Friday, March 15, 2013

Dk Slaa: Tuhuma za Lwakatare kuteka waandishi zimepikwa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amezungumzia video aliyorekodiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare na kusema ni ya kutungwa na vyombo vya dola.

Dk. Slaa pia amelituhumu Jeshi la Polisi kufanya mchezo mchafu kwa maslahi ya kisiasa.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho kufafanua suala la kushikiliwa kwa Lwakatare.

Dk. Slaa, alilalamikia jeshi la polisi kuwa limekuwa likitumika kisiasa huku akitoa mfano wa chama hicho kuwa kimekuwa kikitaarifu jeshi la polisi kuhusu mambo hayo lakini halijawahi kuchukua hatua.

Alisema jeshi la polisi halijawahi kuchukua hatua stahiki kwa suala la mauaji ya Daudi Mwangosi kumwajibisha Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa aliyesimamia na kufanikisha kifo cha mwandishi huyo wa habari, jeshi la polisi pia halikuchukua hatua za kumhoji Dk. Stephe Ulimboka baada ya kuteswa na mtu anayedaiwa kuwa ni Afisa wa usalama wa Taifa wa Ikulu, hali kadhalika hawezi kushangaa ikiwa jeshi la polisi halitaacha kumhoji Absalom Kibanda.

Amesema, jeshi la polisi limekuwa likitoa taarifa za kukichafua chama, akikumbushia suala la Mwangosi, alisema kuwa mara tu baada ya tukio la Mwangosi kuuawa, jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wake lilitoa taarifa kuwa alilipuliwa na kitu kilichorushwa kwake akikimbilia kujisalimisha kwa polisi akitoka kwa wafuasi wa Chadema, jambo ambalo lilikuwa sio kweli.

Hivyo alisema, Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Chama hicho kuhusishwa kwa sakata la sasa la mkanda wa video uliopo katika mtandao na Kibanda ni mwendelezo tu wa kukihujumu chama, unaoratibiwa na Usalama wa Taifa, huku ukitekelezwa na jeshi la polisi. 


Chanzo : Fikra Pevu

1 comment:

  1. Gazeti moja liliandika:aliyemteka ulimboka huyu hapa, likaambulia kufungwa eti uchochezi.mtu fulani kaweka video ya uongo na kweli na kusema aliyemteka kibanda huyu hapa,tumeona mizengwe inayoendelea.kimsingi mahakama iwe makini na suala hili.

    ReplyDelete