Friday, April 26, 2013

Wananchi Njombe wamkana Makinda

Katika hali ya kushangaza wakazi na wananchi wa Mkoa wa Njombe wamemkana Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madai kuwa hawakumtuma kutumikia chama bali kushughulikia kero na matatizo ya wananchi.

Hayo yalitokea katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani hapo katikati ya Jimbo la Njombe Kusini ambalo yeye ndiye Mbunge wake.

Mkutano huo ambao uliongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo( CHADEMA), Dr wilbrod Peter Slaa,Naibu katibu mkuu kutoka zanzibari pamoja na wabunge machachari kutoka katika chama hicho(Mh Joseph Mbilinyi-Mbeya mjini, Mhezekiel Wenje-Nyamagana pamoja na Mchungaji Peter MsigwaIringa mjini) ambao wote kwa pamoja walifukuzwa bungeni kwa madai kuwa wanaleta fujo bungeni.

Dr slaa aliwataka wananchi wamthibitishie kuwa Makinda hakwenda bungeni kuwatetea bali kukitumikia Chama Cha Mapinduzi hivyo wabunge wa Chadema waendelee na kasi hiyo hiyo ya kuisimamia na kuikosoa serikali, hapo ndipo umati wote uliohudhuria mkutano huo uliponyoosha mikono yote juu kwa ishara ya kuunga mkono hoja iliyotolea na kiongozi huyo.

Spika Anne Makinda anatuhumiwa kwa kuliongoza Bunge ki ubabe hivyo kuwanyima wapinzani haki yao ya msingi ya kuihoji serikali juu ya matuimizi mabaya ya mali ya umma 

No comments:

Post a Comment