Tuesday, April 23, 2013

Homa ya udiwani Arusha yapanda

MNYUKANO mkali wa kisiasa, unatarajiwa kuibuka tena Juni, mwaka huu, kati ya CCM na CHADEMA, pale vyama hivyo hasimu vitakapokutana kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani Jimbo la Arusha Mjini. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza Juni 21, mwaka huu, kufanyika chaguzi za marudio kote nchini, ambapo Arusha kata nne zinatarajiwa kutimua vumbi.

Kufanyika kwa uchaguzi huo, kumekuja baada ya CHADEMA kuwatimua madiwani wake, baada ya kwenda kinyume na maelekezo ya Chama.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha, Efatha Nanyaro, pamoja na kuzungumzia maandalizi ya uchaguzi huo, aliituhumu NEC na Serikali kutoijumuisha Kata ya Sombetini.

Nanyaro ambaye ni Diwani wa Kata ya Levolosi, alisema kipindi ambacho NEC ilikuwa inasita kutangaza uchaguzi huo wao walikuwa wakiendelea na maandalizi.

“Tuna uhakika mkubwa wa kushinda kata zote na hili halina ubishi, mpaka sasa wagombea zaidi ya 55, wamejitokeza kuomba kwa kata zote.

“Hatuna uhaba wa rasilimali watu, tumekuwa tukitoa mafunzo ya uongozi kwa muda mrefu, hawa watu ni wasomi wenye nia ya kuitumikia nchi yao,” alisema Nanyaro.

Alizitaja kata zitakazoshiriki uchaguzi na idadi ya wagombea waliojitokeza kuwa ni Kata ya Kimandolu (15), Elerai (18), Kaloleni (10) na Kata ya Themi (12).

Alipoulizwa wingi wa wagombea hao, kama unaweza kuleta mvutano kwenye uteuzi wa jina moja, Nanyaro alisema suala hilo ni vigumu kutokea kwa sasa.

“Mfumo wetu wa kupata viongozi upo wazi kabisa, ni vugumu kuibua makundi, hatutarajii mgogoro na mapema tunatarajia kuanza mchakato wa mgombea kwa kila kata,” alisema Nanyaro.

Akizungumzia Kata ya Sombetini, ambayo diwani wake, Alfonsi Mawazo aliyekuwa CCM alihamia CHADEMA, alisema Serikali imesita kuijumuisha kata hiyo kutokana na kutambua kuwa ni ngome ya CHADEMA.

“Ile ni ngome ya CHADEMA, hata tusipofanya kampeni tutashinda na CCM, Serikali na NEC, wameogopa kwa sababu wanajua tukiichukua na Sombetini basi Halmashauri itaongozwa na CHADEMA.

“Kauli ya Mawazo hakuandika barua ya kujiuzulu haina mashiko, hata kama hakuandika barua, ana zaidi ya vikao vitatu hajahudhuria, hicho tu ni kigezo tosha cha kumfukuzisha udiwani,” alisema Nanyaro.

Katika uchaguzi wa hivi karibuni, CHADEMA kilifanikiwa kunyakua kata nyingine iliyokuwa ikiongozwa na CCM ya Daraja Mbili, baada ya diwani wake kufariki dunia mwaka jana.


Mtanzania

Bonyeza Read More Kuendelea


Wiki iliyopita nilileta taarifa ya CHADEMA kushinda ktk uchaguzi wa kijiji cha Gedamar, Gunyoda Mbulu. Leo naomba kuwaletea taarifa nyingine kuwa CHADEMA wameibuka kidedea ktk uchaguzi wa serikali ya kijiji cha Geterer (Kijiji nilichozaliwa mimi na kukulia), tarafa ya Haydom, Wilaya ya Mbulu uliofanyika 20 April 2013. Na matokeo yalikuwa kama yafuatavyo. 
Petro Aweda ( Chadema) 182. 
Samweil Erro ( CCM ) 170

Mgombea wa CHADEMA Petro Aweda alimshinda mgombea wa CCM Samwel Ero katika mazingira magumu sana kutokana na hujuma walizofanyiwa viongozi wetu. 

A) Vituo vya kupiga kura vilipunguzwa kutoka 4 hadi 1 kilichopo ktk ofisi ya kijiji, jirani na anakotokea mgombea wa CCM. Kwa mujibu wa Jiografia ya pale watu wanaotokea upande wa pili wa kijiji ( kwa mgombea wa CHADEMA) walihitaji karibu zaidi ya saa moja kufika hapo.

B) Rushwa ilikuwa wazi wazi. Makada maarufu wa CCM waliokuwa wamegeukia chadema walipewa mgawo wa kati ya 50,000 hadi 300,000, hata hivyo haikusaidia. Kuna dalili kwamba wengi walichukua pesa wakapigia kura CHADEMA
Nguvu nyingi iliwekwa hapa ili kuweka mazingira ya kisiasa ya kushinda uchaguzi mwingine wa kijiji cha Haydom ambako ni mjini na ni ngumu zaidi kwao na Kata ya Dongobesh ambayo nayo ni ngumu. 

Kampeni za ccm ziliongozwana mjumbe wa NEC Taifa anayewakilisha wilaya ya Mbulu Mr Fratei na viongozi wengine.

Hoja ya Ugaidi. 
CCM waliwatumia wapambe wao kueneza hoja kwamba CHADEMA wameshtakiwa kwa Ugaidi na mkurugenzi wao Lwakatare mpaka sasa yuko mahabusu hivyo, wasichaguliwe. Kitu cha kushangaza ni kwamba taarifa hizi walikuwa wanazisambaza kimkakati katika kampeni ya Nyumba kwa nyumba na si majukwaani. Baada ya viongozi wetu kuona hilo tukawapa majibu sahihi na wakazijibu hoja za CCM kuhusu ugaidi wa Lwakatare sawia. Matokeo yake tukawageuzia ccm hoja kwa kutumia taarifa zilizopo ktk magazeti kwamba, CCM wanawaonea chadema kwa kuwafungulia mashtaka ya uwongo kwa njia zile zile za nyumba kwa nyumba. Mwisho wa siku kura ikakata mzizi wa fitina, CCM wakaumbuka. 


Maswali ya kujiuliza. Kwa kuwa ni dhahiri kwamba CCM walihujumu uchaguzi kwa kupunguza vituo kutoka 4 hadi 1 na bado wakashindwa, Na

Kwa kuwa CCM ilipiganiwa na vigogo wake ktk ngazi ya wilaya wakiongozwa na Mjumbe wa NEC Fratei wakiwa na magari 5 wakasambaa kijiji kizima na bado wakashindwa, na

Kwa kuwa CCM waligawa Rushwa wazi wazi na iko dhahiri kwamba kuna wanaccm wamekula pesa na bado wakakipigia kuraCHADEMA kwa kukichoka chama chao, Na

Kwa kuwa hoja ya ugaidi wa kutengeneza dhidi ya Lwakatare imewageuka CCM badala ya kuwasaidia kama ilivyotokea Getarer, Mbulu (bila kusahau kuzomewa kwa Nape na Kinana Morogoro)

Hivyo basi, naomba kuhitimisha kwamba;
1) kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki 2015 CCM haina fursa ya kushinda.

PAUL AWEDA

No comments:

Post a Comment