Wanachama 10 wa chama cha Mapinduzi (CCM) wa kata ya Sungaji Kijiji cha Dunduma wilayani Mvomero, mwishoni mwa wiki wametimkia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai CCM kimepoteza mwelekeo na kukalia matusi badala ya kushghulikia kero za wananchi.
Kauli hiyo waliitoa katika mkutano wa Mabadiliko (M4C) uliofanywa na Katibu wa Diwani wa Gairo Dustani Mwenda, Diwani wa Mtibwa Luka Mwakmbwa na Katibu wa Mbunge wa Morogoro na Mwenyekiti Chadema Morogoro Suzan Kiwanga, Salum Mpanda, almaarufu Mchungaji.
Waliokabidhi Kadi na namba zao za CCM kwenye Mabano ni pamoja na Hassan Mganga (2700406), Abdalah Kingwange (0096655), Zaina Mgomba (3207629), Juma Mavugo (1459467), Hashim Ally (2640299) Salum Kasiga (3029759), Maneno Mussa (3752991), Bakari Yusuf (0120414 ), Bernard Kaila na (744831), na shabani Abadalah aliyechana Kadi yake kwa hasira kabla ya kuorodheshwa.
Chadema kupitia kwa Katibu Mwenezi wa Kata Amina Masimbo, aliwakabidhi Viongozi wa M4C Kadi za Chadema namba zake kwenye mabano. “Hassan Mganga (2088384), Abdalah Kingwange (2088383), Zaina Mgomba (2088382), Juma Mavugo (2088380), Hashim Ally (2088385) Salum Kasiga (2088378), Maneno Mussa (2088381), Bakari Yusuf (0114853), Bernard Kaila na (2088379), na Shabani Abadalah (2088376)”
Wanachama hao wapya walisema, wamechoshwa na Ubabaishaji wa Ahadi za CCM na Serikali yake zisizo na ukweli. Ambapo viongozi wake tangu wamechaguliwa, hawawatendei haki wananchi na kusiliza kero zao, wakitolea mfano wa Uchaguzi wa mabaraza ya katiba ambapo watu waliteuliwa kimya kimya.
Aidha katika Mkutano huo, Mpanda kwa niaba ya Kiwanga alisema, "Vijana tumekuwa waathirika
wakubwa wa mfumo wa CCM, ambacho kimekuwa kikitenga pesa nyingi za ufisadi za kununua uhuru wetu. Kuna uhusiano mkubwa kati ya dini na kauli za viongozi wa nchi.
wakubwa wa mfumo wa CCM, ambacho kimekuwa kikitenga pesa nyingi za ufisadi za kununua uhuru wetu. Kuna uhusiano mkubwa kati ya dini na kauli za viongozi wa nchi.
“Mitume wote walikuwa vijana na walipambana na mifumo ambayo wanadamu walishaizoea, Mtume Muhamad (S.A.W) alipambana kuondoa ibada ya vinyago pale Makka. Pia Yesu alipambana na Mafarisayo ambao waliishika Torati. Nchi yetu ilipata uhuru kupitia Chama TANU dhidi ya unyonyaji wa wakoloni, hivyo wananchi fahamuni ukomboz mutaupata kupitia CHADEMA dhidi ya CCM.
No comments:
Post a Comment