Thursday, May 23, 2013

Pareso awashauri wanasiasa


MBUNGE wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso (CHADEMA) ameitaka jamii pamoja na wanasiasa kuondokana na dhana potofu kuwa waandishi wa habari ni maadui wao.
Pareso alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akichangia katika hotuba iliyowasilishwa bungeni na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.
Alisema wapo watu wamejenga dhana kuwa waandishi wa habari ni maadui hususan kwa wanasiasa ama kada mbalimbali serikalini na kutokuwa na ushirikiano wa kutosha pindi waandishi wawapo katika kazi zao.
Aidha, alisema kitendo cha jamii pamoja na watumishi serikalini kutotoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kunasababisha jamii kukosa taarifa muhimu.
Alisema sheria ya magazeti iliyopo kwa sasa imepitwa na wakati, kwani imekuwapo tangu kuwapo kwa mfumo wa chama kimoja.
Hivyo aliomba muswada wa sheria ya vyombo vya habari upelekwe bungeni ili kuweka mazingira bora na mazuri kwa waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment