Wednesday, May 22, 2013

CCM kwa sasa tunakubarika mahala ambapo chadema hawajafika tu.

Hali ya siasa hapa nchini mwetu kwa sasa imebadirika kabisa, napenda kukiri kwamba, CHADEMA kwenye hili la kufanya mageuzi ya siasa hapa nchini wameshiriki kwa kiasi kikubwa sana, na wameweza kufanikiwa. Mafanikio ambayo CHADEMA imepata mpaka hivi sasa sio tu uwezo wa kuisambaratisha CCM katika uchaguzi mkuu wa 2015, bali wamefanikiwa kuleta mageuzi ya kifikra kwa watanzania hasa wale wa vijijini ambao ndio walikuwa mtaji mkubwa kwa chama changu CCM katika kushinda kwake chaguzi kuu zote zilizo kwisha kufanyika.

Mpaka hivi sasa watanzania wengi wa huko vijijini wanajua wajibu wa serikali kwa raia na wana diriki kuhoji pale serikali inapofanya uzembe wa makusudi kabisa katika kutimiza wajibu wake, jambo ambalo kwa miaka ya huko nyuma lilikuwa nadra sana kukuta mwanakijiji akihoji serikali aidha kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na njia zinginezo.

Kila mahali nikikuta bendera ya CHADEMA basi panakuwa na vijana wenye kuhoji, wenye uchu na raslimali za nchi yao na bila kusahau hali ya kutokuwa na woga katika kudai haki na stahiki zao, hali hii inaipa joto la tumbo chama changu hasa katika kushawishi watu wa aina hii kuturudisha tena madarakani ifikapo mwaka 2014 kwenye chaguzi za serikali ya mtaa na uchaguzi mkuu ifikapo 2015. Je, ni hoja gani tuitumie CCM kushawishi vichwa vya aina hii kwani wanajua fika kwa miaka zaidi ya 35 CCM imekuwa madarakani na miaka zaidi ya 50 tangu uhuru huku hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya zaidi hata ya watanzania wa enzi za ukoloni.

Sehemu pekee hapa nchini ambazo chama changu kinatembea kifua mbele ni pale tu ambapo CHADEMA hawajafika, sidhani kama kwenye historia ya siasa za hapa nchini CCM ilishawahi kukabwa koo namna hii, CHADEMA wamekuwa wakibana kila mahali na hizo operesheni zao mara SANGARA mara M4C, na mbaya zaidi katika hali ya kustahajabisha, badala watendaji wa chama changu wawe wabunifu wa kutafuta mbinu mbadala ya kuwadhibiti CHADEMA, wameonyesha hali ya kuishiwa mawazo na kutumia mbinu za kubambikia watendaji wa CHADEMA kesi za kupika ili tu chama hicho kipate kashfa na kuchukiwa na watanzania, badala yake ndio kwanza tunazidi kuwatangaza tena kwa kutumia raslimali zetu wenyewe, uzuzu huu jama.

CCM, muasisi wako alishasema, nanukuu, “CCM si mama yangu” ni maneno aliyosema Mwalimu Nyerere baada ya kuchoshwa na viongozi wanaokwenda kinyume cha manifesto (sera) za chama hicho. Yeye ndiye aliyekuwa muasisi wa sera za TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sasa kwanini sisi wengine tulioikuta CCM imeshazaliwa, kukua na kukomaa tuendelee kung'ang'ania ilhali yale yote aliyokuwa akisema baba wa taifa na muasisi wa CCM yametimia? Hatuna budi kuchukua hatua dhidi ya chama chetu ili kunusuru nchi, kwani hata Prof. Baregu alisema, nanukuu, "ikipaswa nichague kati ya nchi yangu na chama changu, basi nitachagua nchi yangu."

Binafsi nadiriki kusema, nimechoshwa na CCM, najua wengi mmeshazoea kuona watu wenye majina wakihama ndio inakuwa inanoga zaidi, lakini siwafichi, ni bora chama kimpoteze mtu mmoja mwenye jina, kwani kinakuwa kimepoteza kura moja, kuliko kupoteza mamia ya wanachama tena kimya kimya bila hata ya kujua kama kimepotelewa na wanachama. CCM kwa sasa kinapotelewa na wanachama wengi kuliko idadi ya wanachama wapya wanao ingia CCM, haya nimekuwa nikishuhudia katika utendaji kazi wangu na ni vyema nikaweka wazi tu.

CCM, serikali uliyounda imethibitisha madhaifu makubwa kupita kiasi na nikianza kuyaelezea hapa sitamaliza, na kila kosa huwa lina adhabu yake, kwa kosa ili la kuunda serikali mbovu (serikali ya awamu ya 4) katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru, hakuna njia nyingine ya watanzania kutuadhibu zaidi ya kutupa kura ya "HAPANA." Watanzania wenzangu wote kupitia mtandao huu wa JF, tuanze kulieleza hili mapema kwani JK ameruhusu wanaotaka urais waanze kujitembeza kwa wananchi, sasa kabla ya kuchelewa na kuruhusu chama hiki kufurukuta, ni kutangaza kura ya "HAPANA" kwenda kwa CCM.

KWA WANA CCM WOTE HUMU JF, KAMA UMEPITIA MALEZI MAZURI NA YALIYO ZINGATIA TAMADUNI NA DESTURI ZETU ZA KITANZANIA, BASI NI IMANI YANGU UTAELEWA MANTIKI NZIMA YA KUFANYA MABADIRIKO NDANI YA TAIFA LETU, KWANI MTANZANIA ALIYE LELEWA KWENYE MILA,DESTURI NA TAMADUNI ZA KITANZANIA, HAWEZI KUWA NA TABIA WALIZO NAZO VIONGOZI WETU WA SERIKALI NA CCM WALIOPO SASA, CCM SIO ILE TULIYO IZOEA, KWA SASA NI CHAMA KINGINE KABISA ILA TU KINATUMIA JINA CCM, SASA SISI TULIO NA MAPENZI MEMA KWA TAIFA KULIKO CHAMA (RUDIA KAULI YA HAYATI BABA WA TAIFA), HATUWEZI KULISALITI TAIFA KWA KULIANGAMIZA MOJA KWA MOJA KWA MASLAHI YA MUDA MFUPI TUNAYO YAPATA NDANI YA CHAMA.

NAPENDA KUMALIZIA KWA KUZITAJA SIFA MBILI TU ZA VIONGOZI NDANI YA CCM, YA KWANZA NI TAMAA NA YA PILI NI UCHOYO.

No comments:

Post a Comment