Tuesday, January 15, 2013

Dk. Slaa aagiza ofisi za matawi zihudumie wananchi


Viongozi wa Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) wametakiwa kuhakikisha wanatumia vyema ofisi na matawi ya chama kuhudumia wananchi ili kuongeza idadi ya wanachama.

Wito huo ulitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wakati wa uzinduzi wa ofisi na matawi katika Manispaa ya Moshi , mkoani Kilimanjaro.

Dk. Slaa alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi  ambao si waadilifu katika kukitumikia chama na kwamba hutumia baadhi ya ofisi na matawi  kwa mambo yao binafsi na kisababisha ofisi za chama kutokuwa chombo cha wananchi.

Alisema chama hicho kimekuwa kikifanya  kazi kubwa licha ya baadhi ya watu kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendesha prppaganda dhidi ya Chadema kuwa kinatishia amani ya nchi.

Mwemyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (Bavicha) Taifa, John Heche, alisema uzinduzi wa ofisi na matawi ya Chadema katika Manispaa ya Moshi ni ishara ya ukombozi wa jimbo hili, kwa ngazi zote ikiwa zitatumika kama ilivyokusudiwa.
Heche alisema, wakati umefika wa kila mwananchi kutambua haki yake na kuitetea bila kuangalia itikati za kisiasa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment