Umati Mkubwa wa watu umekusanyika kumsikiliza Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe mjini Kasulu. Katika Mkutano huo Zitto alijibu maswali mbalimbali aliyoulizwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
(A).Amini ninachokisema mkuu kwani mm sina kadi ya chama chochote, anasema yeye hatagombea ubunge na hajasema yeye ni lazima agombee urais lkn kama atapewa ridhaa yuko tayari kwani anajua anaweza na kama hatatumwa na Chama atamuunga mkono mgombea yeyote atakayegombea kupitia Chadema awe Slaa, Mbowe, Shibuda, Mnyika nk, nk,nk na akasema hata kama ni wewe.
(B).Zitoo anasema nasikia Nape amekuja hapa anasema eti Chadema wanamtenga Zitto mara eti Chadema na Ukanda anasema wapuuzeni hao ni wachonganishi,
anasema suala la Uchaga ni propanganda tu za CCM hatoki mtu chadema hapa na Chadema ni chama cha wote masuala hayo tupia kule, anahoji mbona hawasemi NCCR ni Chama cha Kigoma?
(C). Zitto anasema Kama Chadema ni chama cha Ukanda basi ni cha Wasukuma maana Shinyanga ndio ina wabunge wengi wa Chadema.
(D). Zitto anasema yeye hawezi kubishana na Kabour anasema yule sio level yake yeye level yake ni m/kiti wao Kikwete hana muda wa Kubishana na akina Nape.
Anasema anachokitaka 2015 CDM majimbo yote inabeba majimbo yote ya Uchaguzi. Anasema kamwe hawezi kuwasaliti watu wa Kigoma anaseama kama ana matatizo ya kisiasa atawaambia lkn kwa sasa hana tatizo lolote na anajivunia kuwa Chadema na daima hawezi kukihama chama hiki anajivunia ufanya kazi na Mbowe na anajivunia kufanya kazi na Slaa. Anashangaa kuona wabunge waliochaguliwa ili kuunganisha nguvu bungeni wanagombana wao kwa wao na mmoja wao anashadadia(Machali) mwenzake afukuzwe uanachama(kafulira) anasema huu ni uenda wazimu wa kisiasa.
(E). Sasa Zitto anaongelea suala la Mtwara, anasema wale ni wahanga wa maendeleo kama sisi wana Kigoma japokuwa wao walipata bahati ya kupata rais akawajengea kalami kadogo
anasema utajiri wa gesi ya Mtwara unawza kuiendesha Uingereza kwa miaka 100, Anasema hakuna chama kilichodhamilia kumkomboa Mtanzania kama Chadema, anasema Chadema inamtaka Kikwete aseme aliongea nini na kampuni ya Total alipoenda ufaransa maana kama rais anaenda kuonana na kampuni inayofanya utafiti wa mafuta lake Tanganyika itakuwaje wakiomba kibali? Si TPDC wataagizwa tu mpeni mkataba huyo?
Anamwagiza M/kiti wa Chadema wilaya kuwa siku Mtwara wakiandamana tena na sisi tuandamane kuwaunga mkono.
Anatoa mifano hapa anaseama uchumi wa Angola unashikiwa na watu 12 tu akiwemo Isabela bin nani sijui vile ambaye ni binti mfalme anasema kama tutaruhusu mafuta yaanze kusafirishwa kila eneo kwenda Dar chini ya CCM kuna mijitu ya CCM inataka kujinufaisha na hii miradi.
(F). Anasema wameanzisha M4C anaomba wananchi wajiandae na oparesheni hii ambapo yeye na Mh. Arfi wamepangwa kanda hii, anasema sasa hivi wanakusanya vifaa kama kadi,usafiri, tishet nk.muda wowote kitawaka na ansema haiwezekani CCM waendelee kutawala nchi baada ya 2015 na chama kinachoweza kukitoa CCM madarakani ni Cdm tu.
Anasema hamna mgogoro ndani ya chama chama chenu ni imara hakina udini wala ukanda anaseama natamka rasimi leo kuwa SINYANYASWI NDANI YA CHADEMA NIKO FITI NA HIKI NI CHAMA CHANGU. Na siku ikitokea nitakuja kuwaeleza, anamwambia DJ aweke Leka dutikite kwanza ili apumue.
Sasa ni maswali.
1. Mtaendaje madarakani bila kuungana?
Zitto anajibu= NCCR wenyewe wabunge wenu Machali na Kafulila muwaombe kwanza waungane maana wananikwamisha sana, chadema tuko wazi kwa yeyote anayetaka kushirikiana nasi, lkn kumbuka Cuf wameungana na CCM anachombeza.
2. Kwa nini mnatumia mafuta kuzalisha umeme wakati ni ghali?
Zitto anajibu= Ni sababu ya ufisadi wa watu wenu wa CCM na ufisadi uliojificha ndani ya viongozi suluhisho la umeme wa kudumu Kigoma ni Grid ya taifa na mradi wa Malagarasi, anasema Kigoma Tanesco wanatumia Bil 1 kuzalisha umeme lkn wanakusanya mil 130, tupeni CDm nchi hii nanyi hamtajuta.
4. Inasemekana huelewani na Slaa ni kweli?
Zitto anajibu = nadhani umekosea kuuliza swali ulidhani mimi ni Nape, anamwambia jamani haya mambo ya siasa muwe makini nayo propaganda hizi ni za CCM, namheshimu sana Slaa ni katibu wangu.
5. Inasemekana Chadema ni chama cha wachaga wewe unasemaje?
Zitto anajibu =
Anasema mgombea uraisi wa Chadema chama ambacho watu wanasema ni cha Wachaga Kigoma alipata kura 45% hlf kilimanjaro akapata 36% sasa hapa suala la uchaga na ukanda liko wapi?
Chanzo JF
No comments:
Post a Comment