Saturday, January 26, 2013

Mtwara: Nyumba za Wabunge, Jengo la Mahakama, vyateketea

Kwa kile kinachoaminika kuwa ni kukua kwa MGOGORO WA GESI Mkoani Mtwara na Kusini kwa ujumla, usiku wa kuamkia leo Mahakama ya Mwanzo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani imeteketezwa kwa moto huku nyumba ya Mbunge Hawa Gasia ikivunjwa vioo na kuchomwa motto wakati ile ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara, ndugu Sinani ikiwa imevunjwa tu vioo. 

Chanzo hasa cha vurugu hizo haziko wazi lakini wengi wanazihusisha na sakata la GESI kwani Hawa Gasia na Sinani wamekuwa kwa Muda Mrefu wakishutumiwa kwa kuchochea na kuridhia usafirishaji wa gesi hiyo kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. Uchomaji huo wa moto uliambatana na vurugu na ulipuaji wa mabomu ya machozi kutoka kwa polisi na hadi wakafanikiwa kuzima jaribio la uchomaji wa Kituo cha Polisi cha Shangani.

Wakati huohuo kuna taarifa kutoka Masasi zikieleza nako kuibuka tukio la chomachoma mchana huu wa leo ikihusisha uchomwaji wa Offisi za Serikali, Polisi, nyumba za Wabunge na Offisi za CCM. Hali ya Masasi inaelezwa kuwa ni tete zaidi kuliko ilivyokuwa hapa Mtwara Mjini usiku wa jana ingawaje napo palikuwa na kimuhemuhe cha mabomu ya machozi kutoka kwa polisi.

Bado mpaka sasa haileweki ni nini hasa hatma ya mgogoro huu, maana kwa upande wake Serikali inaonekana kushikilia msimamo wake uleule wa kutaka kusafirisha gesi hiyo wakati upande wa raia wakiwa na msimao wao wa GESI KWANZA MAISHA BAADAYE, kwa maana kutoridhia usafirishaji wa gesi hiyo ikiwa ghafi kupelekwa Dar es salaam.

Wito wangu kwa Serikali ni kuwa, muda ni huu wa kukaa na wananchi ili kujadiliana juu ya mstakabali mzima wa tatizo hili na kutafuta suluhu. Muda ni huu kwa sababu si vyema kuacha hali iendelee kuharibika ndipo tuje baadaye tulazimike kuunda tume za watu kuchunguzwa. Si vibaya kwa Serikali kukiri au kurudi kwa raia na kusema pale ilipoteleza na kutafuta ni namna gani na ni njia ipi sahihi ya kuliendea suala hili.

Ewe Mungu! Ibariki Tanzania, Wabariki Watanzania.

Hassani Samli,
Mtwara.
+255717340671
samlihassani@yhoo.com 





Mtiririko wa taarifa mpya (updates) kutoka kwa Baraka Mfunguo 
(via blogu yake ya Mtwara Kumekucha)

  1. NEWALA: Nyumba ya Mkuchika inawaka moto -- Taarifa za redio mbao sasa  ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na kisha kupiga moto gereza. Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.
  2. Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu.
  3. Maaskari na makachero wawasili  Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
  4. Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa.  Kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto. Ofisi ya Afisa Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.
  5. Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
  6. Wakiwa katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi. 
  7. Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.
  8. Hali imeshakuwa mbaya masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa mama Ana Abdala, hapa Mtwara  mjini maduka yote eneo la soko kuu na stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.
  9. Vurugu zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu zashamiri Mabomu Kibao..Hali ni tete


Chanzo Wavuti

No comments:

Post a Comment