Saturday, May 11, 2013

Chadema yamuonya wakala wa Pembejeo na Mbolea -Mlaguzi


CHAMA cha Demokrasia Wilayani Mvomero Kata ya Sungaji, Kimemuonya Wakala anayesambaza Pembejeo Kijiji cha Mlaguzi aliyejulikana kwa jina la Jafari Tweve, kwamba asithubutu kuchakachua Mbolea na Mbegu za wananchi wake, maana Kijiji hicho ni cha Madiliko ya Ukombozi wa M4c.
Kauli hiyo kwa pamoja imetolewa na aliyekuwa Mgombea wa Kata ya Sungaji Jairos Msigwa na kuungwa Mkono na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho Abasi Tika, wakidai kwamba, wanamtaka Wakala Tweve aache Ubabaishaji kwamba, asipotekeleza atakipata walichokipa viongozi kijiji hicho waliotimuliwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wananchi wa Mlaguzi kupata tuhuma kwamba, Wakala huyo amekuwa na Mawasiliano ya siri na baadhi ya Viongozi wa Kijiji na Kata ili kutengeneza udanganyifu, ambapo wametonywa Mtendaji wa Kijiji hicho Ibrahimu Mbalazi  ambaye hapatikana anashirikishwa.
“Tumeambiwa kuna Mbolea Mifuko Miwili (2) na Mahindi imeshushwa Barabarani na ipo kwa Mwigoe aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kigugu. Kutokana hali hiyo, tumegoma kupokea ppembejeo hizo, hivyo  Kiongozi yeyote atakayethubutu kuchakachua, hapatakalika”.alisema mwananchi aliyeomba asitajwe.
Mwandishi alimtafuta Wakala Tweve, ambaye baada ya mabishano ya kutambuana alikiri ameshusha Mbolea Minjingu Mifuko miwili (2), na Mahindi Kilo 75 si Mifuko 50 ya Mbolea au Mifuko (2) ya Mahindi kama ilivyoelezwa. Alimlalamikia Mtendaji ambaye hakumtaja Jina kuwa alichukua fedha haonekani.
“Kuna Mtendaji Kijana Mweupe Hivi, nilimpa Sh. 30,000/- za Stoo na 30,000/- za kupandisha pembejeo hizi Mlaguzi, lakini hadi leo namtafuta simpati”.alisema Wakala kwa kulalamika kuonesha amedhulumiwa, ikidaiwa fedha hizo ni Laki Tatu na si 60,000/- anavyodai Wakala.
Aidha Mwandishi alimtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mlaguzi Abasi Tika ambaye alikiri kupigiwa Simu na Mtu mwenye Namba 0655-425577 ambapo alimtaka wawasiliane ili wazungumze, jambo ambalo alisema, haoni sababu ya kuzungumza bali kinachotakiwa afikishe Mzigo Kijijini.
Wananchi wa Mlaguzi wamekuwa wakali na waelewa kudai haki yao, ambapo hivi karibuni waliwajia juu Mwenyeikiti na Kamati yake ya watu 25 na kuwapiga chini na kuchagua wa muda, na pia walimjia juu Diwani wao wa Kata ya Sungaji Athumani Mkimbu dhidi ya Matumizi mabaya ya Milioni 4.8/= za Zahanati Mradi ambao unadaiwa uko kwenye Lenta wakati upo kwenye Msingi.

No comments:

Post a Comment