KITENDO cha kuzitupa hoja zilizowasilishwa bungeni na wabunge
John Mnyika wa Chadema na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, kimesababisha chama
kikuu cha upinzani Chadema, kuamua kufanya maandamano nchi nzima ili kuwashtaki
kwa wananchi Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai.
Maandamano hayo yatatanguliwa na mkutano wa hadhara
utakaofanyika kesho Viwanja vya Temeke Mwisho, Dar es Salaam, sanjari na
kuwapokea wabunge wake wanaorejea kutoka kwenye mkutano wa Bunge uliomalizika
jana Dododma.
Chadema kimedai kuwa kanuni za bunge zina upungufu na kwamba
kitendo cha spika na naibu wake kuzima hoja za wabunge hao kinadhihirisha kuwa
viongozi hao wa mhimili huo wa taifa wameshindwa kulinda hoja zenye maslahi kwa
wananchi na wameligeuza bunge kuwa ‘kijiwe cha CCM’.
Hoja zilivyozimwa
Wiki hii, katika kikao hicho cha Bunge, Mnyika aliwasilisha hoja binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Wiki hii, katika kikao hicho cha Bunge, Mnyika aliwasilisha hoja binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, hoja hiyo ilizimwa na Ndugai, ambaye baadaye aliruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, hatua ambayo iliwafanya wabunge wote wa upinzani kusimama kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua hiyo ya Ndugai wakidai kwamba Naibu Spika huyo amevunja kanuni alizopaswa kuzisimamia.
Kitendo hicho pia kilisababisha kikao kuahirishwa kabla ya muda
uliopangwa, huku hoja ya Profesa Maghembe ya kupendekeza kuondolewa
bungeni kwa hoja ya Mnyika ikiungwa mkono na wabunge wa CCM.
Sambamba na tukio hilo Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliwasilisha hoja
binafsi akidai Serikali haina mitalaa ya elimu na kutaka Bunge kuunda
kamati teule kuchunguza udhaifu huo.
Hata hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali, badala yake Ndugai
aliunda kamati kuichunguza mitalaa hiyo kuangalia uhalali wake, kabla ya
kuthibitishwa na Bunge.
Licha ya kuwa Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kuwasilisha bungeni mitalaa hiyo juzi,
ambapo Mbatia alisema hakubaliani na mitalaa hiyo kwa maelezo kuwa
kilichowasilishwa siyo kilichoahidiwa awali na Dk Kawambwa.
Tamko la Chadema
Katika tamko la jana la Chadema mbele ya waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaira alisema :“Kwanza tutawapokea wabunge wote wa upinzani pale Ubungo na baadaye yataanza maandamano kuanzia eneo la Tazara, hadi katika Viwanja vya Temeke Mwisho, ambako utafanyika mkutano mkubwa wa hadhara.”
Tamko la Chadema
Katika tamko la jana la Chadema mbele ya waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaira alisema :“Kwanza tutawapokea wabunge wote wa upinzani pale Ubungo na baadaye yataanza maandamano kuanzia eneo la Tazara, hadi katika Viwanja vya Temeke Mwisho, ambako utafanyika mkutano mkubwa wa hadhara.”
Akizungumzia kibali cha Jeshi la Polisi, Kigaira alisema tayari
wameshatoa taarifa, uwanja wanaotarajia kufanya mkutano huo siku ya Jumapili
hautakuwa na shughuli nyingine, hivyo hakuna kisingizio chochote wala sababu za
kuzuiliwa kwa mkutano na maandamano hayo.
Alisema kilichofanywa na viongozi hao wakuu wa
Bunge, huku Serikali ikiwataka wananchi kuamini kuwa wabunge wa Chadema
ni wakorofi ni sawa na ‘’kubaka demokrasia na ubabe wa kiti cha Spika.’’
“Kazi ya Bunge ni kuibana, kuihoji Serikali na kuwapigania
wananchi, tutafanya mkutano kuwaeleza ukweli wananchi na kamwe hatuwezi
kukubali kuona spika na naibu wake wakiligeuza Bunge kuwa kijiwe cha CCM,”
alisema Kigaira.
Alisema kwa mujibu wa kanuni ya 57 na 58 ya Bunge, waziri au
mbunge, hawezi kuizima hoja ya mbunge mwenzake na kwamba kitendo cha spika
kuruhusu hoja ya Mnyika kutupwa ni kinyume na kanuni hizo.
“Tumeamua kuwapokea wabunge wote wa upinzani kwa kuwa wote
walishirikiana bungeni, lakini pia tumevialika vyama vyote vya siasa
katika kambi ya upinzani kuhudhuria maandamano na mkutano wetu,” alisema
Kigaira na kuongeza:
“Watanzania ndiyo wenye uamuzi, sisi tutakachokifanya ni
kuwaeleza ukweli tu jinsi hali ilivyo kwa sasa huko bungeni, wao ndiyo watapima
kama spika anafaa au hafai na hatimaye kuondoa umungu mtu wao.”
Kigaira alisema kuwa baada ya mkutano huo wataendelea na mikutano katika kanda
10 nchini, zinazojumuisha mikoa 30 na kwamba hadi mwishoni mwa mwezi huu
watakuwa wamemaliza mikutano yote.
“Tunataka Watanzania wachukue hatua,maana Bunge lipo kwa ajili
ya Watanzania ambao ndiyo wenye uamuzi wa kila kitu” alisema Kigaira na
kuongeza:
“Mbona wakati Spika wa Bunge ni Samwel Sitta, kulikuwa hakuna
vurugu za namna hii? Mhimili pekee unaowakilisha kilio cha wananchi ni Bunge,
lakini hivi sasa imekuwa kinyume chake.”

No comments:
Post a Comment