CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza mkakati wa kuhakikisha kinashinda Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ili kukiwezesha kuingia Ikulu.
Kimesema kitatekeleza hatua hiyo pia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wake wapya akiwamo mwenyekiti wa taifa, uchaguzi utakaofanyika ndani ya mwaka huu. Hata hivyo, tarehe, mwezi na ratiba kamili ya uchaguzi huo itatolewa baadaye.
Kujipanga kwa chama hicho sambamba na kujenga hoja kulithibitika pia katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwaka jana mkoani Dodoma, baada ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete kuwataka mawaziri na makada wa chama hicho kufanya mikutano ya hadhara na kutumia vyombo vya habari kujibu hoja za wapinzani, badala ya kutegemea nguvu za Jeshi la Polisi.
Katika mkutano huo, Rais Kikwete alimtaja wazi Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, akidai kuwa aliwahi kumzulia uongo pamoja na mwanaye Ridhiwani.
Rais Kikwete alisisitiza kuwa hiyo ndiyo kazi ya upinzani, akiwaita watu wazima ovyo na kudai kwamba wanasema uongo mbele ya wananchi na kwamba hata wakati mwingine hunukuu takwimu za uzushi kwenye vyombo vya habari.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho, John Mnyika katika Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, ambacho waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusikiliza, alisema watajadili ajenda mbalimbali, kubwa ikiwa ni kuweka mpango kazi wa mwaka huu wa nguvu ya umma.
Alisema pia kikao hicho kitajadili ujenzi wa chama kuanzia ngazi ya mitaa hadi taifa kwa kufanya uchaguzi wake mkuu.
“Tunaanza ujenzi wa chama kwa kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu, ili kujiimarisha zaidi katika harakati za kushinda uchaguzi mkuu ujao,” alisema Mnyika na kuongeza:
“Tunajiweka sawa na namna ambavyo tutasimamia ahadi tulizozitoa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ili kuishinikiza Serikali kutekeleza na kutatua kero za wananchi,” alisema.
“Tunajiweka sawa na namna ambavyo tutasimamia ahadi tulizozitoa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ili kuishinikiza Serikali kutekeleza na kutatua kero za wananchi,” alisema.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam alisema migogoro na vurugu zinazoendelea nchini ni matokeo ya Serikali kushindwa kulinda rasilimali zinazopatikana.
Alisema kuwa kutokana na umuhimu wa mwaka huu kuwa wa nguvu ya umma, chama hicho kimeamua kuwashirikisha wabunge wote wa chama hicho.
Alisema kuwa kutokana na umuhimu wa mwaka huu kuwa wa nguvu ya umma, chama hicho kimeamua kuwashirikisha wabunge wote wa chama hicho.
“Chadema tunaitaka Serikali kuhakikisha inakwenda mkoani Mtwara kuongea na wananchi, kuhusu mgogoro unaoendelea wa gesi ili kurejesha hali ya amani,” alisema Mnyika.
Aliongeza: “Tunaguswa na kuumizwa na kinachoendelea huko, hivyo ni wakati sasa kwa Rais Jakaya Kikwete kujitokeza na kuzungumzia mustakabali wa kile kinachoendelea Mtwara.”
Aliongeza: “Tunaguswa na kuumizwa na kinachoendelea huko, hivyo ni wakati sasa kwa Rais Jakaya Kikwete kujitokeza na kuzungumzia mustakabali wa kile kinachoendelea Mtwara.”
Kikao hicho kilianza jana na kutarajiwa kumalizika leo, huku Kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kikipangwa kufanyika kesho, ambacho kitajadili ajenda kuu ya chama hicho mwaka huu, ya nguvu ya umma.
No comments:
Post a Comment