Sunday, April 14, 2013

Mbowe Ampa Pole Katibu wa Baraza la Vijana Chadema kwa Kufiwa na Baba yake Mzazi

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe leo Jumapili  alikwenda kumpa pole Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), Deogratias Munishi kutokana na msiba baba yake mzazi, Mzee Ephraimu Sabinus Munishi. Kiongozi huyo alifika kuijulia hali familia ya marehemu eneo la Sinza Uzuri, Dar es Salaam, jana. Mazishi ya marehemu Munishi yanatarajiwa kufanyika Kilimashuku, Maili Sita, Moshi, Jumaane wiki ijayo.




No comments:

Post a Comment