Tuesday, April 23, 2013

Wabunge Chadema waahidi kushambulia kwa mikutano


Wabunge sita wa Chadema waliosimamishwa siku tano kuhudhuria vikao vya Bunge, leo wanaanza kushambulia kwa mikutano yao katika Jimbo la Iringa Mjini baada ya kumaliza Mwanza.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema baada ya kufanya mkutano wa leo katika eneo hilo kesho watatua Mbeya Mjini.
“Tunataka tumshtaki Spika na Naibu wake kwa wananchi kwa kitendo chao cha kutuonea sisi na kuwabeba wabunge wa CCM,”alisema Mbilinyi.
Alisema kwa kitendo kinachofanywa na kiti cha Spika ni cha kionevu hivyo wanakwenda kufanya mikutano hiyo ili wananchi waelewe kinachofanyika si kizuri.
“Alhamisi tutakuwa kwa Naibu Spika na Ijumaa tutakuwa Iramba Magharibi kwa Mwigulu Nchemba, kazi yetu ni moja kushughulika na hawa jamaa,”alisema
Wabunge hao wameamua kufanya hivyo kutokana na kuonyesha kukerwa na uamuzi wa Naibu Spika, Job Ndugai kuwafukuza bungeni na kuwataka wasihudhurie vikao kwa siku tano.
Mbali na Mbilinyi wabunge wengine ni pamoja na Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini), Highness Kiwia(Ilemela), Ezekiah Wenje(Nyamagana), Godbless Lema(Arusha Mjini) na Tundu Lissu(Singida Mashariki).
Wabunge hao walifukuzwa bungeni kwa kufanya vurugu ya kuwazuia polisi kumtoa nje Lissu baada ya Ndugai kuamuru hilo.““Tunataka tumshtaki Spika na Naibu wake kwa wananchi kwa kitendo chao cha kutuonea sisi na kuwabeba wabunge wa CCM,”alisema Mbilinyi.

No comments:

Post a Comment