Kambi ya upinzani imeibua sakata la ufisadi wa shilingi Bilioni 133 kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) ikihoji mambo kadhaa ikiwamo kiasi cha fedha zilizorejeshwa hadi sasa.
Pia kambi hiyo inayoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imesema hadi kufikia Juni 30 mwaka juzi, akaunti hiyo ilikuwa na Shilingi bilioni 205.743, licha ya serikali kuagiza kuamuru iondolewe katika Benki Kuu (BoT).
Chadema ilihoji kuhusu sababu zinazoifanya Epa iendelee kuwa chini ya BoT, licha ya uamuzi wa wa serikali kutaka iondolewe.
Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde aliyesoma hotuba hiyo alielezea hofu ikiwa kiasi hicho cha fedha kwenye akaunti hiyo, zitakuwa salama pasipo kufanyiwa ufisadi kama ilivyotokea mwaka 2005.
Silinde alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka juzi, viongozi wakuu wa BoT walijinufaisha kwa mkopo unaofikia Shilingi bilioni 55.668, ikilinganishwa na Shilingi bilioni 38.965 zilizotumika mwaka 2011.
Alisema kutokana na mkopo huo, upinzani ulitaka kujua utaratibu unaotumika kuwakopesha wafanyakazi fedha za kununua nyumba na magari na ukokotoaji wa riba kwa viongozi hao wakuu wa BoT.
Alisema, ripoti ya ukaguzi wa hesabu za BoT kwa mwaka 2011/2012 inaonyesha kuwa benki hiyo ilipata hasara ya Sh. bilioni 52.431 ikilinganishwa na faida ya Sh. bilioni 727.793 ya mwaka 2011.
“Tunataka majibu ya kina kuhusiana na hasara hii, kwa ni haiwezekani taasisi nyeti kama hii ipate hasara na taifa lisipewe taarifa za kina kuhusiana na chanzo cha hasara,” alisema.

No comments:
Post a Comment