Kwa miaka sasa CDM wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na jeshi la polisi la Tanzania linaloongozawa na IGP Said Mwema. Na kwa miaka sasa CDM imekuwa ikitoa hutuba za motomoto kilaa wanachama au mashabiki wake wanapouawa na jeshi hilo huku viongozi wake wakinyanyaswa (mnakumbuka Mbowe alivyobebwa kwa ndege ya jeshi kupelekwa Arusha?). Sasa imekuwa ni tabia kuwa CDM hawawezi kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa bila kufikiria polisi watafanya nini 'this time'.
Jeshi la Polisi (kuanzia juu hadi chini) limeendelea kuwachukulia CDM with contempt; haliamini wana haki yakupinga serikali na kwa hakika linaamini linaweza kuwanyamazisha ilimradi tu. Matokeo yake CDM wako chini ya huruma ya jeshi la polisi. Makala hii ya Februari 2012 iligusia kitu hicho hicho: Bwagamoyo: Polisi wataendelea kutuua mpaka lini? Kuna haja ya kufanyika kitu.
a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!
b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.
c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!
Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini.
No comments:
Post a Comment