni ‘eneo lote la Visiwa vya Ungujana Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yakeambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwaJamhuri ya Watu wa Zanzibar.’ (ib.1)Pande mbili za Muungano zimewahi kutofautiana kuhusu eneolao la bahari, hasa kwa sababu inadhaniwa kwamba bahariinayopakana na maeneo ya Tanganyika na Zanzibar ina mafuta narasilimali nyingine. Waziri Tibaijuka alipopeleka ombi Umoja waMataifa kuongeza eneo la nchi kwa maili 150, mjumbe mmoja waBaraza la Wawakilishi aliwasilisha hoja binafsi kumlaumu Waziri wa Zanzibar mhusika kwa kuridhia ombi hilo.

Ukimya wa Rasimu juu ya kueleza kwa uwazi mipaka ya utawalawa Washirika ni wa ajabu kweli kwa sababu ni wazi kwambahuwezi kuzungumzia utawala wa mamlaka yoyote yale bilakubaini mipaka yake. Ukimya huu unaweza kuzaa migogoro.Nitaendelea kutoa mifano mingine katika uchambuzi wanguunaofuata.
***
Sasa, ni juu yangu kuthibitisha udhani (au hypothesis) wangu.Kabla sijaanza kufanya hivyo, ningependa kusema kwa dhatikabisa kwamba Tume hii ya watu 32 wenye kuwakilisha maslahitofauti na hisia mbalimbali ilifanya kazi katika mazingira na halingumu sana. Hayo yalitegemewa kutokana na mfumo wenyewe waTume. Wachache wetu tulitahadharisha mapema lakini viongoziwaliosheheni busara wakaamua vinginevyo.Katika hali hii, mhadhara wangu usichukuliwe hata kidogo kamakuibeza au kuipuuza kazi waliyofanya akina Mzee Warioba nawenzake. Sina shaka kwamba wengine wao walipoteza usingizina hata kuteseka moyoni mwao kuhusu maaumuzi menginewaliyoyafanya. Kwa hili, wanastahili pole zetu, zaidi ya pongezi.
II.
UKUU WA KATIBA(SUPREMACY OF THE CONSTITUTION)
Magwiji wa katiba (Wheare 1966, Singh 1994: A-29 na kuendelea,Nwabueze 2003: juz. 1, sura 3, Seervai 1997: juz. 1, sura v, Shivji
1990/2009) wanaafiki kwamba mfumo wa shirikisho una angalau
sifa ku nne. Hizo ni:

Kwamba mwananchi anatawaliwa na serikali mbili, yaani serikaliya shirikisho na serikali ya mshirika;Kwamba kuna mgawanyo wa madaraka miongoni mwa serikali;Kwamba Washirika, na katiba na sheria zao, zina hadhi sawa; naKwamba Katiba ya Shirikisho ni sheria kuu (supreme law).Je, Rasimu inakidhi sifa hizi? Kwa maoni yangu, kwa kiasi kikubwa,mfumo wa shirikisho katika Rasimu unakidhi sifa tatu za awali.Kila mwananchi pande zote mbili atatawaliwa na serikali mbili;Wabara watatawaliwa na Serikali ya Shirikisho na Serikali ya Bara,Wazanzibari watatawaliwa na Serikali ya Shirikisho na serikali yaZanzibar. Pia kuna mgawanyo wa madaraka kati ya serikali tatu.Washirika, yaani Bara na Zanzibar wana hadhi sawa (ib. 61(5)).Sifa inayotatanisha ni ya mwisho, ile inayosema kwamba Katibaya Shirikisho ni sheria kuu. Nitazichambua ibara zinazohusika.Kabla sijafanya hivyo, nieleze kwa muhtasari tu maana na dhanaya Ukuu wa Katiba (supremacy of the constitution).‘Ukuu wa Katiba’ maana yake ni sheria zote, madaraka, majukumuna mamlaka yanatokana na katiba na katiba ndio chanzo chauhalali wa utawala. Katiba yenyewe inapata mamlaka yake kutokakwa wananchi katika ujumla wao. Ndiyo maana, katika msamiatiwa kawaida, tunasema katiba ni sheria mama. Nikitumia msamiatihuo kwa katiba ya shirikisho, naweza nikasema kwamba katibaya shirikisho ndio mama na baba wa shirikisho. Katiba na sheriaza Washirika, ingawa zina mamlaka kamili katika maeneo yao,zinatokana na katiba ya shirikisho na zinapata uhai wao wa kisheriakwa mujibu wa katiba ya shirikisho. Muhimu zaidi ni kwamba,kama kuna masharti ya katiba au sheria za Washirika ambazozinakinzana na katiba au sheria za shirikisho zilizopitishwa kwamujibu wa katiba ya shirikisho, basi sharti husika inakuwa batilikwa kiasi kile. Kwa lugha ya kimombo dhana hii inaitwa
supremacy

clause,
yaani kipengele cha ukuu wa katiba ya shirikisho. Katikakatiba zote za shirikisho duniani kuna kipengele cha ukuu;Marekani, Australia, India, Canada n.k. Sitazinukuu zote isipokuwambili, Katiba za Marekani na Australia. Ibara ya VI ya Katiba yaMarekani inasema:
This Constitution, and the Laws of the United States whichshall be made in Pursuance thereof; and all Treaties made,or which shall be made, under the Authority of the UnitedStates, shall be the supreme Law of the Land; and theJudges in every State shall be bound thereby, any Thingin the Constitution or Laws of any State to the Contrarynotwithstanding.
Na kifungu 109 cha Katiba ya Australia kinasema hivi:When a law of a State is inconsistent with a law of theCommonwealth, the latter shall prevail, and the formershall, to the extent of the inconsistency, be invalid.Kwa kifupi, vipengele vyote viwili vinasisitiza ukuu wa katibaya shirikisho. Na hii ina mantiki na umuhimu wake usiopingika.Ukitaka shirikisho liwe imara na liwe na nguvu, basi hakunabudi Washirika wakubali kutambua na kutii masharti ya katibaya shirikisho. Bila hivyo, shirikisho litayumba na kutakuwa namigogoro kutokana na vipengele vya katiba na sheria na vitendovya vyombo vya Washirika kukinzana na kugongana kila mara.Sasa tuangalie vipengele vya Rasimu vinasemaje kuhusu ukuu waKatiba ya Shirikisho. Ibara 8(1) inasema:Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika waMuungano kwa mambo
yasiyo ya Muungano, Katibahii itakuwa sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano.(Msisitizo wangu)

Hii ina maana kwamba ukuu wa Katiba ya Shirikisho ni kwamambo saba tu ya muungano yaliyotajwa katika nyongeza; lichaya mambo hayo, katiba za Washirika ni sheria kuu katika maeneoyao kwa mambo yote mengine yaliyosalia (
residual powers).Tuendelee. Ibara ya 61(4) inasema:Washirika wa muungano watatekeleza majukumu yaokwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.‘Kuzingatia’ sio kubanwa; Kiingereza chake ni ‘to take accountof’, ‘to bear in mind’. Unaweza ukazingatia masharti ya Katibaya Shirikisho na baada ya hapo ukatenda kinyume chake, lakinihata hivyo utakuwa hujavunja katiba. Hii inaeleweka zaidiukisoma ibara ndogo inayofuata inayotaka Washirika kutekelezamajukumu yao kwa masuala yasiyo ya Muungano ‘kwa mujibu’wamasharti ya katiba zao. ‘Kwa mujibu’ inaleta maana ya kubanwa,huwezi ukakiuka. Kwa hivyo, masharti ya Katiba ya Shirikisho
yanakushawishi
; masharti ya katiba ya Mshirika yanakushurutisha.Niangalie ibara nyingine ya mwisho ambayo inakaribia kidogokuuzungumzia ukuu wa Katiba ya Shirikisho. Ibara 109(5)inasema:Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Tanzania Barana Katiba ya Zanzibar, Katiba hii itakuwa na nguvuya sheria katika Jamhuri ya Muungano kwa mamboyanayohusu Muungano na endapo sheria nyingineyoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii,basi sheria hiyo nyingine, kwa kiasi kinachokiukaKatiba hii, itakuwa batili.Kuna dhana mbili zilizotumika katika kipengele hiki: ‘mamboyanayohusu’ (Muungano) na ‘sheria’. Bila shaka ‘mamboyanayohusu Muungano’ ni dhana pana zaidi kuliko ‘mambo ya

Muungano’. Mambo ya Muungano ni yale saba yaliyotajwa katikanyongeza. Mambo yanayohusu Muungano ni hayo saba pamojana yale yote yaliyozungumziwa katika Katiba ya Shirikisho. Kwamantiki hiyo hiyo, neno ‘sheria’ haliwezi likawa na maana panazaidi ya sheria inayohusu mambo ya Muungano yanayotungwa naBunge la Shirikisho kwa mujibu wa ibara 109. Kwa hivyo, ukuu waKatiba ya Shirikisho unaozungumziwa katika ibara hii ni juu yashughuli za Muungano tu. Sheria yoyote juu ya mambo yanayohusuMuungano ikikiuka masharti ya Katiba ya Shirikisho, sheria hiyoni batili. Lakini hii haihusu katiba na sheria za Washirika.Uchambuzi wangu wa ibara hizi zote zinazohusu hadhi ya Katiba yaShirikisho katika uhusiano wake na katiba na sheria za Washirika,unaweza kuhitimishwa kama ifuatavyo:Mosi, hakuna popote pale katika Rasimu tunapokuta Ukuu waKatiba ya Shirikisho (kwa maana ya
supremacy clause) umewekwakwa uwazi na ufasaha, kama ilivyo katika katiba nyingine zashirikisho nilizozitaja hapo awali.Pili, vipengele vinavyohusika, ama vinatatanisha au viko kimya, auyote mawili, kuhusu kipengele cha ukuu.Tatu, hii, kwa maoni yangu, haikutokea kwa makosa au kwakuteleza bali ni tokeo la maelewano kwa maana ya compromise.Nathubutu kusema kwamba kama jambo hili lingejadiliwa katikaTume, kungekuwa na mvutano mkali sana.Mwisho, utatanishi na ukimya huu utapalilia vyanzo vya migogorona mivutano kati ya mamlaka ya Washirika na Muungano siku zausoni. Athari zake haziwezi kuepukika. Nitatoa mifano michachemuhimu kadri ninavyoendelea na mhadhara wangu.

A.Tunu, Dira, na Malengo
Rasimu ina Tunu, Dira na Malengo ambayo yamesistizwa sanana Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Mzee Warioba. Yaliyomokatika Tunu, Dira, na Malengo ni udugu, utu, umoja, uzalendo,uwazi, n.k. na haya yamerudiwarudiwa. Kwa upande wangu,sitasemea hayo. Kwa kadri nijuavyo, hakuna utawala popote paleduniani, uwe wa kibepari, kijamaa au wa mabavu, utakaopingahizi Tunu, hata kama hawatekelezi. Lakini jambo mojawapoambalo liko kwenye utangulizi (ib. 1(2)) na Malengo (ib. 11(1)) nisuala zima la kujitegemea. Kwa mfano, lengo kuu mojawapo katikaMalengo (ib. 11(1)) linasema na ninanukuu:Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha nakudumisha udugu, amani, umoja na utengamano wawananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatiaustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenyedemokrasia, utawala bora na
kujitegemea (msisitizowangu).Nimechagua ibara hii kuizungumzia kwa sababu kujitegemeakuna nafasi ya kipekee katika historia yetu ya kisiasa. Mwalimuna Sokoine walikuwa wanasistiza sana umuhimu wa kujitegemeakwa hoja kwamba tusipojitegemea tutapoteza uhuru wetu.Pamoja na hili, kwetu sisi mtazamo wa kujitegemea uliendanana ujamaa, ujamaa na kujitegemea. Haya mawili yalikuwa kamachanda na pete. Sasa ujamaa umefutwa kabisa katika Rasimu kwahoja kwamba ni itikadi (kana kwamba soko huria, ubinafsishajin.k. sio itikadi). Kwa vyovyote vile, kidole kimekatwa, tumebakina pete inahengihengi.Niendelee na mfano wangu. Sura ya Pili inazungumzia MalengoMuhimu. Malengo yapo katika Katiba ya sasa lakini Malengoyalivyowekwa katika Rasimu, yanaturudisha nyuma hatua mbili.
16
Kwa nini? Kwanza, katika Rasimu Malengo ni mwongozo kwahivyo hayabani kisheria. Katika Katiba iliopo Malengo yana nguvuya sheria (ib. 7(1)) ingawa sio kimahakama (ib 7(2)). Pili Malengokatika Rasimu ni kwa ajili ya vyombo vya Muungano tu (ang. ib.10(1) na ib. 238(1) maana ya neno ‘serikali’). Katika katiba iliopoMalengo yalibana vyombo vyote vya serikali zote mbili.Lakini hata kama yangekuwa yanabana vyombo vya Washirika,bado yasingekuwa na nguvu ya sheria kwao. Hii ni kwa sababuya kutokuwa na kipengele cha ukuu. Kwa mfano, inaweza kutokeawashauri waelekezi wa ndani na nje wakaishauri serikali yaTanganyika
kwamba mtazamo wa kujitegemea umepitwa nawakati katika dunia ya utandawazi. Katika utandawazi kunakutegemeana, sio kujitegemea. Isitoshe, washauri wataendelea,tukiweka mtazamo wa kujitegemea, ambao unahusishwa naujamaa, katika katiba, kuna hatari ya kutoweza kuvutia uwekezajikutoka nje. Kutokana na ushauri huo, katika katiba ya Tanganyika,lengo kuu linaweza likasomeka hivi:
Lengo kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu,amani, umoja na utengamano wa wananchi wa Tanganyika kwakuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Tanganyika huru yenyedemokrasia, utandawazi bora na
kutegemeana.
Pasipo na shaka, lengo hili linagongana na lengo kuu la Katiba yaShirikisho. Hata hivyo, ndio lengo litakalo ongoza vyombo vyaTanganyika kwa sababu Katiba ya Shirikisho haiko juu ya katibaza Washirika; yaani, inakosa ukuu.Kwa mujibu wa lengo jingine (ib. 11(1)(xi), Serikali inaagizwa‘kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezajiwa haki ya mtu kujipatia elimu …’. Serikali inayomaanishwakatika kipengele hicho ni Serikali ya Muungano, lakini Serikaliya Muungano haisimamii elimu kwa sababu elimu sio jambo la
Muungano. Na inawezekana kabisa katiba za Washirika zisiwe nalengo linalofanana na hili. Kwa hivyo, lengo hili jema halina maana- chombo kinachoagizwa kutekeleza lengo, hakisimamii elimu,na vyombo vya Washirika vinavyosimamia elimu havibanwi nalengo. Kwa hivyo, jambo linalopendeza kulisikia ni ganda tupu bilatunda!Kwa hitimisho, nigusie ibara (10)(2) ambayo inaagiza Serikali yaMuungano kutoa taarifa Bungeni juu ya utekelezaji wa Malengoangalau mara moja kwa mwaka. Swali ni kwamba malengo yotemuhimu yanaangukia chini ya mamlaka ya Washirika ambaoni watekelezaji na hawabanwi na Katiba ya Shirikisho. Katikaukweli huu, hii taarifa itakayowasilishwa Bungeni itakuwa na ninina itakuwa na maana gani. Kwa kifupi basi, watekelezaji wakuuwa Malengo hawabanwi na masharti haya; yule ambaye siomtekelezaji ndiye anayebanwa!
B. Maadili na Miiko ya Uongozi
Mzee Warioba pia amechangamkia maadili na miiko ya viongoziiliyowekwa katika Rasimu, Sura ya Tatu. Kuna ibara kama nanepamoja na ibara ndogo chungu nzima juu ya suala la maadili namiiko. Hizi zinawahusu viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwana ambao watatajwa katika sheria ya Bunge (ib.14(3)). Bungelinalozungumziwa hapa ni Bunge la Muungano. Lakini Katiba zaWashirika hazihitaji kufuata au kuwa sambamba na vipengelehivyo. Wana hiari kuweka au kutokuweka, au kurekebisha aukuchagua vipengele wanavyotaka kwa sababu maadili na miiko siojambo la muungano na Katiba ya Shirikisho haiwabani Washirika.Kwa mfano, ib.20(2)(a)(iii) inasema kwamba kiongozi wa ummahapaswi ‘kujilimbikizia mali kinyume na sheria’. Sasa, sheria ipiinayozungumziwa hapa? Je kama hakuna sheria ya Washirikainayokataza viongozi wa umma kujilimbikizia mali, kipengele

hiki katika Katiba ya Shirikisho kitakuwa na uzito gani? Ni wazi,haiwezi ikawa na nguvu yoyote katika maeneo ya Washirika.Sasa nimulike kwenye haki za binadamu.
C. Haki za Binadamu
Wakereketwa wameshangilia sana haki za binadamu katikaRasimu na wana sababu nzuri tu kufanya hivyo. Rasimu imeelezakwa ufasaha haki za binadamu na imeongeza haki nyingineambazo hazimo katika katiba zilizopo. Kuna mapungufu hapa napale lakini haya yanarekebishika. Kwa mfano, haki ya wananachikuandamana kuonyesha hisia zao za kulaumu au kutoridhika najambo fulani haikuwekwa. Pia hakuna haki ya wafanyakazi kugomakama silaha yao muhimu ya kushinikiza waajiri wao kutekelezamatakwa yao.Kuna haki mbili muhimu ningependa kuzitaja hapa. Ib. 39(3)inaeleza kwamba raia wa Jamhuri ya Muungano ‘hatapelekwakatika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojianoya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.’ Hili ni jambo jema;hususan inapiga marufuku ile inayoitwa ‘rendition’.
Pendekezolangu ni kuongeza vipengele viwili kuweka wazi kwamba nimarufuku raia wa Jamhuri (a) ‘kufungwa au kuwekwa kizuizininchi ya nje bila ya kufuata sheria ya nchi hiyo; na (b) ‘kuhojiwa
na maafisa wa ujasusi au usalama wa nchi za nje katika eneo la
Jamhuri’.

Lakini suala ambalo linatatanisha ni: Hati hii nzuri ya haki zabinadamu ina uzito gani katika maeneo ya Washirika? Haki zabinadamu sio jambo la Muungano na Katiba ya Shirikisho sio Katibamama. Je, kama katiba za Washirika zikikosa vipengele vinginevya haki au kuandikwa tofauti na kuwa na maana na tafsiri tofauti,itakuwaje?
Nitoe mfano. Katika kutekeleza haki ya mwananchikushiriki katika utawala, wagombea huru wanaruhusiwa na

Rasimu katika ngazi zote za utawala. Iwapo katiba za Washirikahazina kipengele kama hicho, basi mgombea huru atakuwa nahaki ya kugombea uchaguzi katika ngazi ya Bunge la Muunganona Urais wa Muungano tu, lakini hakuna mgombea huru atakuwana haki kugombea nafasi za serikali za mitaa au mabunge yaWashirika au urais wa Tanganyika au Zanzibar.
Huu ni mfanomwingine wa wananchi kupewa ganda bila tunda.
Sasa nimefikia sehemu muhimu ya mhadhara wangu, muundo na
taasisi za muungano.
III.

MUUNDO NA TAASISI ZA SHIRIKISHO
Hitimisho langu juu ya muundo wa muungano ni kwamba, mosi, nitegemezi na, pili, ni dhaifu kwa sababu umejengwa juu ya msingiwa mchanga wa dhamira na nia nzuri badala ya msingi wa maweya nguvu za kikatiba zilizowekwa na wananchi wenyewe. Ni kamakwamba suala la Muungano ni ujirani mwema badala ya umojawa nchi. Nitalifafanua kwa kuchambua mifano ya maeneo kamamanane hivi.
A.Taasisi Kuu za Kusimamia Muungano
Muungano wa Jamhuri ya Muungano umeainishwa kama shirikisholenye serikali tatu (ib. 57(1), serikali ya muungano au shirikisho,serikali ya Tanzania Bara na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7
Kwa maoni yangu, kwa usahihi zaidi, hizi zingeitwa dola tatu kwasababu zote zina mihimili mitatu ya dola, yaani, serikali, bunge namahakama, na mamlaka yao ya utawala. Kwa kukwepa kuainishana kutaja kwa jina lake dhana inayokusudiwa, ina athari zakeza kutokuelewana na kuzaa mizozo isiokuwa ya lazima. Mfanomzuri ni yale malumbano yaliyotokea juu ya Zanzibar kuwa nchiau sio nchi.
Inawezekana, kwa busara zake, Tume ilichagua kwa

maksudi msamiati uliozoeleka kuepuka malumbano juu ya maanaya dola na nchi. Tuachane na hili, tuendelee.Kuna taasisi mbili za mahusiano baina ya serikali hizi tatu -, Tumeya Uhusiano na Uratibu wa Serikali (ib.102(1) na Mawaziri Wakaazi(ib. 64). Mawaziri Wakaazi watateuliwa na Washirika na watakuwa
na ofisi zao Makao Makuu ya Serikali ya Muungano. Eneo la Makao
Makuu halijulikani kama litakuwa katika eneo la Tanganyikaau Zanzibar, au litakuwa linahamahama kati ya Tanganyika naZanzibar. Vyovyote vile, itabidi serikali ya muungano iombe
serikali za Washirika kuipatia eneo lake la kujenga ofisi za makao
makuu pamoja na Ikulu ya Rais wa Muungano.
Jukumu mahsusila hao Mawaziri Wakaazi ni kusimamia uhusiano baina ya serikaliza Washirika, kwa upande mmoja, na kati ya Serikali ya Muunganona serikali ya Mshirika mhusika, kwa upande mwingine.Tume ya Uhusiano ina wajumbe sita - makamu wa rais waMuungano, ambaye atakuwa mwenyekiti, marais wawili waWashirika, Mawaziri wawili Wakaazi na waziri mwenye dhamanaya mambo ya nje ya Muungano (ib. 102(2). Jukumu na lengo kuula Tume ni kusimamia na kuweka taratibu na mazingira mazuriya mashauriano, mashirikiano, na utatuzi wa migogoro baina yaserikali tatu (ib. 103-104). Kwa jumla, Tume ya Uhusiano siochombo cha utendaji (executive) isipokuwa tu kitahusika katikautatuzi wa migogoro ambao nitauzungumzia hivi punde. Katikahali halisi ya ulinganisho wa nguvu za kisiasa, sidhani kwambaTume inaweza kufanya maamuzi yanayobana pande zote husika,
bali, zaidi ni kufikia maelewano, ambayo pia huwezi kuwa na
hakika kwamba yatatekelezwa. Isitoshe, marais hawa watatuwakitoka vyama tofauti (mbali na wagombea binafsi), vyenye sera
na mielekeo tofauti, hata kufikia maelewano inaweza kushindikana
na kusababisha mivutano na migogro isiyokuwa na mwisho.Pili, katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro, tume inaweza

kufanya uamuzi lakini upande wowote ambao haukuridhika unahaki ya kukata rufani katika Mahakama ya Juu na uamuzi waMahakama unakuwa wa mwisho (ib. 104(1)(e) Kwa vyovyote vile,Tume sio ngazi ya kwanza katika kutatua mgogoro kwa sababupande zote hazilazimishwi kuanzia mgogoro katika Tume bali zinahiari ya kuanzia ama katika Tume au katika Mahakama.Kwa kujumuisha, navyoona mie, chombo hiki kikuu cha kiungobaina ya serikali tatu, kitakuwa na changamoto kama tatu hiviambazo zinaweza zikageuka kuwa matatizo.Mosi, kuna suala la protokali. Marais kuwa chini ya uenyekitiwa Makamu wa Rais ina utata. Katika hali ya kawaida, masualaya protokali yasingekuwa ya kuzingatiwa lakini kwa sababuzisizoeleweka wakuu wa nchi zetu wanajali sana protokali, labdakudhihirisha ukuu wao.Pili, ambayo ni muhimu zaidi, hakuna uwiano wa nguvu za kisiasakatika Tume. Kwa vyovyote vile, mwenye nguvu katika Tumeatakuwa Rais wa Bara - yeye ndiye mtawala wa eneo kubwalenye wananchi wengi, yeye ndio mwenye rasilimali nyingi,yeye ndiye anatoa mchango mkubwa wa kuendesha serikali yamuungano, ikiwemo gharama za Tume yenyewe. Kwa hivyo,tupende tusipende, yeye ndiye atakuwa na sauti nzito. Isitoshe,kutokana na muundo wa serikali tatu, rais wa Bara hataona aibukujitutumua kinyume na ilivyo katika serikali mbili wakati raismwenye dhamana ya Bara pia ni rais wa muungano.Tatu, ikiwa Tume inataka kufanya uamuzi wowote, itakuwa vigumukwa sababu kila upande unawakilishwa na watu wawili wawili.Nne, katika hali hiyo, mara nyingi, hasa katika masuala nyeti au
mazito ya kitaifa, hata kufikia maelewano itakuwa vigumu. Kati ya
Washirika, unaweza kukuta kila mara upande dhaifu ambao hojazake zinaelekea kutokubalika, ataomba kikao kiahirishwe ili arudi

kwake kushauriana na wenzake au kupata maoni ya wananchiwake. Kwa wanasiasa, hii inakuwa ni mbinu ya kuahirisha
maafikiano, yaani,
delaying tactics.Kwa jumla, na bila kubeza, tathmini yangu ya Tume hii ni kwambahaina tofauti ya msingi na zile kamati zisizoisha za akina Shekilangojuu ya kero za Muungano.
B. Bunge la Muungano
Mamlaka ya kutunga sheria juu ya mambo yote yanayohusuMuungano yamewekwa chini ya Bunge la Muungano. Mambo ‘yoteyasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Tanzania Barana Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.’ Bila shaka, mamlaka hayayatatumika kwa mujibu wa Katiba zao. Kuhusu Bunge, nitagusiamambo matatu yanayotatiza.Moja, ni majimbo ya uchaguzi wa Bunge la Muungano. Kwamujibu wa ib. 105(3) ‘kila mkoa kwa upande wa Tanzania Barana wilaya kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ni jimbo la uchaguzi’.Wanahabari wetu waliobobea wamekwishapiga hesabu. Kunamikoa 25 Bara na wilaya 10 Zanzibar. Kwa kuwa watakuwepowabunge wawili kutoka kila jimbo, mmoja wa kiume na mwinginewa kike (ib. 104(4), basi tutakuwa na wabunge 70, 50 kutokaBara na 20 kutoka Zanzibar. Pia watakuwepo wabunge watanokuwakilisha kundi la walemavu ambao watateuliwa na Rais wamuungano. Naona tunaweza kutabiri kwamba watatu watatokaBara na wawili watatoka Zanzibar ili kuwe na uwiano na idadiya watu. Jumla tutakuwa na wabunge wa Bara 53, ambayo niasilimia 71, na 22 kutoka Zanzibar, ambayo ni asilimia 29. Kwahivyo, uwiano wa Bara na Zanzibar ni asilimia 71 kwa asilimia 29,Wabara wakiwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wote. Uwianohuu moja kwa moja unapingana na msingi wa kwanza kabisawa shirikisho. Shirikisho linasimama kwenye usawa wa kisiasa

(
political equality) wa Washirika bila kujali ukubwa au idadi yawatu wao. Kwa hivyo, uwakilishi wao hasa katika chombo chakutunga sheria unatakiwa kuwa sawa.Lakini kuna jambo jingine la kutatanisha. Mikoa na wilaya ningazi za utawala ambazo haziko chini ya mamlaka ya Muungano.Ugawaji wa maeneo ya utawala ni mamlaka ya vyombo vyaWashirika, hususan Rais. Kwa mfano, kwa mujibu wa ibara 2Aya Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais ndiye mwenye mamlaka yakugawa maeneo ya mikoa na wilaya. Sioni sababu ya Zanzibarkukibadilisha kipengele hiki kwa sababu hawashurutishwi naKatiba ya Shirikisho (Rasimu) kufanya hivyo. Isitoshe, hakunachochote katika Rasimu kumzuia rais au marais wa Washirikakubadilisha mipaka na kuongeza idadi ya mikoa au wilaya katikamaeneo yao.Tuchukue mfano. Kwa sababu zozote zile, rais wa Zanzibaranaamua kugawa Zanzibar katika wilaya 20. Hii itamaanishakwamba kutakuwa na wabunge 40 kutoka Zanzibar, ikifanya jumlaya wabunge kuwa 95 badala ya 75 katika Bunge. Mabadiliko hayamara moja yatakuwa yamebadili uwiano kati ya Bara na Zanzibar- asilimia 56 kutoka Bara na 44 kutoka Zanzibar. Na, je, jambohili likitokea katikati ya muda wa Bunge, kutakuwa na uchaguzimpya? Nimesema rais anaweza kufanya hivyo kwa sababu zozotezile lakini pia anaweza kufanya hivyo kwa maksudi ili kujiongezeauwakilishi katika Bunge la Muungano. Kwa lugha ya kimombo, hiiinaitwa gerrymandering. Vilevile, kwa upande wa Bara, rais waTanganyika anaweza kuongeza idadi ya mikoa.Pili, Rasimu inaruhusu wagombea huru na pia uwezo wa wapigakura kumuondoa mbunge wao hata kabla ya kipindi chake kwasababu zilizotajwa (right of recall) (ib. 124). Mambo haya yotemawili yanahusika na wabunge wa Bunge la Muungano nasio mabunge ya Washirika. Kwa hivyo, Washirika wanaweza

wakaamua bila kuvunja katiba ya Shirikisho kwamba katikamaeneo yao hawatakuwa na wagombea huru wala haki yawapigakura kuondoa wabunge wao. Na hii sio nadharia tu.Viongozi watarajiwa wamekwishaanza kuonyesha wasiwasi waokuhusu mgombea huru na haki ya wananchi kuweza kumuondoambunge wao kabla ya muda.Jambo la tatu linawagusa wananchi kwa karibu sana. Ib. 107(2)(h)inaeleza kwamba miongoni mwa madaraka ya Bunge ni ‘kujadilina kuridhia mikataba yote inayohusisha rasilimali na maliasilizinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.’ Jambo hilini jema kabisa na la kulifurahia, angalau mikataba hii izungumzweBungeni kwa uwazi badala ya wananchi kuambiwa kwamba nisiri ya kibiashara. Lakini, rasilimali na maliasili – ardhi, mafuta,madini, gesiasilia, maji, mapori, n.k. – sio jambo la Muungano.Rasilimali na maliasili ni chini ya mamlaka ya Washirika nawao ndio watayasimamia. Katika hali hii, Serikali ya Muunganoitaingia kwenye mikataba ipi na kuhusu rasilimali gani? Ni mfanomwingine wa wananchi kulishwa maneno matamu yasiyo nauhalisia. Ni haki hewa.Sasa niangalie taasisi nyingine nyeti na muhimu, jeshi la polisi.
C. Jeshi la Polisi
Nianze kwa kuweka wazi kwamba polisi haimo miongoni mwa yalemambo saba ya Muungano kinyume na katiba ilioko (Nyongezaya Kwanza, jambo la nne). Pamoja na kutamka kwamba Jeshi laPolisi ni chini ya mamlaka ya Muungano na jeshi ndilo litakuwana jukumu la ‘ulinzi wa watu na mali zao’ (ib. 227(1), Rasimuinasema kwamba ‘Washirika … wanaweza kuanzisha vikosi vyaulinzi vitakavyosimamia masuala ya usalama wa watu na malikatika maeneo yao.’ (ib. 232(1) Bila kutafuna maneno, ibara hiini wazi na maana yake ni kwamba Washirika wanaweza wakawa

na majeshi yao ya polisi, ilimradi yasiitwe polisi kwa jina, ingawayana majukumu na muundo unaofanana kabisa na ule wa Jeshi laPolisi. Kwa hivyo, utakuta kuna majeshi matatu ambayo majukumuyao ni yale yale. Katika hali hii huwezi kuepuka migongano nakama tujuavyo vikundi vyenye silaha vikigongana, unaoathirika niusalama wa wananchi. Bila shaka, waandishi wa Rasimu walionauwezekano huo; usuluhishi wao ni kuongeza kipengele kinginekinachosema, ‘Vikosi vya ulinzi vya Washirika wa Muungano,vitatekeleza majukumu yao kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi laJamhuri ya Muungano ili kuepusha mgongano wa mamlaka …‘ (ib. 232(2). Tuwe wa kweli, jambo muhimu kama uwezekanowa migongano kati ya majeshi unaweza kweli kuliachia nia nadhamira njema ya kushirikiana? Tena kikatiba? Busara inahitajikwamba angalau kikatiba unaweka mazingira na masharti yakuepuka migongano, sio kuweka mazingira ya migongano na halafuukasema washirikiane ili kuepuka migongano. Haileti maana walahaina mantiki. Ndio maana huwezi ukawa na vikosi vya usalamazaidi ya kimoja vyenye majukumu yale yale wakifanya kazi katikamaeneo yale yale. Kama busara ingetumika, basi ‘polisi’ ingewekakatika orodha ya mambo ya muungano na lingeundwa jeshi mojatu la polisi la Jamhuri ya Muungano. Na ingekuwa marufuku mtu,taasisi au serikali nyingine yoyote kuunda vikosi vya usalamahuru nje ya jeshi la Jamhuri.Kwani wajumbe wazito wa Tume hawakuwa na busara auhawakuliona hili? La hasha, wajumbe wengine katika Tumewana busara tele, utaalam wa mambo ya kikatiba na tena wanauzoefu wa kuendesha nchi kwa zaidi ya robo karne. Kwa hivyo,ninashawishika kueleza vipengele hivyo kama maelewano, tenazaidi ya maelewano, kuhalalisha kinachoitwa ‘idara maalum’katika Katiba ya Zanzibar ilioko (Sura ya Kumi). Idara maalumya Zanzibar inajumuisha Jeshi La Kujenga Uchumi (JKU), KikosiMaalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Chuo cha Mafunzo (cha

wahalifu) (ib. 121(2). Rais wa Zanzibar ana mamlaka kamili juu yaidara maalum na tena kikatiba anaitwa ‘Kamanda Mkuu wa IdaraMaalum’.Rasimu hii ikipita kuwa sheria kama ilivyo, mimi sitashangaaikiwa Zanzibar itarekebisha Katiba yao katika ibara ya 26(1)ambayo ilivyo inasomeka: ‘Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambayeatakuwa Mkuu wa Nchi ya Zanzibar, Kiongozi Mkuu wa Serikaliya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.’ Baada yamarekebisho, ibara inaweza ikasomeka: ‘Kutakuwa na Rais waZanzibar ambaye atakuwa Mkuu wa nchi ya Zanzibar, KiongoziMkuu wa Serikali ya Mapinduzi, Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.’Na hii haitakuwa kinyume cha Katiba ya Shirikisho kwa sababu,moja, polisi sio jambo la muungano na, pili, Katiba ya Shirikishoyenyewe inaruhusu.Vilevile Tanzania Bara wanaweza likaufuata nyanyo na kuwa navikosi vyao vya usalama na ulinzi. Hali halisi ilivyo, vikosi hivyovya Bara au Tanganyika vitakuwa na uongozi wa kitaalam, silahaza kisasa na nguvu zaidi kuliko Jeshi la Polisi la Jamhuri ambalolitajikuta halina fedha za kujiendesha.Nitatoa mfano mmoja wa kuonyesha migongano hatarishiinayoweza kutokea katika hali halisi. Ingawa mfano huu ni wakudhania, sio kama hauwezekani kutokea. Rais wa Jamhuri kwatathmini yake anaona kuna hali ya hatari katika eneo mojawapo laBara ambao inahitaji kudhibitiwa mara moja. Kwa mujibu wa ib.81, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa,kikao ambacho hakikuhudhuriwa na Rais wa Bara, anatangazahali ya hatari na kupeleka kikosi cha FFU kuidhibiti. Utangazwajiwa hali ya hatari sio jambo la muungano (kinyume na Katibailioko ambayo inasema mamlaka juu ya hali ya hatari ni jambola Muungano, Nyongeza ya Kwanza). Rais wa Bara pia anapeleka

kikosi chake cha usalama kudhibiti hali hii na kumtaka Rais waJamhuri aondoe mara moja kikosi cha FFU. Rais wa Jamhurianakaidi ushauri huu. Kwa vyovyote vile, kutatokea mgongano kwasababu katika hali halisi vikosi vyote viwili vina hadhi sawa, kikosicha Bara kwa mujibu wa Katiba ya Bara na kikosi cha Jamhuri kwamujibu wa katiba ya muungano. Lolote linaweza kutokea katikahali kama hii ambalo haliwezi kutabirika.
D. Mahakama ya Rufani na Mahakama ya Juu
Mahakama katika ngazi ya Jamhuri ni mbili, Mahakama ya Juuna Mahakama ya Rufani. Mahakama ya Rufani ni mahakamainayosikiliza rufani kutoka mahakama kuu za Washirika kamatulivyozoea isipokuwa sio ngazi ya mwisho. Uamuzi wa Mahakamaya Rufani unaweza kupingwa katika Mahakama ya Juu na uamuziwa Mahakama ya Juu ni wa mwisho.Mahakama ya Juu ndio mahakama mpya. Pamoja na kusikilizarufani zote kutoka Mahakama ya Rufani, ina majukumu mahsusiya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua mambo matatu –– kusikiliza na kuamua mara ya kwanza na mwisho mashauriyanayohusu uchaguzi wa Rais wa Jamhuri;– kusikiliza na kuamua mashauri kuhusu tafsiri ya Katibaya Shirikisho yanayoletwa na serikali yoyote kati ya tatuzilizopo;– kusikiliza na kuamua migogoro baina ya serikali hizoinayoletwa na mmoja wao.Pia ina mamlaka ya kutoa maoni ya kishauri kwa Serikali yaMuungano au Serikali za Washirika. Rasimu haiko wazi kwambainatoa maoni pale tu inapoombwa au inaweza kufanya hivyo kwautashi wake yenyewe.Mahakama ya Juu ina Jaji Mkuu na Naibu wake na majaji saba

wengine, jumla ya majaji wakiwa tisa. Mahakama ya Rufani inaMwenyekiti na majaji wengine 17. Kwa jumla kuna majaji 27 katikaMahakama za Jamhuri (Sio mzigo mdogo huu!) Kuna vipengelevinavyosisitiza uwiano wa uwakilishi kutoka pande mbili zamuungano.Jambo la kutatanisha katika muundo huu ni hili. Mahakamaya Juu na Mahakama ya Rufani sio miongoni mwa mambo yaMuungano. Pamoja na ukweli huu, ib.158(3) inaweka mamlaka yakutunga utaratibu na sababu za rufani mikononi mwa Washirikakwa mujibu wa katiba na sheria zao. Matokeo yake ni kwambaWashirika wanaweza, wakitaka, kuamua mashauri yapi yaendekatika Mahakama ya Rufani ya Jamhuri na yapi yazuiliwe.Kwa mfano, Katiba ya Zanzibar ya 1984 iliopo inazuia kesi zozotezinazohusika na tafsiri ya Katiba ya Zanzibar, na kesi za Kiislamuzilizoanzia katika Mahakama za Kadhi kusikilizwa na Mahakamaya Rufani, hii pamoja na kwamba Mahakama ya Rufani ni jambo laMuungano (nyongeza ya pili). Inawezekena kabisa kwamba baadaya Rasimu kuwa sheria, katiba za Washirika zikasema kwamba –– kesi zote za tafsiri za katiba zao;– kesi zote za uchaguzi pamoja na uchaguzi wa marais wao;– kesi zote za uhaini dhidi ya serikali zao;– kesi zote sinazohusu ukiukwaji wa haki za binadamu aumaadili na miko ya viongozi; n.k.hazitapelekwa katika Mahakama ya Rufani ya Jamhuri na badalayake zitasikilizwa na kuamuliwa mara ya mwisho na mahakama zaoza rufani au na jopo la majaji (ya idadi iliyotajwa) wa MahakamaKuu yao. Isitoshe, wanaweza kwenda mbali zaidi kwa kusemakwamba matokeo ya uchaguzi wa marais wao hayatapingwa katikamahakama yoyote ile. Wakifanya hivyo, na hakuna sababu yakisheria kwanini wasiweze, hadhi ya Mahakama za Jamhuri, pamojana kazi yao, itapungua.

Sasa niangaze taasisi nyeti ya Muungano, na hii sio nyingine,isipokuwa Benki Kuu.
E. Benki Kuu
Uchumi unaotegemea uuzaji na ununuaji wa bidhaa, fedha namzunguko wa sarafu na uhamishaji wa fedha unakuwa na nafasiya kipekee. Akiba inawekwa kupitia fedha; uwekezaji unahesabiwakwa fedha; rasilimali zinathaminiwa kwa fedha. Benki Kuu, angalaukinadharia, ni taasisi nyeti inayosimamia fedha katika sura zakembalimbali. Majukumu muhimu ya Benki Kuu ni kutoa na kusimamiasarafu na fedha na mzunguko na uhamishaji wake; kusimamiaujazi wa fedha (money supply) na amana (bank deposits) katikabenki zote pamoja na za kibiashara; kutunga na kusimamia sera yakifedha (monetary policy); kuratibu, kudhibiti na kuhakiki mabenkiya biashara na uwekezaji katika nchi; kudhibiti mfumuko wa bei,ikiwemo bei ya fedha za kigeni (foreign exchange rate); na hatimayeni benki ya serikali. Kwa muhtasari basi Benki Kuu ni mtunzaji,mlinzi, mwangalizi na msimamizi wa fedha za taifa pamoja na akibaya nchi, ikiwa akiba ya dhahabu au fedha za kigeni.Kwa maoni yangu, katika nchi na uchumi kama wetu, na ili kuepukamisukosuko ya fedha, hakuna budi Benki Kuu idhibiti na kuongozasoko, badala ya kufuata soko. Benki Kuu ikifuata soko bila kuwa namsimamo kwa mujibu wa sera ya fedha, na mtazamo wa maendeleowa nchi, basi litakuwa kama bendera inayopepea kwa kuelekezwana upepo badala ya kudhibiti mwelekeo wa upepo. Benki Kuuinatakiwa kuwa kinu kinachonasa upepo ili kujijengea nguvu, siobendera inayoyumbishwa na upepo.Kwa vyovyote vile, huwezi kuwa na Benki Kuu zaidi ya moja katikanchi moja hata kama ni nchi ya shirikisho. Je, Rasimu inasema ninikuhusu Benki Kuu?Kwanza, ‘Sarafu na Benki Kuu’ ni jambo la Muungano. Hii ni tofauti

na Katiba ilioko inayosema kwamba, ‘Mambo yote yanayohusikana sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti);mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote zamabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusikana fedha za kigeni’ ni jambo la Muungano (nyongeza ya kwanza,jambo la 12). Hii ni pana zaidi, inataja sio sarafu tu lakini mamboyote yanayohusika na fedha, ikiwemo, bila shaka, sera za kifedha.Pamoja na hayo inataja usimamizi wa fedha za kigeni.Pili, Rasimu katika ib. 218 inasema Washirika wanaweza wakawana benki zao zitakazokuwa na jukumu la ‘kutunza akaunti ya fedhaza serikali husika, kusimamia Sera za Kifedha na benki za biasharakatika mamlaka zao.’ Nitarejea kwenye hii hivi punde.Tatu, majukumu ya Benki Kuu yaliyotajwa katika Rasimu nimanne –‘(a) kutoa sarafu, kudhibiti na kusimamia mzunguko wa sarafu;(b) kuandaa na kusimamia Sera na Mipango inayohusiana nasarafu;(c) kudhibiti na kusimamia masuala ya fedha za kigeni; na(d) kusimamia Benki za Washirika wa Muungano.’Aya (a) na (b) haina shida kwa sababu zinahusika na sarafuambayo ni jambo la Muungano. Lakini aya (c) na (d) sio mambo yaMuungano. Kwa kuwa masharti ya Katiba ya Shirikisho, ambayohayahusiki na mambo ya Muungano, hayawabani Washirika,inawezekana kabisa Washirika wasitilie maanani aya hizi nawakafanya shughuli zao kupitia benki zao kama kwamba mashartihaya ya kusimamiwa na Benki Kuu, na fedha zao za kigenikudhibitiwa na Benki Kuu, yasingekuwepo.Nitahitimisha na kujumuisha hoja yangu juu ya Benki Kuu kamaifuatavyo:

Moja, Benki Kuu iliyotajwa katika Rasimu inakosa majukumumuhimu ya Benki Kuu za kawaida.Pili, benki za Washirika zina uhuru wa kutekeleza mamlaka yoteya benki kuu isipokuwa kutoa na kudhibiti mzunguko wa sarafu.Kwa hivyo, Benki Kuu ya Shirikisho ni Benki Kuu kwa jina tu.Ukweli ni kwamba inafanana zaidi na baraza la sarafu, yaani‘currency board’, kuliko Benki Kuu.
F. Mapato na Gharama za Muungano
Rasimu inataja vyanzo vinne vya mapato ya Muuungano (ib. 215).Vyanzo hivyo ni –‘(a) ushuru wa bidhaa;(b) maduhuli yatokanayo na taasisi za Muungano;(c) mchango kutoka kwa Washirika wa Muungano; na(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.’Aya (a) na (b) zimetajwa katika mambo ya Muungano. Ushuru
wa bidhaa una utata kidogo. Ninafikiri hii haimaanishi ushuru
wa bidhaa unaosimamiwa na idara ya forodha kwa maana ya
excise duty
. Kwa hivyo labda inamaanisha ushuru au kodi kama
value added tax
(VAT), sales taxproduce cess n.k. Kama hii ndioiliyokusudiwa inahitaji ufafanuzi zaidi. Kwa vyovyote vile, ushuruwa bidhaa unakusanywa mahali pa uzalishaji, uuzaji na ulaji. Kunamasuala mawili hapa. Moja, Serikali ya Muungano itahitaji vyombo
na maofisi katika sehemu mbalimbali za maeneo yote mawili ya
Muungano kuweza kukusanya ushuru. Hii yenyewe inaweza ikawana gharama kubwa. Pili, ili kuziba nakisi katika bajeti yake, Serikaliya Muungano itajikuta kila mara inaongeza ushuru huu, jamboambalo litawaongezea wananchi mzigo. Pamoja na kulipa ushuruhuu wananchi watakuwa wanalipa kodi na malipo mengine kwaserikali zao.

Inaelekea ushuru wa bidhaa ndio utakuwa chanzo kikuu chamapato ya Serikali ya Muungano. Maduhuli inamaanisha karona malipo yanayolipwa serikalini kwa huduma mbalimbali (k.m.pasipoti, hati ya uraia, visa, n.k.). Kuna idara moja tu katika mamboya Muungano ambayo inaweza kutoa mapato haya, nayo ni ‘uraiana uhamiaji’. Kuna usajili wa vyama vya siasa pia lakini hii inawalakin nitaozungumzia baadae.Ninahisi kwamba mapato makubwa ya Muungano yatatokana namchango wa Washirika. Ni wazi kwamba Bara ndio itachangiaasilimia kubwa sana. Inanishangaza kwamba Rasimu haitajikabisa uwiano wa mchango kutoka kwa Washirika. Jambo hili ni laawali kabisa kuandikwa katika rasimu yoyote ya Shirikisho.Hili la mkopo kutoka nje na ndani sina hakika nalo. Serikali ambayohaina chanzo chake huru cha mapato au sekta ya uzalishaji auwalipa kodi wakubwa, hususan mashirika, chini yake, itakuwa nahali ngumu ya kupata mikopo.Kwa jumla, kuna utatanishi na wasiwasi kwa upande wa mapatoya Muungano. Kwa upande wa gharama, ni wazi kwambakuendesha serikali ya muungano kutakuwa na gharama kubwa.Kazi inayofanywa na taasisi moja au idara moja katika muundouliopo sasa itahitaji taasisi mbili. Kwa mfano, badala ya kuwa naTume moja ya uchaguzi, sasa kutakuwa na tume mbili, moja yaMuungano na nyingine ya Bara. (Ukiongeza ya Zanzibar kutakuwana Tume tatu za uchaguzi.) Na hivyo hivyo kuhusu tume nyingine.Ukiangalia juujuu tu, licha ya taasisi na idara za kawaida katikaserikali, kuna tume karibu nane na mabaraza mawili yenyewajumbe wazito ambao bila shaka watakuwa na mishaharaminono na marupurupu poa. Wananchi wamekwishaanzakuonyesha wasiwasi wao kwa kuwaongezea mzigo wa kubebaserikali kamili nyingine, zaidi ya hizi mbili tulizonazo.

G. Mambo ya Muungano
Kama tulivyoona, kuna mambo saba katika mambo ya Muungano.Sina mengi ya kusema zaidi ya yale niliyoyasema kwamba polisi,Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani na mambo yote yahusuyofedha na fedha za kigeni yangefaa kuwa mambo ya Muungano.Kuna jambo moja la Muungano ambalo mimi binafsi sioni mantikiya kuwa kwenye orodha hii - ‘Usajili wa Vyama vya Siasa’. Ukiwaumeshaweka muundo wa serikali tatu, jambo linalofuata ni juuya chama cha siasa chenyewe kama kinataka kugombea uchaguzikatika eneo moja tu na sio lingine. Kwa hivyo, unaweza ukawa nachama cha siasa ambacho kinagombea uchaguzi katika Zanzibartu, au Bara tu, au katika ngazi ya Muungano tu.
H. Michakato ya Katiba na Mengineyo
Kabla sijaenda kwenye sehemu yangu ya mwisho na kuhitimishaningependa kutahadharisha kuhusu michakato ya katiba zawashirika. Siku moja baada ya kuzinduliwa kwa Rasimu tulianzakuwasikia viongozi wachache, na hata wahariri wa magazeti,wakitoa maoni yao juu ya katiba ya Tanganyika. Wengine walidirikikusema wala hakuna haja ya kusuburi kupitishwa kwa Rasimu,maandalizi yaanze mara moja. Wachache, wakiwemo viongoziwaandamizi, walinukuliwa wakisema wala hakuna haja ya kupatamaoni ya Watanganyika kwa sababu maoni yamekwishatolewakwa Tume ya Mzee Warioba. Na wakaongeza kwamba wajumbe waTume ya Warioba kutoka Tanganyika wanaweza kugeuzwa kuwaTume ya Katiba ya Tanganyika. (Nisingeshangaa kama mwingineangesema wala hakuna haja ya kuwa na Bunge la Katiba, Wabungekutoka Bara katika Bunge lililopo wanaweza wakajigeuza kuwaBunge la Katiba.) Kiongozi mmoja wa serikali, kutokana nabusara na uzoefu wake, amekaririwa akasema kwamba mchakatowenyewe hautachukua muda. Kwamba ukianza mara baadaya uzinduzi wa Katiba ya Muungano mwezi wa Aprili unaweza ukamalizika Desemba 2014 na 2015 tukawa na uchaguzi waBunge na Rais wa Tanganyika pamoja na uchaguzi wa Bunge laMuungano na Rais wa Muungano. Mimi binafsi nilibaki kuduwaakuona jinsi tulivyomeza mwendo wa
fastafasta!Kwanza, sio sahihi hata kidogo kuzumguzia jambo ambalo hatunauhakika nalo hata kidogo. Kwa nini tuwachukulie wananchi wetu nikama mbumbumbu ambao watakubali chochote wanachoambiwapamoja na rasimu hii? Mabaraza hayajaijadili; wananchi wenyewehawajaijadili ingawa wameanza kutoa maoni yao, pamoja nahisia zao za hofu na wasiwasi. Rasimu ya pili haijatoka; hatujuimarekebisho yatakayofanyika. Bunge la Katiba halijaketi. Hatujuikwamba litapitisha rasimu hii bila mabadiliko, tena makubwa.Kura za maoni bado.Pili, nani ameamua kwamba mchakato wa kupata katiba yaTanganyika, ikiwa muundo wa serikali tatu utapita, utafananana ule wa katiba ya Muungano? Mchakato wa kupata katiba yaTanganyika unaweza ukawa tofauti kabisa; unaweza ukawa borazaidi na wa demokrasia pana zaidi. Inawezakana kabisa kwambamchakato wa katiba mpya ya Tanganyika usianze na tume bali namkutano wa kitaifa wa kujenga mwafaka.Tatu, sio sahihi kisiasa au kimantiki, kusema kwamba wananchiwamekwishatoa maoni yao, kwa hivyo hakuna haja ya kurudi kwao.Walipotembelewa na Tume ya Warioba maoni waliyokuwa wakitoani juu ya katiba ya Muungano, sio ya Tanganyika wala Zanzibar.Mfano uliokuwa mbele yao ulikuwa wa katiba ya Muungano, siowa Tanganyika. Labda zaidi ya asilimia 95 wala hawajui kwambatuliwahi kuwa na Katiba ya Tanganyika. Ni kweli kabisa, maoniyaliyotolewa mbele ya Jaji Warioba yalikuwa ni manunguniko namatakwa yao. Sasa Tume inasema haiwezi kushughulikia mambomengi ya msingi, kama vile rasilimali na madaraka ya umma, kwahoja kwamba katika muundo waliopendekeza mambo haya ni ya
Washirika na sio ya Jamhuri ya Muungano. Je, nani anajua kwambawananchi wameridhika na hoja hiyo? Je wananchi wakisemakwamba Rasimu irejeshwe kwenye Tume ili Tume ifanye kazi yaziada kuutafuta muundo ambao utashughulikia kikatiba mamboyao ya msingi?Ukweli ni kwamba, kuna mengi hatujui wala hatuwezi kutabiri,kiasi kwamba kuanza mjadala wa mchakato mwingine wakati huo
uliopo wenyewe haujafikia tamati, ni sawa na kupiga ramli. Na, nne,
kuna hatari katika kufanya hivyo. Ni sawa na kuwapotoshea lengowananchi kwa kuanza mjadala mwingine kabisa na kuwafanyawaache kujadili hili ambalo liko mbele yao. Sina haja ya kuongezazaidi juu ya suala ambalo ni wazi.Kabla sijahitimisha nigusie, angalau kwa muhtasari, matumaini yawananchi ya Tanzania Mpya.
IV.

MATUMAINI YA TANZANIA MPYA
Tulipoanza mchakato wa katiba mpya, wengi wetu, pamoja nawananchi wa hali ya chini, tulikuwa na matumaini kwambatutajadili na kujiwekea hatma mpya ya nchi yetu yenye matumainina mwelekeo unaojali walio wengi, hususan wavujajasho. Maonimengi yametolewa na wananchi, mengi yakiwa manunguniko,matatizo na hali ngumu ya maisha kwa jumla. Ilikuwa ni juu yawajumbe wa Tume, kwa busara zao, na utaalam wao, kufanyauchambuzi, kuyaainisha maoni na kutafsiri matakwa ya wananchikatika lugha na dhana ya katiba.Haraka haraka tunaweza kusema kwamba maoni mengi yawananchi yalijikita kwenye maeneo matatu ya msingi yanayogusamaisha yao kwa karibu. Moja, ni demokrasia kwa maana yamadaraka ya umma - demokrasia itakayowawezesha wananchi
36
vijijini na mitaani kuweza kujiamulia mambo yao wenyewe. Pili, niudhibiti, usimamizi na uangalizi wa rasilimali na maliasili za taifaili utajiri huo uweze kuwanufaisha wananchi na vizazi vijavyo.Tatu, ni mpango, mazingira na taratibu zitakazotoa kipaumbelekwa huduma za lazima na bora kwa wananchi waliowengi,
kama elimu, afya, maji safi, makazi bora, hifadhi ya uzeeni, na
ajira stahiki kwa vijana. Kwa jumla, ilitegemewa kwamba Tumeingependekeza mfumo na muundo wa siasa, utawala, uchumi, namazingira utakaokidhi matakwa haya.Kwa mfano, madaraka ya umma, kwa maana ya mfumo wa serikaliza mitaa kuanzia ngazi za chini kabisa kama kijiji, shehia, mtaana kuendelea, hayajawekewa masharti ya kikatiba. Rasimuhaikuzungumzia kabisa serikali za mitaa, isipokuwa ibarandogo moja ambayo inasisitiza kwamba serikali za Washirika‘zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kugatuamadaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa’ kwa mujibuwa Katiba za Washirika. Hili halina uzito wa maana kwa sababuinawaachia Washirika mambo muhimu ya kuainisha mfumowa demokrasia. Hoja ya Tume ni kwamba jambo hilo, pamojana lile la rasilimali na huduma za elimu, afya n.k. sio mambo yaMuungano na ni juu ya Washirika kuyashughulikia katika katibazao jinsi wanavyoona inafaa. Ni vigumu kuikubali hoja hii kwasababu Katiba ya Shirikisho, inatakiwa, kama katiba mama,kuweka misingi ya mfumo na miundo ya mambo haya ya msingi.Kitakachofanyika na katiba za Washirika ni kufafanua, kwa mujibuwa hali yao halisi, bila kuivunja misingi iliyowekwa na katiba yaShirikisho. Haieleweki kwa nini, kwa mfano, haki za binadamuzimewekwa kwa ufasaha mkubwa katika Rasimu wakati haki zabinadamu sio jambo la Muungano. Kwa nini, kwa mfano, tunu,malengo n.k. yame rudiwarudiwa katika rasimu wakati hizizinaweza zisitiliwe mkazo katika Katiba za Washirika? Na papohapo hoja inatolewa kwamba madaraka ya umma na usimamizi
37
wa rasilimali sio jambo la Muungano na kwa hivyo hayakuguswana rasimu. Hoja hii, kwa heshima, haina mshiko.Inaelekea tulitarajia mlima, tukapewa kichuguu. Hata hivyo, labdahatujapoteza yote. Hii ni rasimu ya kwanza, bado kuna nafasiilimradi tuhakikishe kwamba mijadala juu ya rasimu haiharakishwina inakuwa huru bila kuingiliwa, na wananchi kutishwatishwa.Wananchi waielewe vizuri rasimu na maana yake halisi kwa undaniili waweze kuijadili na kuitafakari kikamilifu na kwa kina.

HITIMISHO
Katika kuhitimisha mhadhara wangu nitarejea kwenye udhaniau hypothesis yangu. Nilisema kwamba ninavyodhani mimi,masharti mengi ya Rasimu yalikuwa maamuzi ya maelewano kwamaana ya compromise na sio mwafaka kwa maana ya consensus.Baada ya uchambuzi wangu, ninadiriki kusema kwamba muundowenyewe wa serikali tatu uliopendekezwa ni compromise kati yawale waliosimamia serikali mbili na wale waliopigania muunganowa mkataba, kwa maneno sahihi, kuuvunja muungano. Wanaserikalimbili waliona afadhali kuwa na Muungano, hata kama niwa serikali tatu, badala ya kuuachia uvunjike; wakajifariji kwamatumaini ya dhamira ya wananchi na nia ya viongozi.Wana-mkataba wakaona kuwa kwa wakati huu wakubali serikali
tatu wakijua fika kwamba muundo wa serikali tatu hautadumu na
vyovyote vile utavunjika.Nilisema pia kwamba compromise inazaa uamuzi legelege.Compromise juu ya muundo, kwa maoni yangu, imezaa muundowa muungano legelege. Kuna maeneo mengi nimechambuana kudhihirisha kwamba yatazaa migogoro ambayo hatimayeinaweza kuuvunja Muungano. Kero za Muungano zitaendelea,safari hii kutoka pande zote mbili.

Muungano ukivunjika hakuna mwananchi atakayenusurika,awe wa Tanganyika au wa Zanzibar. Tuna mifano mingi ya hivikaribuni. Shirikisho la Sovieti liliposambaratika, likazaa migogorona vita vya wenyewe kwa wenyewe – mgogoro wa mpaka kati yaUzbekistan na Krygistan; mgogoro kuhusu maji kati ya Uzbekistanna Tajikistan; vita vya Chechnya visivyoisha; vita kati ya Azerbaijanna Armenia, n.k. Waliofaidika ni mashirika ya kibeberu ambayowalitua kama tai kupora rasilimali za Urusi.Shirikisho la Yugoslavia lilipogawanyika likazaa vita katika eneolile kiasi kwamba mpaka leo halijatulia. Wanasiasa wenye uchuwa madaraka wakisukumwa na nchi za Magharibi, wakatumiauhasama wa jadi kati ya makabila na dini kushawishi mgawanyiko.Makabila na dini zilizofanya kazi kwa pamoja, kwa kiasi fulani, chiniya uongozi wa Rais Tito, na mfumo wa Shirikisho, yakagawanyika.Leo hii nchi ambayo ilikuwa na amani kwa zaidi ya miongo mitatuimegawanyika katika nchi kama saba (Croatia, Serbia, Bosnia,Macedonia, Montenigro, Kosovo na Slovenia). Na vita badovinaendelea. Waliofaidika ni nchi za Magharibi kupitia NATO yao.Mwandishi mmoja anaweka wazi maslahi ya nchi za Magharibikatika kusambaratisha Yugoslavia. Nimnukuu kwa sababu mfanohuu una mengi ya kutufundisha:Beginning in 1990 Germany and the United Statessought and achieved the breakup of Yugoslaviain two stages—1992-1995 and 1998-1999. TheGerman government aimed at this division becauseit wanted to include as territory of its “vital interest”Slovenia and Croatia, the most economicallydeveloped states of the Yugoslavian confederation. …Through them Germany would achieve access to theAdriatic Sea.

The United States was interested in the more recentlyestablished states (Bosnia, Serbia, the former SocialistRepublic of Macedonia), which controlled the onlyroute from east to west and from north to south throughthe Balkan mountains. The Balkan area, along withRomania, Bulgaria, Turkey and the Arab nations, formsa European-Middle East bloc, which the United Stateswants to control (including the former states of theSoviet Union—Kazakhstan, Azerbaijan, Turkmenistan,Tajikistan) for the complete exploitation of the great oilresources of the Caspian Sea.

Na hapa, karibu na nyumbani, Sudan ya Kusini ilipojitengakumekuwa na migogoro juu ya mafuta, ambayo bado inaendelea.Nimewahi kusema na ninarudia. Suala la Muungano sio letu tu.Kuna nchi za kibeberu zina maslahi makubwa ya rasilimali pamojana ya kijeshi katika eneo letu, hasa Bahari ya Hindi. Tukibezamambo haya nyeti kwa sababu tu ya uchu wa madaraka ya viongoziwachache, tutawapeleka watu wetu kwenye hali mbaya.
***
Tume imesema, ingawa hatujaiona taarifa yao rasmi bado, kwambawananchi wengi walitaka serikali tatu. Lakini, kwa heshima,ningependa kuhoji msimamo huu. Jukumu la Tume halikuwa tukukusanya maoni na kuhesabu nani amesema nini. Jukumu laTume lilikuwa ni kupokea maoni, kuyaainisha na kuyachambuaili kupata kiini chake na sababu zake. Wajumbe walipoambiwa nawananchi wa eneo moja kwamba wajengewe india ndogondogo,haikumaanishwa hivyo, bali wananchi walikuwa wanadai hospitali;kwa kuwa viongozi wanapelekwa India kupata huduma za kiafya,basi wao pia wakataka wajengewe hospitali bora katika maneneoyao na wote, viongozi na wananchi, watibiwe humohumo nchini.

Hatimaye, ukiangalia kwa undani kero za Muungano, kwamfano, suala lenyewe sio idadi ya serikali bali ni la demokrasia.Wazanzibari kwa muda mrefu tu wamedai haki yao ya kujiamuliamambo yao wenyewe; kushirikishwa katika maamuzi muhimu;kutokudhalilishwa, na kupewa heshima ya mshirika huru. Madaihaya ni halali. Hoja yangu kwa muda mrefu ni kwamba tusiangaliesuala la Muungano kwa jicho la idadi ya serikali bali kwa mtazamowa demokrasia. Na tukifanya hivyo tunaweza kubuni muundowa kipekee kutokana na historia yetu na hali halisi ya Washirikakutokuwa na uwiano wa uchumi, eneo au idadi ya watu.Muundo wa serikali tatu, au shirikisho kama unaoainishwa,unajikita kwenye usawa wa kisiasa (political equality). Kwa msingihuu, uwakilishi, hususan katika vyombo vya kuchaguliwa, haunabudi uwe sawa bila kujali idadi ya watu. Lakini katika hali yetuya uchumi, mchango wa Washirika katika gharama za shirikishohauwezi ukawa sawa, wala sio haki, kwa sababu hatuna usawa wakiuchumi. Kwa vyovyote vile, Tanzania Bara itachangia asilimiakubwa ya gharama za Shirikisho. Hatimaye, anayelipa mpigazumari ndiye anayechagua wimbo.Kwa maoni yangu, kama tungekuwa na mtazamo wa kidemokrasiatungeweza kubuni muundo ambao unakidhi matakwa ya pandezote mbili bila hatari ya kuuvunja Muungano. Mimi binafsinimewahi kutoa pendekezo la muundo mbadala. Mara ya kwanzaniliwasilisha pendekezo langu kwa Baraza la Wawakilishi kamamiezi michache iliyopita. Kwa muhtasari, nilipendekeza dolakamili mbili, la Zanzibar na la Muungano. Bunge la Muunganolitakuwa na mabaraza mawili, Baraza la Wananchi na Baraza laNchi. Wajumbe wa Baraza la Wananchi watachaguliwa mojakwa moja na wananchi wa pande zote mbili kutoka majimboni.Baraza la Nchi litakuwa dogo lenye, tuseme kama wajumbe 30,15 kutoka Bara na 15 kutoka Zanzibar wakichaguliwa na Bunge
 la Zanzibar na wabunge kutoka Bara katika Baraza la Wananchiilimradi wasiwe wajumbe wa bunge lolote lile. Na nilipendekezaorodha tatu – moja ya mambo ya muungano, nyingine ya mamboya kushirikiana (concurrent matters) na orodha ya tatu ni juuya mambo ya pamoja (joint interest). Kutokana na muda siwezikufafanua; nia yangu ni kudhihirisha kwamba muundo mbadalaunawezekana.Rasimu imezinduliwa. Imeanza kujadiliwa. Tuchukue nafasi hiikuijadili kwa makini ili hatimaye malengo na matumaini ya waliowengi yatimizike.
Makamu Mkuu wa Chuo, wanakigoda wenzangu, rafiki zangu na

wageni waalikwa. Mhadhara huu ulikuwa ni mchango wangu wamwisho katika wadhifa wangu wa Nyagoda wa Mwalimu Nyererelakini, nikiwa na uzima wa afya, hautakuwa mchango wangu wamwisho katika mijadala ya kitaifa.Nawashukuru sana kwa kunisikiliza. Ahsanteni na kila la heri.

2 comments:

  1. Sisi kutoa dhamana ya mkopo kwa watu wote kwenye% 3, mtu yeyote nia wanapaswa kuwasiliana nasi kupitia : victorialoancompany01@gmail.com na chini ya maelezo:

    Majina ...
    Kiasi ( $) ...
    Nchi ....
    Hali .....
    Mji .......
    Tel ...
    Muda ...
    Ngono .........
    Je kutumika kabla ..........

    Kumbuka: Hakikisha kutuma jibu yako ya barua pepe:
    victorialoancompany01@gmail.com

    ReplyDelete
  2. Habari am Bi, kiutamaduni na Tumaini, Taasisi mkopo halali na za kuaminika na mikopo
    katika sheria na masharti wazi na ya kueleweka kwa 2% kiwango cha riba. kutoka
    USD $ 12,000 kwa $ 8,000,000, Euro na paundi tu. Mimi kutoa mikopo ya biashara,
    Mikopo binafsi, mikopo ya wanafunzi, gari mikopo na mikopo kwa kulipa bili. kama wewe
    haja mkopo una kufanya ni kwa ajili ya wewe kuwasiliana nami moja kwa moja
    Katika: (merithope6@gmail.com)
    God Bless You.
    dhati,
    Bibi: sifa Hope
    Barua pepe: (merithope6@gmail.com)

    Kumbuka: majibu yote upelekwe kwa: (merithope6@gmail.com)

    ReplyDelete