Monday, May 27, 2013

Godbless Lema - MESEJI YA VITISHO ILITOKA KWA MKUU WA MKOA

Tarehe 21 /5/2013 Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) L iberatus Sabas ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliongea na waandishi wa habari juu ya shutuma zangu juu ya ujumbe wa maneno mfupi niliopokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Magessa Mulongo siku ya tarehe 25.04.2013 kutoka kwenye namba anayotumia mkuu wa Mkoa namba 0752960276 namba ambayo imesajiliwa kwa jina la Magessa Mulongo kwenda namba 0764150747 namba ambayo imesajiliwa kwa jina la Neema Lema namba ninayo tumia Mimi , ujumbe unaosema “ Umeruka kihunzi cha kwanza nitakuonyesha kuwa mimi ni Serikali , ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi “

Nimesikitishwa na kufedheheshwa sana na taarifa hii ambayo sasa inathibitisha bila mashaka kuwa Jeshi la Polisi Arusha hasa Mkuu wake anatumika na sina shaka kusema kuwa yeye ni KIPEPERUSHI cha Mkuu wa Mkoa , baada ya Mimi kupokea ujumbe huu tarehe 25/4/2013 nilitoa taarifa kwa vyombo vya habari na nia yangu ya kwenda mahakamani juu ya vitisho hivi .

Haya yafuatayo ni maswali ya msingi ninayojiuliza bila kupata majibu sawia kuhusu taarifa ya Jeshi la Polisi na Mtandao wa simu wa Vodacom .
1) Kwani nini Jeshi la Polisi walikataa kuchukua maelezo yangu Mimi juu ya tuhuma hizo nzito dhidi ya Mkuu wa Mkoa ambaye amenitumia meseji kupitia simu yake ya mkononi kama ninavyolalamika ? lakini pia ni muda takribani mwezi umepita tangu nimetoa malalamiko yangu je katika kipindi chote cha mwezi mzima Jeshi la Polisi waliona ni busara kwenda Kampuni ya Vodacom kutafuta mawasiliano yangu na Mkuu wa Mkoa bila hata kuchukuwa maelezo ya mlalamikaji ambaye pia kwa nafasi yake katika Jamii ni Mbunge ? 

Bonyeza Read More Kuendelea



2) Nilipokuwa rumande Msaidizi wa Mkuu wa Makosa ya Upelelezi Arusha alinifuata na kuniomba nimpe simu yangu, nilimwambia sina nimemwachia Mke wangu na walimtafuta Mke wangu na kumuomba hiyo simu na kumuhakikishia kuwa akiwapa simu wataniachia na kunifutia kesi na Mke wangu aliwajibu kuwa simu alidondosha kwenye gari ya Polisi ile ambayo walinichukua nayo usiku wa siku waliyonikamata , waliita ile gari wakatafuta hiyo simu na walipokosa walichukua pochi ya Mke wangu na kumwaga vitu vyote na kuanza kuitafuta simu na kumpekua , Je Polisi hapa walikuwa wamekusudia nini ? 

3) Kwa namna ya kawaida sana ya upelelezi baada ya Polisi na Vodacom kukuta simu ninayotumia imesajiliwa kwa jina lingine katika msingi wa kawaida wa utafiti Kama ambavyo naelewa au kufikiri vyema huyu mwenye Jina hili angetafutwa kwani meseji ilionekana imetoka kwa Magessa Mulongo na imekwenda kwa Neema Lema , lakini aliyekuwa analalamika ni Godbless Lema , je kama Polisi sio Kipeperushi cha Serikali walipata wapi ujasiri wakutoa maelezo waliyotoa wakati kwenye usajili wa mitandao ya simu namba 0764150747 imesajiliwa kwa jina la Neema Lema bila hata kuchukua nafasi ya kumtafuta Neema Lem a kujua ni nani huyo ambaye simu yake inatumiwa na Mtu mwingine ? na ni kwanini Polisi hawakusema kuwa mimi nimedanganya kwani namba hiyo sio yangu ni ya Neema Lema ?

4) Mimi kama mteja ni nayetumia namba 0764150747 nimehiifadhi namba ya Magesa Mulongo 0752960276 kama ( RC ARUSHA VODA) na ndio jina lililokuja na ujumbe wa vitisho katika simu ninayotumia . Vile vile katika barua ya Vodacom kuna maelelzo ambayo ni ya mashaka , kwamba namba ya simu ya Magesa Mulongo ilituma meseji kwenda namba 0764150747 yenye usajili wa jina la Neema Lema kuwa ni kweli kuwa meseji ilitumwa na namba ya Mulongo isipokuwa Center number sio ya Vodacom , swali , kama namba ya Mulongo ni ya Kampuni yao ndio iliyotuma meseji basi hata hiyo center number ni ya kwao kwani kama ingekuwa sio ya kwao Kampuni ya Vodacom isingeweza kuona taarifa zake katika mfumo wake wa mawasiliano na kuzitolea taarifa hivyo kama wameweza kuwa na taarifa zake maana yake ni kuwa mawasiliano hayo yamepita katika mitandao yao ndio maana Kampuni ya Vodacom imepata taarifa za mawasiliano haya na kuyathibitisha kwa Polisi bila hata Kampuni yenyewe kuchuka nafasi ya kumtafuta mlalamikaji na kujua nini kilichotokea kwenye simu yake , lakini vile vile mimi kama mteja sina wakati wa kukagua center number pindi napotumia simu yangu na sijawahi kufanya hivyo na wala sijawahi kuzingatia kwani sio wajibu muhimu katika matumizi ya simu yangu ya mkononi.

5) Wakati Polisi walipoita vyombo vya habari dhana muhimu hapa ilikuwa ni kutaka kumsafisha Mkuu wa Mkoa na ndio maana barua ya Vodacom kwenda Polisi iko kwenye mitandao ya kijamii jambo mabalo Polisi au Vodacom wasingepeswa kufanya hivyo kama kungekuwa hakuna malengo ya kisiasa katika taarifa hii lakini kitendo cha Polisi cha kutoa taarifa bila kuona meseji kutoka katika simu ninayotumia huu ni uhuni mwingine ambapo ni wa msingi kwa Jeshi la Polisi kwani taarifa zinaonyesha kuwa Polisi wote ambao wamekuwa watesaji na waonevu kwa Viongozi wa Upinzani wamekuwa wakipanda vyeo na kupata thamani kubwa machoni kwa Watawala dhalimu na mifano halisi ya wazi iko mingi.


6) Ni dhahiri kwamba zinatumika njia nyingi kumsafisha Mkuu wa Mkoa kwa masilahi ya Serikali . Katika kesi ya uzushi niliyofunguliwa na Polisi ujumbe huu wa meseji utatumika kama ushaidi na mahakama itaona na kufafanua ukweli halisi , hivyo wote wanoangaika wasubiri kwani hivi punde tutakutana mahakamani .



GODBLESS J LEMA ( MP)

26/5/2013

No comments:

Post a Comment