Wednesday, February 13, 2013

Wasaliti CHADEMA wakimbilia CCM


ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana la CHADEMA Juliana Shonza pamoja na aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki mwaka 2010, Mtera Mwampamba, wamejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Shonsa ambaye hivi karibuni alitimuliwa ndani ya Umoja wa Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), alikabidhiwa kadi yake ya CCM na Mwenyekiti wa CCM, taifa, Rais Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Akizungumza mjimi hapa mbele ya Kikwete, Shonza alidai amefanya uamuzi huo kutokana na CHADEMA kukosa demokrasia.
Aliilalamikia CHADEMA kuwa imekithiri kwa ufisadi, lakini imekuwa mstari wa mbele kuzungumzia ufisadi wa CCM.
Aidha alisema ndani ya CHADEMA kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Kwa upande wake Mwampamba alisema amejiunga na chama hicho kwa hiari yake mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote.
Rais Kikwete ambaye ndiye aliyetoa kadi za CCM kwa vijana hao, aliwapongeza kwa kuamua kujiunga na chama hicho tawala.

No comments:

Post a Comment