Sunday, August 5, 2012

Toa maoni yako sasa kwa Mnyika (Mb) kuhusu Muswada wa marekebisho ya Fao la Kujitoa

Ndugu wafanyakazi na wadau wa hifadhi ya jamii, 

Katika mkutano wa leo, pamoja na mambo mengine napendekeza maoni yatolewe kuhusu masuala yafuatayo: 

Mosi, kuhusu taarifa ya Serikali kuwa marekebisho kuhusu kusitisha fao la kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa Mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatayomwezesha kumudu hali ya maisha uzeeni. 

Pili, kwamba mchakato wa marekebisho hayo ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka Vyama vya Wafanyakazi, Chama cha Waajiri na Serikali 

Tatu, kuwa mchakato unaendelea wa kuandaliwa kwa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama kwa kutambua tofauti za ajira, tofauti za mazingira ya kazi, tofauti za sababu za ukomo wa ajira na umuhimu wa mwanachama kunufaika na michango yake wakati angali katika ajira. 

Nne, juu ya uamuzi wa kusitisha maombi mapya ya kujitoa kwa kipindi cha miezi sita kufuatia kuanza kutumika kwa sheria mpaka pale miongozo itakapotolewa na elimu kwa wadau kuandaliwa. 

Tano, maoni mahsusi ya kuingizwa kwenye Muswada Binafsi wa Sheria kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (1), Taarifa ya Muswada huo kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (2), hati ya kuwasilisha muswada kwa dharura na hoja ya kutengua masharti kuhusu muda wa utangazaji wa Miswada ya Sheria kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka 2007). 

NAMNA YA KUCHANGIA:
 

Bofya hapa kwenda moja kwa moja kwenye blog ya Mnyika yenye "post" mahususi kwa sual ahili, baada ya mada “post” iliyoko hapo, angalia chini eneo limeandikwa “comments” bofya hapo na utafunguka ukurasa wa kuandika. Unaweza andika na jina lako, au ukawa huru wa kutoandika jina “anonymous”. Changia sasa!! 

Aidha, mwenye nyaraka yoyote anaweza kuituma kupitia jmnyika@parliament.go.tz na nakala kwenye mbungeubungo@yahoo.com; nyaraka hizo kwa ajili ya rejea ni pamoja na Social Security Ammendment Act no.5 ya mwaka 2012, Sheria za Hifadhi ya Jamii zinazohusika, Taarifa na mapendekezo yaliyowasilishwa na kupelekea kufutwa kwa mafao ya kujitoa (withdrawal benefits) na maelezo kuhusu hatua ambayo kifungu husika kiliingizwa na hatimaye kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili 2012. 

John Mnyika (Mb) 
Bungeni-Dodoma 
05/08/2012 


No comments:

Post a Comment