Monday, June 10, 2013

Hatma ya dhamana ya Lwakatare leo

Hatma kuhusu dhamana ya  Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, anayekabiliwa na shitaka la kupanga njama za kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Denis Msacky, itajulikana leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Mei 27, mwaka huu Mahakama ya Kisutu ilishindwa kuamua kuhusu dhamana ya Lwakatare na mwenzake, Ludovick Joseph, kutokana na Hakimu Aloyce Katemana ambaye anasikiliza kesi hiyo kukuwa na dharura. Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Sindi Fimbo ambaye alishindwa kutoa uamuzi na kuamua huiahirisha hadi leo.

Machi 8, mwaka huu, Lwakatare na mwenzake walipandishwa kizimbani mahakamani hapo na kusomewa mashitaka manne yakiwamo na shitaka ua ugaidi.

Hata hivyo, Mei 8, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimfutia Lwakatare mashtaka matatu ya ugaidi yaliyokuwa yanayomkabili na kubakiwa na shitaka moja la kula njama ua kumnywesha sumu Msacky,.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Lawlence Kaduri baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na mawakili wa Lwakatare na kusema kuwa Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP) hakuwa na uhalali wa kufuta kesi ya awali iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18, mwaka huu na muda mfupi kuirudisha mahakamani hapo kwa hakimu mwingine.

Licha ya Mawakili wa Lwakatare kuwasilisha maombi yao pia Mahakama Kuu iliitisha jalada la kesi hiyo kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kulipitia kabla ya kutolewa uamuzi.

Akisoma uamuzi huo wa Mahakama, Jaji Kaduri alisema mashtka yaliyofunguliwa Kisutu dhidi ya Lwakatare hayakuwa na uhalali wa kisheria na kuamua kuyatupilia mbali na kubakiza shitaka moja ambalo ni la kupanga njama za kumnywesha sumu Msacky.

Shitaka alilobaki nalo Lwakatare kwa sasa ni la jinai ambalo dhamana yake yake inaruhusiwa tofauti na yale matatu ya ugaidi ambayo hayana dhamana kisheria.

No comments:

Post a Comment