Wednesday, May 22, 2013

TEF yatetea hotuba ya kambi ya upinzani bungeni

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesema halioni kama kulikuwa na hali ya uchochezi kwenye hotuba iliyowasilishwa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Dodoma juzi, kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo.

Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Nevile Meena, alisema hotuba hiyo ilikuwa haina uchochezi kwani msemaji alikuwa amerejea kwenye matukio yaliyokuwa yametokea.

“Sielewi vipimo vya habari  za uchochezi ambavyo vinatumiwa na Bunge ili kubaini ukweli ulikuwa ndani yake, labda namna ya usomaji ama uwasilishaji ambao ulitumiwa na mwasilishaji wa hotuba hiyo”  alisema.

Alisema mwasilishaji alikuwa sahihi katika  hotuba hiyo, hususani kurejea katika matukio ambayo yalishatokea kama vile kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoani Iringa, Daus Mwangosi. 

Mengine ni kutekwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.

Alisema ripoti ya CPJ iliyotolewa mwaka huu na kuonyesha kuwa Tanzania ipo miongoni nchi 20 ikikamata nafasi ya juu katika nchi zinazotawaliwa na vitendo vya unyanyasaji wa waandishi wa habari.

1 comment:

  1. Alisema ripoti ya CPJ iliyotolewa mwaka huu INAONESHA kuwa Tanzania ipo miongoni MWA nchi 20 ikikamata nafasi ya juu katika nchi zinazotawaliwa na vitendo vya unyanyasaji wa waandishi wa habari.

    ReplyDelete