BAVICHA
YAANZISHA SHINDANO LA KUPATA NEMBO YAKE
Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) liko kwenye mchato wa kutafuta nembo
yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya CHADEMA. Nembo hii itakuwa
alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbali mbali
ya vijana ndani ya CHADEMA.
Katika
kufanikisha upatikanaji wa nembo, BAVICHA inatambua uwepo wa vipaji mbalimbali vikiwemo
vya ubunifu miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao baadhi yao ni wanachama na
wafuasi wapenda mabadiliko wa Chadema.
Ili
kutoa fursa kwa vijana hawa kutumia vipaji vyao na kutoa mchango wao kwa Chama
na Baraza lao, BAVICHA imeandaa shindano maalumu la ubunifu wa NEMBO YA BAVICHA
na hivyo kukaribisha wale wote ambao wangependa kushiriki kwa kubuni nembo hii.
VIGEZO MUHIMU VYA KUZINGATIWA
Kwa wale
wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hili watapaswa
kuzingaztia vigezo vifuatavyo katika ubunifu wao;
1.
Rangi zitakazotumika ni lazima ziwe zinatokana na rangi kuu za CHADEMA
2.
Nembo kuu ya Chama inaweza pia kutumika kubuni nembo ya BAVICHA
3.
Mbunifu atoe maana halisi ya nembo atakayoibuni kwa mukhtadha wa vijana na
maudhui mapana ya CHADEMA
MUDA WA SHINDANO
Muda wa
shindano hili la kupata nembo ya BAVICHA utakuwa ni mwezi mmoja yaani kuanzia tarehe
26/02/2013 - 26/03/2013. Mbunifu anaweza kuwasilisha ubunifu wake moja kwa moja
ofisi za BAVICHA zilizopo mtaa wa Togo Kinondoni – Manyanya, au kwa kutumia
barua pepe: bavicha.chadema@gmail.com
MCHAKATO WA UCHAMBUZI
Baada ya
wadau mbalimbali kuwasilisha nembo walizozibuni, Sekrataiati ya BAVICHA
itazichmbua na hatimaye kupata nembo tatu bora ambazo zitawekewa utaratibu wa
kushindanishwa na baadae kuingizwa kwenye vyombo vya kimaamuzi ili kupata nembo
moja itakayotumiwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)
ZAWADI
Kwa kuwa
shindano hili linalenga kuwapatia vijana wa CHADEMA na wasio wa CHADEMA lakini
wenye mapenzi na CHADEMA fursa ya kutumia na kuvitangaza vipaji vyao na hivyo
kutoa mchango wao katika ujenzi wa BAVICHA imara, mshindi wa shindano hili
atapewa Shilingi 500,000/= kama zawadi
na pia cheti maalumu cha kutambua mchango wake kwa BAVICHA.
WALENGWA
Walengwa
wa shindano hili ni vijana wote wa CHADEMA pamoja na wanachama na wafuasi wa
CHADEMA wenye ujuzi/kipaji cha ubunifu.
WITO
BAVICHA
inawahamasisha vijana wa CHADEMA na wote wanaopenda mabadiliko kushiriki
shindano hili ikiwa ni sehemu ya kuijenga taasisi hii ya vijana ndani ya
CHADEMA
Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Katibu Mkuu - BAVICHA
No comments:
Post a Comment