Wednesday, April 3, 2013

Kamati Kuu CHADEMA kukutana leo


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa siku mbili kwenye kikao chake cha kawaida jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 3-4 Aprili, 2013.
Katika kikao hicho cha siku mbili, Kamati Kuu itajadili pamoja na mambo mengine, yatokanayo na kikao kilichopita, hali ya kisiasa nchini, pia itapokea taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika mwezi Februari mwaka huu, ikiwemo mpango wa uendeshaji chama kwa kanda.
Aidha, Kamati Kuu pia itajadili mpango kazi na bajeti ya Chama kwa mwaka 2013-2014

Imetolewa leo tarehe Aprili 2, 2013, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA



No comments:

Post a Comment