Friday, February 22, 2013

Mbinu wanazotumia Shule binafsi ili Wanafunzi wafaulu

Hapa nitaelezea kwa kina mbinu wanazotumia shule nyingi za binafsi ambazo huwa zinafanya vizuri.

Binafsi nimesoma shule ya Feza Boys miaka kadhaa iliyopita na kwa sasa ni Engineer, ijapokuwa wazazi wangu walikuwa maskini sana, shule iligharamia kila kitu kuanzia Form One mpaka Form Six.

1) Wanafunzi kuwa na vitabu vya masomo yote kwa kila mwaka wa masomo.
shule inatoa vitabu kwa wanafunzi wote kila mtu na kitabu chake toka mtu akiwa form one.Pia wanapewa vitabu vyote kila mwaka yaani wakiwa form two, three na four. 

2) Wanafunzi kuwa na muda wa kujisomea kila siku.
Wakati nikiwa pale wanafunzi wote lazima kila siku wasome madarasani jioni baada ya mlo wa jioni. Kusoma wanaanza saa moja jioni mpaka saa nne usiku na kuna viongozi ambao wanakuwa wanasimamia wanafunzi kusoma na kuwasaidia pale wanaposhindwa kuelewa kitu wanachokisoma.

3) Mitihani ya kila wiki
Kila wiki kuna mtihani mmoja wa somo moja kwa kila darasa. Kwa mfano kama wiki hii mkifanya physics basi next week mnafanya english au somo lingine lolote. Wanafunzi wote wanaofanya vizuri kwa kila darasa uitwa mbele na wanaofanya vibaya pia. Mtu akiwa wa mwisho zaidi ya mara tatu basi mzazi wake uitwa na kupewa taarifa na wanajadili jinsi ya kumsaidia huyu mwanafunzi.

4) Wanafunzi kukatazwa kutumia simu
wanafunzi hawaruhusiwi kumiliki simu kipindi chote cha shule. Wanaruhusiwa kuwa nazo ila lazima waziweke kwa viongozi maalum wa maadili ya wanafunzi na wanazitumia pindi tu pale ambapo wanahitaji kuwasiliana na wazazi wao.

5) Wanafunzi kuwa na nidhamu kwa walimu na kati ya wanafunzi kwa wanafunzi
Wanafunzi wanafundishwa maadili mema kati yao wenyewe kwa wenyewe au kwa watu wengine. Kama mtu hana nidhamu shule inamfukuza ata kama baba yake akiwa na uwezo wa kifedha namna gani.

6) Mazingira mazuri ya shule
Shule kuwa na mazingira mazuri pia inachangia kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi. Mwanafunzi anapokuwa katika mazingira mazuri ata akili pia ufurahia na inakuwa rahisi kujifunza vitu kirahisi sana.

7) Waalimu bora na wenye motisha ya kufundisha
Waalimu wanalipwa vizuri hivyo wanafundisha kwa moyo wote na wanakuwa happy kufundisha, pia tabia za usikivu za wanafunzi uwafanya waalimu kupenda kazi zao. 

Baada ya kuelezea baadhi ya sababu tajwa hapo juu. Mimi binafsi naona serikali inaweza kufanya baadhi ya mambo hapo juu na idadi ya wanaofeli kila mwaka inaweza kupungua na kutengeneza vijana wenye upeo mkubwa kwenye mambo mengi.

  1. Serikali iwanununulie vitabu wanafunzi - kila mwanafunzi awe ana vitabu vyake kwa ajili ya masomo yote. Uwezo wa kufanya hivi tunao ata ikibidi serikali kukopa lakini kutengeneza taifa la wanafunzi wenye upeo na uelewa kwani ni azina ya vizazi vijavyo.
  2. Serikali pamoja na taasisi mbalimbali zihamasishe wanafunzi watumie muda mwingi waweze kujisomea badala ya kuhamasiha maaparty kama ya kina diamond na mambo mwengine ya starehe. Party wanafunzi wanaweza kwenda ila kipindi cha likizo ambacho watakitumia kurifresh mind zao baada ya kupiga msuli semester nzima.
  3. Serikali ikae chini na waalimu na itatue madai yao ya msingi - mwalimu ata awe anajua vitu kiasi gani lakini kama hana motisha ya kufundisha basi ni kazi bure tu.
  4. Serikali ijifunze kutoka kwa shule binafsi na serikali zinazofanya vizuri.
  5. Serikali iongeze idadi ya shule za bweni ambazo pia lazima ziwe na usimamizi mzuri na sheria ambazo inabidi zifuatwe.
  6. Wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni - hii ni pamoja na kujua mwanao mwelekeo wake ukoje toka akiwa form one hii itasaidia mzazi kuchukua hatua stahiki mapema zaidi maana mwanafunzi anaeelekea kupata sifuri huwa anajulikana toka mwanzo.


Source: http://www.wavuti.com/

No comments:

Post a Comment