Sunday, April 28, 2013

Mbowe asema mfumo wa kura “Waliosema Ndiyooo wameshinda” haufai Bungeni!

Akizungumzia suala la mashine za kura bungeni, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amesema utaratibu unaotumika sasa wa kura za ndiyo na hapana ni wa zamani na hautendi haki, kwani huegemea zaidi katika uamuzi wa Spika na si wabunge.

“Lakini Bunge letu lina vifaa vinavyoonesha namna ya kupiga kura na kuonekana kwenye meza ya Spika, tena yapo maelekezo yanayomwezesha mbunge husika jina lake lionekane au la, sasa sielewi kwa nini bado tunang’ang’ania mfumo wa ndiyo na hapana, hapa kuna mchezo mchafu,” alisisitiza.

Alisema mfumo huo ukitumika, utaongeza uhuru wa wabunge kupiga kura bila kujali itikadi za vyama na kutanguliza maendeleo ya wananchi, kwani kwa sasa mtindo wa kura za “ndiyo“ na “hapana” hufanya Wabunge wengine washindwe kutoa uamuzi sahihi kwa hofu ya kuitwa wasaliti.

Pamoja na hayo, Mbowe alisema kambi ya upinzani inaitaka Serikali iwasilishe utekelezaji wa maazimio kuhusu suala la Richmond, ripoti ya Jairo, maazimio ya kamati ndogo ya Maliasili na Utalii kuhusu usafirishaji wa twiga na wanyama wengine hai na suala la mabilioni ya fedha yaliyofichwa Uswisi.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumzana waandishi wa habari mjini Dodoma hapo jana.


No comments:

Post a Comment