Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willbroad Slaa amelaani kitendo cha Rais Jakaya Kikwete cha kuidhinisha mishahara mikubwa na marupurupu kwa wabunge wakati watumishi wa kada zingine wakiambiwa serikali haina fedha za kuwalipa stahiki zao.
Amesema kuwa siku za hivi karibuni Rais Kikwete ameidhinisha malipo kwa wabunge hadi kufikia Sh milioni 11 kwa mwezi huku akishindwa kuwaongezea mishahara walimu pamoja na madaktari.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji vya kata mbalimbali za Jimbo la Morogoro kusini, mkoani hapa, Dk. Slaa aliwataka wafanyakazi kote nchini kutohamishia hasira zao kwa wananchi baada ya kushindwa kutekelezwa kwa madai yao badala yake waendelee kuibana serikali kwani ndiyo adui yao mkubwa.
Alisema kuwa anashangazwa na Rais Kikwete katika hotuba yake ya hivi karibuni wakati akihutubia Taifa na kuwaambia walimu na madaktari hakuna fedha za kuwaongezea mishahara na kuwalipa posho za mazingira magumu wala kuboresha sekta ya afya lakini ameshasaini nyongeza ya wabunge kutoka Sh. milioni 7 hadi milioni 11 kwa mwezi.
Alisema kuwa kitendo cha serikali kuendelea kukandamiza makundi mbalimbali katika jamii, hasa wafanyakazi, wakulima na wafugaji, huku ikikwepa kujadili na kushughulikia vyanzo vya manung’uniko yao ya muda mrefu kutaendelea kuiweka kitanzini hivyo kupunguza ari ya wananchi katika juhudi za kujitafutia maendeleo.
“Niliona kwenye mtandao, nikaona walimu wanatumiana meseji, ujumbe mfupi kwenye simu zao ambao kama kweli wataufanyia kazi maskini watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote watakuwa katika hali mbaya,” alisema Dk Slaa.
Aliwataka watumishi hao wa kada mbalimbali kuacha kuzihamishia hasira zao wananchi ikiwa pamoja na wanafunzi ambao hawana kosa lolote badala yake waendelee kuikataa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kushindwa kuwalipa madai yao.
“Chondechonde walimu wangu naombeni hasira zenu msizihamishie kwa watoto wetu kwani hao hawana kosa lolote, kila mtu mwenye akili timamu anajua madai yenu ni ya msingi sana, lakini adui yenu ni Rais Kikwete, anayeongoza Serikali ya CCM,” alisema Dk Slaa.
Alisema kuwa Chadema inajua uhalali wa madai ya wafanyakazi na kwamba kinachofanywa na Serikali si kwamba haina fedha za kuwalipa bali imekuwa ikipuuzia madai hayo ambayo andapo rasilimali za nchi hii zingeweza kutumiwa vizuri madai mengi yangetekelezwa.
Katika hatua nyingine, akizungumza katika mikutano ya hadhara katika vijiji mbalimbali vya Kata za Ngerengere na Makambarai, Dk. Slaa aliwaambia wananchi kuwa serikali ya CCM ambayo imetawala kwa miaka 50 imeshindwa kuwahudumia hasa kutengeneza fursa za wananchi kujitafutia na kupata maendeleo kwa ajili ya ustawi wao.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment