Friday, May 17, 2013

Chadema Mkamba yavuna Wanachama 15 toka CCM


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kijiji cha Mkamba-Kidatu; Kimevuna wanachama 15 kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa madai wamekasirishwa na Serikali yao ya Kijiji, kwa kuuza Kiwanja ch Kliniki kwa Milioni Saba, kwa mfanyabiashara mmoja.
 
Hayo yalijiri 12.5.2013 kijijini humo, yakitanguliwa na wananchi kumkataa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji chao, Ndenda Tidi na Halmashauri yake, ambapo tangu 10.3.2012 waligomea kufanya kazi za Maendeleo na Michango yoyote, hadi wasomewe mapato na matumizi ambayo hawajawahi kusomewa.
 
Akihutubia Mkutano huo Mwanachama na Mwanaharati wa Mabadiliko ya M4Cwa CHADEMA Methew Likwina alisema, kama wananchi wa Mkamba wasipobadilika na kukataa kutumiwa kama vyombo vya Tija kwa Mafisadi, wataendelea kuwa watumwa kwenye nchi yao, na baadaye wayauzwa wao.
 
“Ni aibu kwa Viongozi wa Serikali ya Kijiji hiki, kuwadanganya wananchi kuwa wamekopa Shilingi Laki 550,000/- kwa Mfanyabiashara mmoja ili zisaidie Maendeleo ya Kijiji na kuwalazimisha wachange fedha ili kulipa, wakati ni Uongo kumbe Uongozi wa Kijiji unadaiwa urejeshe fedha za Kiwanja hicho.
 
”Chadema tunazo taarifa za kubunguruka Diri ya Mauzo ya Kiwanja cha Kliniki alichouziwa Mfanyabiashara mmoja hapa Kijijini (Nyaraka tunazo), ambapo baada ya CHADEMA kupiga kelele, Mwenyewe anataka arudishiwe fedha Zake! Wananchi hawawezi kulipa deni, Lipeni ninyi”.alisema.
 
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Kijijini humo, Lugano Mwambalaswa, alikiri kuwapokea wabachama hao 15 waliorudisha Kadi zao na kupewa Kadi mpya za Chama chake, ambapo waliahidi kutoa Ushirikiano Mkubwa ili kuharakisha Mabadiliko nchini Kote yanafanyika
 
Diwani wa Kata ya Kidatu, Asajile Mwasumbi (CUF,) amekiri kuwepo kwa kosa la uuzaji wa Kiwanja hicho, ambacho anasema, tangu mwaka 1967 kiliashainidhwa kuwa pajengwa Kliniki, lakini Mwenyekiti Tidi (CCM) kwa uroho, aliuza na wananchi wamegomea kufanya kazi zote Maendeleo.
 
Aidha wananchi kwa upande wao, wamewatuhumu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hassan Masala, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero, Azimina Mbilinyi, kuwa ndio wanaokwamisha maendeleo yao kwa kuwakumbatia waovu.

No comments:

Post a Comment