Meya wa Halmashauri ya Musoma Alex Kasurura (Chadema), amemkaanga Naibu Spika na Mbunge wa Kongwa Job Ndugai akisema, pamoja na kujigamba kwenda nchi nyingi za Nje, bado ameshindwa kuwatafutia Soko la Mahindi na Mafuta ya Alizeti wananchi wake, bali alichoweza ni Ubabe wa kuwafukuza wabunge wanaowatetea hata wananchi wake.
Kasurura alisema hayo 26.4.2013 katika Mkutano wa mabadiliko (M4C,) uliofanyika kata ya Pandambili na Kijiji cha Hembahemba Kata ya Njoge, ikiwa ni hatua ya kupinga kitendo cha Spika Anne Makinda na Naibu Spika Ndugai, kuwafukuza wabunge watano wa Chadema wanaotetea Haki za wananchi, na kuwabeba Wabunge wanaotukana matusi bungeni.
Akiwahutubia maelfu ya wakazi hao, Kasurura alimkaanga Ndugai kwa wapiga kura wake akisema, Mbunge wenu anajigamba kwa safari anazofanya nje ya nchi, lakini safari hizo haziwasaidii chochote kwa sababu ameshindwa hata kuwatafutia Soko la Mafuta mazuri ya alizeti mliyonayo, badala yake mmekuwa mkihangaika kuweka barabani.
“Si Alizeti tu, pia ameshindwa kuwatafutia Soko la Mahindi wakazi wa Hembahemba na Kibaigwa, na amefikia kutowajali kiasi kwamba ametoa mwanya kwa Wakenya ambao wamekuwa wakija kununua Mahindi yenu kwa bei Ndogo na kwenda nayo kwao kuweka vifungashio vizuri na kuyauza Sudan na Somalia kwa bei kubwa.
“Nimeshangazwa pia kuona Shule za Kongwa zina hali Mbaya, hazina Madawati, Wanafunzi wanasomea Chini, Walimu wana Hali mbaya! Hawana Nyumba! Lakini nimesikitishwa zaidi wananchi wa hembahemba wamejenga Zahanati kwa nguvu zao bila msaada wa Halmashauri, lakini Serikali imeshindwa kupeleka Madawa! Je, Mbunge? hatuna!.walijibu.
Aliongeza kusema, Umoja wa Mataifa( UN), nao pia wanayanunua Mahindi hayo Kenya na kuyasafirisha kwenda kwenye nchi zenye shida ya Njaa ya Chakula, lakini wananchi wake mmetelekezwa mnakosa kitu cha kuwaongezea Uchumi ili muweza kumudu maisha magumu aliyodai yamesababishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha aliwataka wananchi hao kufanya mabadiliko dhati na kujiunga Chadema), ili waonje matunda ya Rasilimali yao na kutolea mfano wa Halmashauri zinazoongozwa na Chadema ikiwemo ya Musoma, ambapo alidai wao wanapokosa maji, Musoma ina Mradi wa Maji wa zaidi ya Bilioni 35/-, na kusema hivyo haiingii akilini Ndugai kuwafukuza wabunge wanaowatetea bungeni likiwemo jimbo lao.
No comments:
Post a Comment