Saturday, April 13, 2013

Leticia: Wanaume wanaopenda ngono waanzishiwe vituo vya mafunzo


Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (Chadema), ameitaka serikali kuanzisha kituo maalum cha kuwafundishia wanaume wanaopenda ngono ya dezo kutoka kwa walemavu wa viungo au akili.

Ushauri huo alitoa jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza na kusema: “Wanaume wengi nchini wanaowavizia walemavu, wanaweza kuwa na matatizo ya ubongo au hawajiamini na vilevile hawana uwezo wa kushawishi wanawake.

Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo aliitaka serikali ianzishe kituo cha kuwafundisha wanaume jinsi gani wataweza kuachana na ngono ya dezo."

Ushauri wake huo ulilifanya Bunge zima kulipuka kwa vicheko huku wengine wakiunga mkono swali hilo. Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, alisema awali katika mila na desturi kwa baadhi ya makabila walikuwa wanawafundisha baadhi ya vitu watoto wa kiume wanapoenda jando.

“Nataka kusema hivi kwa serikali kuanzisha kituo maalum kwa ajili ya kuwafundishia wanaume haiwezekani…na hili ni jambo binafsi na si kwamba wanakuwa na matatizo baadhi yao hawana matatizo kabisa ni watu wazima na wana akili zao ila tu wanatamaa za kimwili.

“Kwa kweli mimi kama mama ninahudhunishwa na vitendo vya wanaume kuchukua walemavu wa akili au viungo kwenye kufanya nao mapenzi…kwa kweli hili si jambo la busara,” alisema.
Awali katika swali lake la msingi, Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mikakati gani kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vya kinyama vinakoma.

Pia, alitaka kujua kama ipo tayari kufanya marekebisho ya Sheria ya Kujamiiana ili kuongeza adhabu kwa watuhumiwa. Waziri Kombani alisema: “Ni kweli wapo baadhi ya wanaume wanaowarubuni wasichana walemavu na wale wanao ombaomba mitaani.”
Alisema vitendo hivi ni kinyume na Sheria ya makosa ya kujamiiana yaani ‘The Sexual Offences Act, 1998 Act No.4/1998’.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment