Sunday, May 12, 2013

Jaji Werema hawatendei Haki watanzania


WANANCHI wamekuwa na wasiwasi na hawaelewi kwa nini Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema alitaka baadhi ya mapendekezo ya taarifa kuhusu vigogo walioficha mabilioni ya fedha kwenye akaunti za nje ya nchi ikiwemo Uswisi yaondolewe.

Kitendo cha serikali kubadili maazimio takriban matano kati ya saba, ambacho pia kilizua ubishani mkali wa kutofikia muafaka baina ya mtoa hoja, wabunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema, ambaye alipendekeza mabadiliko hayo kimmewatia wasiwasi wananchi.

Hoja hiyo iliyoasisiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) iliyokuwa na maazimio saba ya kufanikisha fedha hizo zirejeshwa, hatimaye iliporwa na serikali na kuyabadili maazimio hayo.

Mapendekezo yaliyozua mvutano ni pamoja na pendekezo lililotaka serikali ishirikiane na Benki ya Dunia kupitia kitengo cha ‘Assets Recovery’, ambapo katika marekebisho, Werema alitaka lifutwe kwa madai linafanywa na vyombo vya uchunguzi vya ndani.

Pendekezo la pili ambalo lilipingwa na Werema ni kuhusu viongozi wa umma kuwa na akaunti katika benki za nje kwa madai kuwa suala hilo linahusu benki za nje, na ipo sheria ya fedha za kigeni inayoshughulikia.

Pendekezo la tatu ni kutangaza akaunti za watu wenye fedha nje ya nchi katika vyombo vya habari, ambapo Werema alisema kipengele hicho kiondolewe kwa sababu kinavunja usiri wa benki mbalimbali.

Pendekezo la nne ambalo linataka Watanzania waeleze wamezipataje fedha hizo pia alitaka liondolewe kwa sababu vipo vyombo vinavyohusika na uchunguzi kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kile cha Intelligence Union Unit.

Mbali na hayo, Werema alipendekeza suala la Meremeta lipelekwe kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa sababu linahitaji hoja mahususi na kwamba anakubaliana na Zitto kwamba serikali haiwezi kujivua nguo.Jtunahoji; Je kuna mangapi tumejiva nguo?

Mtanzania mwenzetu aliyesimama kidete bila hofu  kutokukubaliana mapendekezo hayo yafutwe, alikuwa  Zito aliyesema “Mimi sikubaliani na mapendekezo ya Mwanasheria Mkuu, mapendekezo haya anayotaka yafutwe ndiyo msingi wa hoja yenyewe, kuyafuta ni kuifuta hoja,” alisema Zito.

Si Zito tu lakini Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), alipinga msimamo wa Werema wa kutaka kufuta mapendekezo hayo kwa maelezo kuwa kufanya hivyo ni kutoitendea haki hoja hiyo ambapo akisema hoja kwetu maana yake ni Watanzania.

Hata hivyo, Mpina alimtaka Zitto pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe, kuanza kutekeleza mapendekezo ya hoja hiyo kwa kutaja majina ya watu walioficha fedha nje ya nchi.

Ingawa, ilionekana kuibuka hoja upande wa serikali kumtaka Zitto ayataje majina ya watu anaodai wametorosha fedha nje ya nchi kwa kile kilichoonekana kutaka kumfanya akubaliane na kile ambacho kinapendekezwa.

Kauli za kumtaka Zitto awataje kwa majina  watu hao ilizungumzwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, na Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia.

Baada ya mjadala huo mrefu huku hali ya kutoafikiana ikionekana kushindwa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alimtaka Zito pamoja na wabunge wengine wakubali vyombo viendeleze uchunguzi.

Ikiwa Waziri Mkuu alimuomba Zito awaunganishe na mchunguzi binafsi ambaye atawawezesha kukamilisha kazi hiyo na kisha matokeo yake kuyaleta katika mkutano wa 11, jambo la kuahirisha haki ni kuahirisha maisha ya watnzania.

Wananchi waliohojiwa kwa nyakati tofauti kuhusu Sakata hilo, wanalalamika kuwa, kwa lengo la Jaji Werema kutaka kufuta baadhi ya mapendekezo hayo, hawatendei Haki watanzania.

Wanadai hawatendewi kwa sababu yeye (Jaji Werema) siyo pekee anayeweza kuamua kukataa mapendekezo ya haki zao kama inavyofanywa kwa Uchaguzi wa Wajumbe wa Maoni ya Katiba.

Katika hoja hiyo, Mtanzania mwenzetu na Kiongozi mwenye uchungu na ki ya watanzania walalahoi Ztto, aliitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya Watanzania walioficha fedha haramu nje ya nchi, ambapo sh bilioni 312 zinadaiwa kufichwa nchini Uswisi, na haziwasaidii wasio na kitu nchini.

Ni rai yangu sasa, Watanzania tumuunge Mkono Zito na Mpina, tupige kelele kwa uwezo wetu wote kila mtu alipo kwa dini na dhehebu lake, kwa maombi na kilio, ili Mungu aingilie kati Shetani asiwatumie watanzania wenzetu miongoni mwetu, kuminya na kuficha haki hiyo.

No comments:

Post a Comment