Friday, September 14, 2012

CDU ya Ujerumani yakanusha kuwa mfadhili wa CHADEMA

Chama Cha CDU kimeelezea kushangazwa na na madai ya kukifadhili CDM kwa kukipatia fedha na kwamba madai hayo si ya kweli. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo juzi, Mwakilishi wa CDU, Hedrich Klaus-Juirgen alisema ushirikiano wake na CDM si wa kukipatia fedha bali ni wa ushirikiano wa kawaida katika kukijengea uwezo. Alisema CDU imekuwa na ushirikiano na vyama vyote vya siasa vilivyoko katika umoja wa vyama vya siasa vya kidemokrasia ambao CDM ni mwanachama na ndio maana vinaushirikiano katika kukijengea uwezo na si vinginevyo. Alisema hata CCM imekuwa na ushiorikiano na vyama mbali mbali duniani na kwamba kutokana na ushirikiano huo vyama hivyo pia vimekuwa vikipata misaada kama hiyo ya kukijengea uwezo.

Mwananchi

1 comment:

  1. Mwizi akiiba atakubali. Acheni ushoga na kukumbatia utengenezaji wa gongo

    ReplyDelete